Siri za kifo cha Kamanda Barlow zavuja, kamanda wa Polisi Muna atajwa! Taarifa zamfikia Pinda

Benz Petrol

JF-Expert Member
Nov 22, 2012
503
225
Gazeti nimelisoma zaidi ya mara mbili sijaamini macho yangu. Hata hivyo, kilichoandikwa hapo kimefupishwa sana. Kwa kuwa kina wahariri wazoefu sina haja ya kuhofia taarifa yake. Ukweli nchi yetu iko pabaya. Wakituhumiwa kuwa wanaua waandishi wanalalamika.
Mkuu, Kama unaweza kutuwekea nakala (scanned copy) ya hili habari tafadhali!
 

mpalu

JF-Expert Member
Sep 15, 2010
2,506
2,000
Raha ya habari hii nawashauri msome JAMHURI. Lipo mitaani, lakini Dar es Salaam nakala nyingi zimenunuliwa na walioandikwa. Hii ni wiki ya pili Jamhuri linahujumiwa. Wiki iliyopita kulikuwa na habari ya Naibu Spika na madudu (vielelezo) vyote vya kina Kawambwa juu ya uamuzi wa mfumo wa kutumia kwenye mitihani ya kidato cha nne 2012. Magazeti yote Dodoma yalipigwa kiberiti. Hatufi moyo. Tutaendelea kuyafunua tu. Tunaanzia Wanapoishia Wengine!
dawa yao walilinua mnatoa remix aidha kwa kuchapa nakala zingine au kuirudia habari kwenye nakala ya wiki nyingine
 

piper

JF-Expert Member
Jan 17, 2012
3,254
1,195
inabidi ifanyike overhaul ya nguvu kwenye jeshi la polisi sasa. kila siku twasikia maovu yao mara wakamatwe na bangi, waibe vidhibiti ie, madawa ya kulevya, wakamatwe na "mambo ya kinana" nk. this is too much. polisi badala ya kukamata wahalifu, wao ndo wamekuwa wahalifu.
Wameona nao wajichukulie chao mapema, ndo nchi yetu ilipofikia mkuu, very sad
 

Ally Kombo

Verified Member
Nov 11, 2010
11,432
1,225
Sasa ni wazi kwamba aliyekuwa kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza ameuawa na genge ndani ya Polisi akiwemo Kamanda Polisi anayejulikana kwa jina la Muna, gazeti la Jamhuri limeripoti katika ukurasa wa Mbele kabisa (Nimesoma kwenye website yao Deo Balile akilalamika gazeti kununuliwa kwa jumla na watu wasiojulikana)

Kuvuja kwa siri hiyo kumetokana na mmoja wa jambazi sugu ajulikanaye kwa jina la Edward Malele kujisalimisha ktk vyombo vya ulinzi na kutoa siri zote.

Jambazi huyu aliombwa wa genge ndani ya polisi kushiriki katika mpango wa kumwua kamanda Barlow. Akakataa kwa kuwa aliwahi kumfahamu kwa karibu kamanda Barlow.

Baada ya kukataa kutekeleza agizo hilo baada ya siku chache alishtakiwa kwa kosa la ujambazi na kuswekwa Rumande.

Akiwa huko ndani ya wiki moja alisikia habari za kifo cha kamanda Barlow. Akajua akina na Muna aliowakatalia wamefanya kazi aliyoikataa yeye. Na alijua yuko mahabusu kwa sababu ya kukataa mradi huo.

Baada ya kukaa huko muda mrefu bila shitaka kueleweka wala mshataki wake huko Lupango walimua kumwaichia. Akagoma kutoka kwa sababu anajua kuwa, kwa kuwa amepelekwa huko ili kuficha siri hivyo, akitoka lazima atauawa. Baada ya muda akaamua kukubali kutoka lupango na kukimbilia kituo cha JWTZ huko Mwanza.

Huko JWTZ Alijieleza vya kutosha na wanajeshi walimwonea huruma wakampa Nauli na Tsh 10,000/= ya kula njiani ilie aende Bungeni huku wakiwa wamemkabidhi namba za simu za wabunge 2 wa upinzani ili wamsaidie.

Kutokana na kutokuelewa kwake alipokuwa anashangaa shangaa katika eneo la Bunge, alikamatwa na polisi wanalinda eneo hilo. Polisi hao wakapiga simu Dodoma central na Mwanza. Haraka haraka mwanza wakataka arudishwe mwanza kwa kuwa ni jambazi sugu.

Hata hivyo, kwa katika kurupushani hiyo taarifa zimeshameshamfikia Pinda na Nchimbi ambapo gazeti linaripoti kuwa Pinda ameagiza kijana huyo apewe ulinzi na asirudishwe Mwanza.

Hata hivyo amepelekwa kusiko julikana.

Kwa mapana zaidi soma gazeti la Jamhuri KAMA zinanunuliwa kwa kasi na watu wasiofahamika.

My take;
CCM inaua waandishi na polisi ambao imetofautiana nao. Huo ndio ukweli, watake wasitake. CCM ni janga la kitaifa. na Imeshindwa kuongoza nchi.
From this generation Bilionea.
aiseeh ! Hiyo conclution yako ndo imenikera kweli !
Hawa jamaa kama wamedhulumiana magunia ya bange ccm hapo ina husika vipi ?
...yaani umenitia kichefu chefu !
 

Jagarld

JF-Expert Member
Apr 7, 2011
1,990
2,000
Hello memberz mambo vp? Nimejiunga na hii Great thinkerz camp pamoja sana.
karibu sana japo umetukuta kwenye arobaini ya barlow,ebu nenda kuna jukwaa moja linaitwa jukwa la utambulisho kuna walinzi huko watakupatia kiti upumzike na vinywaji pia,karibu sana tena ndg.
 

Elungata

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
35,550
2,000
Lazima uwe na akili ya maiti kutetea polisi wanaofanya biashara ya bangi.
jitahidi kuwa unaangalia mambo from different perspective,kisha unatumia logic kuconclude.

Eti ameonekana akizubaazubaa bungeni hajui la kufanya?...JAMBAZI LEO AWE MZUBAIFU ,hajui pa kuanzia hadi anawafuata tena maaskari na kuanza kuropoka....coomon man.
 

alles

JF-Expert Member
Oct 14, 2006
356
0
Huko nyuma RAIA MWEMA nao walilipoti kwamba kifo cha kamanda Barlow hakitokani na sababu za mapenzi kama mwanzo polisi walivyotaka kupotosha bali sababu nyingine zinazohusisha genge la kihalifu ndani na nje ya polisi.Nahisi ndio maana mpaka leo uchunguzi wake unasuhasua.
check Raia Mwema - Makachero waibua mapya.
 

artorius

JF-Expert Member
Jan 4, 2012
757
0
Poleni wanafamilia ya ACP liberatus Barlow,sasa ni wakati wa kufuatilia kwa nguvu hili sakata
 

M.L.

Senior Member
Feb 11, 2012
185
0
Chonde chonde, natafuta website ya gazeti la Jamhuri.Siipati. Nisaidieni...chonde chonde jamani. Nataka kuiona habari nzima bila chenga wala kwi kwi!
 
Nov 17, 2011
32
0
Jamani tanzania hatuna jeshi la polisi tuna kikundi cha uhalifu,mauaji,uporaji,ugaidi kambi ya upinzani haikukosea kusema jeshi la polisi livunjwe
 

kadoda11

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
21,523
2,000
Sasa wameanzana wenyewe kwa wenyewe hatari sana,na wakuu tujuzane hasa huyu aliyefanya mpango wa kummaliza wana chuki au imekuwaje hasa,mwenye data zaidi au mwenye hiyo habari nzima iwekwe humu ndani....

Serikali imejaa magaidi tu hamna hata mmoja msafi alafu Chadema wakiwapinga mwisho wa siku wanaonekana wanatetea fujo na kuishia kuwafungulia kesi.

Mkuru nchi imemshinda maana haonyeshi uongozi wake bali nchi inaongozwa na watu wengine kabisaaaa yeye anakula kuku tu ikulu alijisemea pinda liwalo na liwe...

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
kuna mchungaji mmoja ana kakibwagizo kake ka kuombea sadaka anasema "watashindana lakini hawatashinda"
 

Maubero

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
1,531
1,500
Huko JWTZ Alijieleza vya kutosha na wanajeshi walimwonea huruma wakampa Tsh 10,000/=
Mmmmh!! 10,000/= aende bungeni???? Kutoka Mwanza???[/QUOTE]
hahahahahhh! hao waliompa hiyo hela, hawakuwa serious.
Safari ya mwanza -DODOMA kwa shs.elfu 10?
 

Songambele

JF-Expert Member
Nov 20, 2007
4,460
2,000
Sio mahaba tena! wanasiasa na hili mnajitishwa tena mbona kama lilieleweka vizuri na huyo jambazi sugu ambaye mnaamini kila alichosema. Mbona hajakataa kama yeye sio jambazi na ameua watu wangapi, ameumiza wangapi na amebaka wangapi. Siasa isipoteze uwezo wetu wa kufikiri jamani, facts and evidence zinahitajika hapa.

Sasa wameanzana wenyewe kwa wenyewe hatari sana,na wakuu tujuzane hasa huyu aliyefanya mpango wa kummaliza wana chuki au imekuwaje hasa,mwenye data zaidi au mwenye hiyo habari nzima iwekwe humu ndani....

Serikali imejaa magaidi tu hamna hata mmoja msafi alafu Chadema wakiwapinga mwisho wa siku wanaonekana wanatetea fujo na kuishia kuwafungulia kesi.

Mkuru nchi imemshinda maana haonyeshi uongozi wake bali nchi inaongozwa na watu wengine kabisaaaa yeye anakula kuku tu ikulu alijisemea pinda liwalo na liwe...

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 

makawanda

Member
Feb 26, 2013
9
20
serekali yetu inaelekea wap kila siku lazima ipate aibu kwa maovu wanayofanya. Inatisha na kama ndo ivo wananchi 2taanza kuishi kwa uoga sana wakati nchi yetu na serekali n kwa ajili ya wananchi. Tuangalie sana ndugu zangu nchi inapoelekea.
 

Ukwaju

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
11,393
2,000
Mkuu, Kama unaweza kutuwekea nakala (scanned copy) ya hili habari tafadhali!
Sawa lakini humo kwenye gazeti huyo Malele kawataja hata Madiwani wa CCM na CDM
kwenye hii Scanner itabidi uZOOM hadi 100% kuweza kuisoma vizuri au mwenye msaada (Mod) amsaidie Billionea One kuiweka vizuri maana hii ni kwa idhini ya yeye mwenyewe Manyerere Jackton namuomba aridhie na pia akishirikiana na Balile watuwekee kwenye link gazeti lao la Jamhuri maana hata gazeti la wiki iliyopita tulilikosa hivihivi
gazeti.jpg
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom