Siri yafichuka: Kumbe hakimu Arusha alishawishiwa na Mkuu wa Mkoa kukataa kumtoa Lema!

Kwa nguvu zote wapenda haki wote vita yetu kubwa iwe kwenye katiba ya nnchi hii!! Hapa ndio ulipo umuhimu wa katiba....katiba yetu ya sasa ya kila uteuzi kufanywa na raisi wa nnchi...ni tatizo....hawa wakuu wote wa mikoa ni ccm members....wewe unategemea nini ?....haya sasa shime shime moto wote kwa wapenda haki....uhamie kwenye katiba mpya ya nchi yetu ili ituondolee umwagaji wa damu kwa taifa letu kabla hatujafika huko

wadau: Nilikuwa naumiza kichwa changu bure kwamba ilikuwaje hakimu yule wa arusha alikataa kumtoa lema mahabusu huku dhamana aliisha iweka wazi. Kumbe ni msukumo wa kisiasa kutoka kwa mkuu wa mkoa. Soma sehemu ya habari hii hapa chini na utajua kwa nini sakata lote lile ambalo alikuwa la azima lilitokea -- ni bahati tu hakuna mtu aliyepoteza maisha.

Kama kawaida yao wanasiasa wa ccm hasa siku hizi huyo rc anasema uongo kabisa -- alikwenda mahakamani kufanya nini siku ile. Ni dahiri angeweza kutumia simu kumpigia simu hakimu bila ya yeye kwenda lakini simu zinaweka kumbukumbu.

Mahakimu wetu!!!! Watanzania tutakimbilia wapi? Polisi ccm, mahakimu ccm!!! Huku nchi inafilisika kwa kasi ya ajabu!!



mkuu wa mkoa wa arusha, magessa mulongo ameonya kuwa vyombo vya dola havitakubali kuwaacha baadhi ya watu kuigeuza arusha sehemu isiyotawalika akisema kuanzia sasa, yeyote atakayejaribu kuvuruga amani na utulivu kwa njia au sababu yoyote atadhibitiwa kikamilifu bila kujali cheo wala itikadi yake kisiasa.


akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, mulongo alisema: “mtu yeyote atakayechezea amani na utulivu wa arusha atakiona cha mtema kuni. Huu ni uamuzi wa kikao cha kamati ya ulinzi na usalama. Hatuwezi kukubali baadhi ya watu wafanye arusha isitawalike.”

mkuu huyo wa mkoa ambaye ndiye mwenyekiti wa kamati hiyo, pia alizungumzia tuhuma kuwa anaingilia utendaji wa baadhi ya idara ikiwamo polisi na mahakama akisema hizo ni tuhuma zisizomnyima usingizi kutekeleza wajibu na majukumu yake kiutendaji na kuongeza kwamba, uwepo wa shughuli za kisiasa ikiwamo mikutano ya hadhara ya vyama, hauwezi kuvuruga mipangilio yake ya kazi.


alitoa kauli hiyo baada ya juzi kudaiwa kuonekana maeneo ya mahakama ya hakimu mkazi arusha asubuhi kabla ya ombi la kutolewa kwa hati ya kumtoa lema mahabusu, ili awekewe dhamana kukataliwa na hakimu judith kamara na hivyo kuzua taharuki miongoni mwa viongozi, wanachama na wapenzi wa chadema.

“kweli jana (juzi) nilikwenda mahakamani kulingana na ratiba yangu ambayo haiwezi kuvurugwa na uwepo wa mbowe au shughuli zozote za kisiasa arusha. Nilikwenda kumsalimia jaji mkuu ambaye ni mmoja wa wakuu wa mihimili ya dola aliyeko hapa kwa kazi za kimahakama. Sijaenda kutoa maelekezo lema anyimwe dhamana na kusema hivyo ni dharau dhidi ya uhuru wa mahakama,” alisema mulongo.
 
So what next after that..He is starting with that style while is still new in that post.....Let me hope he will get result soon
 
hapa kuna cha kushangaza? Hii ndio kawaida ya Tanzania na ccm. Ukweli ndio huu...hii nchi ni hovyo kweli! Alafu tatizo imejazaa majinga kibao ambayo hayaoni ukweli.
 
Tatizo la haya yote ni kuwa kila kiongozi ni mwanachama wa magamba. nawaonea sana huruma baadaya ya nchii hii kukombolewa, sijui watafanyaje, maana hakutakuwa na wakuu wa mikoa wala wilaya, majaji walioteuliwa kwa kupendelewa hawatakuwepo. na hii wanayofanya sasa nod itakuwa rekodi yao wakati wanafanyiwa usaili upya.

VIVA CHADEMA!!!!!!!!!!!!!!!
 
Vyombo vya dola vimeshakuwa ni vitengo vya magamba na hivyo kupoteza imani miongoni mwa Watanzania walio wengi.

Mkuu si unakumbuka zile tik-tak zilizorukwa na samasoti ziliznpigwa na JAJI MKUU na kundi lake mwaka jana katika suala la Mgombea binafsi. Ilidaiwa kuwa Rais alitia mkono. Maji hufuata mkondo. It is not suprising though it pains, Mahakama ya Hakimu mkazi kutawaliwa na siasa mkoa kama vile Mahakama ya Rufaa ilivyotawaliwa na siasa za Ikulu.

BAK username yako inanikumbusha mwana-JF mmoja aliyekuwa initial ya BAK, jina lake halisi aliitwa Bubu Ataka Kusema.
 
Msisahau kwamba Magesa Mulongo ameletwa Arusha katika utekelezaji wa azimio la bagamoyo!!

Huyu bwana mdogo kutoka umeneja wa TTCL tawi la Sumbawanga juzi juzi tu, mpaka leo hii kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha unatarajia nini hapo....
 
Wadau: Nilikuwa naumiza kichwa changu bure kwamba ilikuwaje hakimu yule wa Arusha alikataa kumtoa Lema mahabusu huku dhamana aliisha iweka wazi. Kumbe ni msukumo wa kisiasa kutoka kwa Mkuu wa mkoa. Soma sehemu ya habari hii hapa chini na utajua kwa nini sakata lote lile ambalo alikuwa la azima lilitokea -- ni bahati tu hakuna mtu aliyepoteza maisha.

Kama kawaida yao wanasiasa wa CCM hasa siku hizi huyo RC anasema uongo kabisa -- alikwenda mahakamani kufanya nini siku ile. Ni dahiri angeweza kutumia simu kumpigia simu hakimu bila ya yeye kwenda lakini simu zinaweka kumbukumbu.

Mahakimu wetu!!!! Watanzania tutakimbilia wapi? Polisi CCM, mahakimu CCM!!! Huku nchi inafilisika kwa kasi ya ajabu!!



Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magessa Mulongo ameonya kuwa vyombo vya dola havitakubali kuwaacha baadhi ya watu kuigeuza Arusha sehemu isiyotawalika akisema kuanzia sasa, yeyote atakayejaribu kuvuruga amani na utulivu kwa njia au sababu yoyote atadhibitiwa kikamilifu bila kujali cheo wala itikadi yake kisiasa.


Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Mulongo alisema: “Mtu yeyote atakayechezea amani na utulivu wa Arusha atakiona cha mtema kuni. Huu ni uamuzi wa kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama. Hatuwezi kukubali baadhi ya watu wafanye Arusha isitawalike.”

Mkuu huyo wa mkoa ambaye ndiye mwenyekiti wa kamati hiyo, pia alizungumzia tuhuma kuwa anaingilia utendaji wa baadhi ya idara ikiwamo polisi na mahakama akisema hizo ni tuhuma zisizomnyima usingizi kutekeleza wajibu na majukumu yake kiutendaji na kuongeza kwamba, uwepo wa shughuli za kisiasa ikiwamo mikutano ya hadhara ya vyama, hauwezi kuvuruga mipangilio yake ya kazi.


Alitoa kauli hiyo baada ya juzi kudaiwa kuonekana maeneo ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha asubuhi kabla ya ombi la kutolewa kwa hati ya kumtoa Lema mahabusu, ili awekewe dhamana kukataliwa na hakimu Judith Kamara na hivyo kuzua taharuki miongoni mwa viongozi, wanachama na wapenzi wa Chadema.

“Kweli jana (juzi) nilikwenda mahakamani kulingana na ratiba yangu ambayo haiwezi kuvurugwa na uwepo wa Mbowe au shughuli zozote za kisiasa Arusha. Nilikwenda kumsalimia Jaji Mkuu ambaye ni mmoja wa wakuu wa mihimili ya dola aliyeko hapa kwa kazi za kimahakama. Sijaenda kutoa maelekezo Lema anyimwe dhamana na kusema hivyo ni dharau dhidi ya uhuru wa Mahakama,” alisema Mulongo.
Ndg yangu hivi vyombo vya dola ni taasisi za chama tawala!!!!!!!!! Hivi vyombo haviko huru vinatumika kulinda maslahi ya chama tawala, wanafanya kufaatana na maelekezo ya watawala!!!!!!!! Tunahitaji katiba mpya itakayotoa uhuru kwa vyombo vya utawala kama mahakama, Bunge vinavyo tunga na kutafsiri sheria na katiba ya nchi!!!!!!! hapa kwa sasa hakuna uhuru ni manyanyaso kwa watetea haki!!!!!!!!!
 
Nawapongeza sana wazalendo wa Arusha - Yaliyotokea na yatakayoendelea kutokea ni njama chafu na dhaifu za mfumo wa utawala ndani ya taifa letu. Wote tunadhamana ya kulinda na kutetea kwa hali zote taifa letu. Huyo mkuu wa mkoa anadhani yeye ni zaidi ya taifa? Atapita ila nchi itaendelea kuwepo tu.

CCM wasije wakajidanganya kama wao ndo wenye dhamana ya kututawala. Ni masikitiko kama hii mihimili tuliyo nayo haijitambui. Tatizo ajira nyingi hapa nchini zinatolewa sio kwa weledi alio nao mtu ila yeye ameletwa na nani! Ukiisha kujua umeipata hiyo nafasi kwa kubebwa either kiitikadi, kikabila ama vinginevyo......... lazima ulipe fadhila. Ukweli mtu ambaye anapewa dhamana ya uongozi na kusahau majukumu yake ya kazi ujue hata hiyo nafasi hakuipata kihalali...yaani hakuwa na vigezo stahili.

Ilikuwa danganya toto kuondoa matawi ya chama sehemu za kazi. Hebu angalia yaliyotokea na yanayoendelea kutokea
  1. CCM - Jeshi: Katibu itikadi .............. Gen. Shimbo,
  2. CCM - Mahakama: Katibu itikadi .............. ?,
  3. CCM - Bunge: Katibu itikadi .............. Makinda.
List ni ndefu sana ila hali hii ndo inayoangamiza taifa.
 
Dhamana yake ilikuwa wazi toka siku ile alipokamatwa akaandika Tamko lake, mahakama ikafanya kazi yake mpaka tarehe 14 ndio kesi ya yake itatajwa tena..

Mahakama inafanya kazi kwa mujibu wa sheria za nchi..

Naomba unijibu na mimi kwa nini Lema, alikataa dhamana wakati ni haki ya mshitakiwa, akangangania kwenda Jela na sasa hivi anataka kutoka?

Kwa hiyo alichokuwa anakipigania mpaka kwenda Jela kakipata?
Riz Mhs Lema nizaidi ya unavyo fikiri, wanamapinduzi woote ni watu wa kurisk maisha yao kama Mandela!!!!!!! Hata Kenya kina Laira wali sacrifice maisha yao, Kamkunji na whatever wakafika hapa walipo leo!!!!! Unadhani SA ingekombolwea vipi bila kuwa na kina Mandela?????????
 
tunazidi kuimarika kutokana na nguvu ya upinzani kuzidi kushuka.
Uchumi wa nchi hii ni wetu sote na siyo wa CCM. Watu tunajisahau, tunataka serikali itufanyie kila kila kitu.
Kwa hiyo wewe Rejao wizi unaofanywa na wanamgamba unaona ni sawa tuu wala haikugusi kwa kuwa ni mwana maghamba???????? Sisi hatutanyamaza hata kama ni vitisho vya jela mpaka ukombozi upatikane!!!!!!!!
 
Lema anakihalibu chadema analeta bangi zake tutaka umaarufu chama kimeacha oparesheni sangara ambayo inasambaza chama vijijini sasa chama kinafanya oparesheni mpa umaarufu lema.Dk slaa acha ujinga wa kushauliwa na mchumba wako josephine jenga chama acha ujinga kama umechoka kazi nenda kalee katoto ka uzeeni acha siasa za kutumika.hizo pesa unazotumia kuendeshea kesi za bwana misifa lema ni za walipa kodi watanzania wote
 
Msisahau kwamba Magesa Mulongo ameletwa Arusha katika utekelezaji wa azimio la bagamoyo!!



Hilo azimio litakuwa ni maangamizi kwa watu wa Arusha maana sasa it is Arusha unrest! J3 Lema atapelekwa mahakamani. Huko lazima risasi na mabomu yatapigwa. J3 itakayofuata Dr Slaa na Lisu watapandishwa kizimbani tena na hali itakuwa hivyohivyo.

Hii yote ni kwasababu ya ujinga tu. Wangemwachia Lema mambo yangekuwa yamekwisha na utulivu ungekuwepo. Sasa wameahirisha vurugu na kuziweka nyingine kwenye ratiba.

Sijui Mungu amewafanyaje watu wa ccm! Hawasiki, hawaoni, hawafikiri. Wamekuwa kama maiti! I'm very sorry!
 
Hapa ndipo uwa mambo yanapoharibikia kwa kuweka muonekano hii ya watawala kutokutumia picha ya kujiepusha na tafsiri mbaya toka kwa umma,Kwa Mkuu wa Mko kwenda hapo haikuwa na sababu ya kwenda hapo hakijua kuwa kuna CDM na watu wake mahakani wakiwa na vuguvugu lao.Hakika kila watendaji wa Serikali wanapovaa kofia ya Serikali matendo yao ya CCM basi utibua nyongo za wananchi wenye kuongozwa na CDM kuongeza chachu ya kuibua mtafaruku ambao hawakua na sababu.
 
habari ina maana, sababu jana watu waliishi kwa hofu na kusimama shughuli za kiuchumi na maisha kwa ujumla pale arusha.Kutokuiona hukatazwi, sababu wewe ni kipofu wa ukweli. upo kupotosha umma,wewe ndo nape magamba .Jifunze kujali masilahi ya umma, hasa utawala bora kuhusu haki inapovunjwa kwa masilahi ya ccm
 
Naomba niweke sawa moja ya kifungu cha kauli ya Mku wa mkoa Bwana Magesa Mulongo. ''Hatuwezi kukubali baadhi ya watu wafanye Arusha isitawalike kimabavu''.
 
Lema alikataa wemyewe dhamana angetokaje sasa hakimu hana kosa labda kama aliona ampe kibano zaidi ili ashike adabu siku nyingine asirudie
 
Back
Top Bottom