Hamis Mwalimu
New Member
- Feb 15, 2016
- 1
- 2
Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazokabiliwa na upungufu mkubwa wa madaktari katika hospitali zake zote.Upungufu huu wa wataalamu umekuwa kikwazo kikubwa katika kuimarisha upatikanaji wa huduma bora za afya katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu.
Licha ya wizara ya afya kutambua ukweli huu, kumekuwepo na sintofahamu kubwa juu ya dhamira ya kweli ya wizara hii kuboresha upatikanaji wa huduma za afya kwa watanzania masikini, baada ya siri kufichuka kuwa kuna zaidi ya madaktari 700 wametelekezwa mtaani tangu mwaka 2014 huku watanzania wakiendelea kupata huduma duni za afya na pengine kukosa huduma kabisa, na matokeo yake wagonjwa wengi wamejazana Muhimbili.
Ikumbukwe kuwa tangu aingie madarakani raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.John Pombe Magufuli mbali na mambo mengine anayoyafanya,amekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa anaboresha upatikanaji wa huduma za afya na kuhakikisha kuwa kila mtanzania ana haki ya kupata huduma bora za afya.
Lakini dhamira ya watu aliowateua kusimamia wizara hii sio njema kwani wanalifahamu suala hili na bado wamekaa kimya, huku Rais akihangaika peke yake kutatua matatizo ya mfumo wa afya nchini.