Siri yafichuka: Kumbe hakimu Arusha alishawishiwa na Mkuu wa Mkoa kukataa kumtoa Lema!

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
233
Wadau: Nilikuwa naumiza kichwa changu bure kwamba ilikuwaje hakimu yule wa Arusha alikataa kumtoa Lema mahabusu huku dhamana aliisha iweka wazi. Kumbe ni msukumo wa kisiasa kutoka kwa Mkuu wa mkoa. Soma sehemu ya habari hii hapa chini na utajua kwa nini sakata lote lile ambalo alikuwa la azima lilitokea -- ni bahati tu hakuna mtu aliyepoteza maisha.

Kama kawaida yao wanasiasa wa CCM hasa siku hizi huyo RC anasema uongo kabisa -- alikwenda mahakamani kufanya nini siku ile. Ni dahiri angeweza kutumia simu kumpigia simu hakimu bila ya yeye kwenda lakini simu zinaweka kumbukumbu.

Mahakimu wetu!!!! Watanzania tutakimbilia wapi? Polisi CCM, mahakimu CCM!!! Huku nchi inafilisika kwa kasi ya ajabu!!

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magessa Mulongo ameonya kuwa vyombo vya dola havitakubali kuwaacha baadhi ya watu kuigeuza Arusha sehemu isiyotawalika akisema kuanzia sasa, yeyote atakayejaribu kuvuruga amani na utulivu kwa njia au sababu yoyote atadhibitiwa kikamilifu bila kujali cheo wala itikadi yake kisiasa.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Mulongo alisema: "Mtu yeyote atakayechezea amani na utulivu wa Arusha atakiona cha mtema kuni. Huu ni uamuzi wa kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama. Hatuwezi kukubali baadhi ya watu wafanye Arusha isitawalike."

Mkuu huyo wa mkoa ambaye ndiye mwenyekiti wa kamati hiyo, pia alizungumzia tuhuma kuwa anaingilia utendaji wa baadhi ya idara ikiwamo polisi na mahakama akisema hizo ni tuhuma zisizomnyima usingizi kutekeleza wajibu na majukumu yake kiutendaji na kuongeza kwamba, uwepo wa shughuli za kisiasa ikiwamo mikutano ya hadhara ya vyama, hauwezi kuvuruga mipangilio yake ya kazi.

Alitoa kauli hiyo baada ya juzi kudaiwa kuonekana maeneo ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha asubuhi kabla ya ombi la kutolewa kwa hati ya kumtoa Lema mahabusu, ili awekewe dhamana kukataliwa na hakimu Judith Kamara na hivyo kuzua taharuki miongoni mwa viongozi, wanachama na wapenzi wa Chadema.

"Kweli jana (juzi) nilikwenda mahakamani kulingana na ratiba yangu ambayo haiwezi kuvurugwa na uwepo wa Mbowe au shughuli zozote za kisiasa Arusha. Nilikwenda kumsalimia Jaji Mkuu ambaye ni mmoja wa wakuu wa mihimili ya dola aliyeko hapa kwa kazi za kimahakama. Sijaenda kutoa maelekezo Lema anyimwe dhamana na kusema hivyo ni dharau dhidi ya uhuru wa Mahakama," alisema Mulongo.
 
Vyombo vya dola vimeshakuwa ni vitengo vya magamba na hivyo kupoteza imani miongoni mwa Watanzania walio wengi.
 
Ali forefeit right yake (lema)...... kwa hiyo inabidi aanze upya, asubiri hearing.
 
sijaona cha maana hapa...habari haina mashiko wala mwelekeo.
 
Vyombo vya dola vimeshakuwa ni vitengo vya magamba na hivyo kupoteza imani miongoni mwa Watanzania walio wengi.

BAK,
Hivi unaweza kuniambia Lema kwa nini alikataa dhamana wakati ni haki ya mshitakiwa
 
Hata mimi nilishangaa vipi hakimu anakataa kutoa hati ya kumleta Lema mahakamani huku dhamana alishaweka wazi. In fact hakimu huyo alishatoa hati za namna hivyo katika kesi kadha huko nyuoma, inakuwaje ya Lema inakataliwa?
 
sijaona cha maana hapa...habari haina mashiko wala mwelekeo.

Nakusikitia upofu wako na magamba uliyo nayo ndiyo yanakufanya huoni. Kuna siku utaona tu madudu haya chama chenu yanafanya -- iko siku nchi hii itakuwa huruu.
 
Msisahau kwamba Magesa Mulongo ameletwa Arusha katika utekelezaji wa azimio la bagamoyo!!
 
Hata mimi nilishangaa vipi hakimu anakataa kutoa hati ya kumleta Lema mahakamani huku dhamana alishaweka wazi. In fact hakimu huyo alishatoa hati za namna hivyo katika kesi kadha huko nyuoma, inakuwaje ya Lema inakataliwa?

Kwa nini usishangae Lema kungangania kwenda Jela halafu nyie mnangangania kumtoa wakati mwenyewe kaenda kwa mapenzi yake Jela?
 
Nakusikitia upofu wako na magamba uliyo nayo ndiyo yanakufanya huoni. Kuna siku utaona tu madudu haya chama chenu yanafanya -- iko siku nchi hii itakuwa huruu.

Usipoteze wakati wako na hbnuyo mtetezi wa magamba na maovu. Nchi yenyewe tayari inajiporomokea fasta. Kwa madudu tunayosikia kila dakika haiwezi kuibuka tena.
 
Nakusikitia upofu wako na magamba uliyo nayo ndiyo yanakufanya huoni. Kuna siku utaona tu madudu haya chama chenu yanafanya -- iko siku nchi hii itakuwa huruu.
ipo siku...but not now! wewe unawaza kesho, sisi tunawaza leo namna ya kuendelea kujiimarisha!
Mtabaki na mawazo hayo hayo...IKO SIKU!
 
Kwa nini usishangae Lema kungangania kwenda Jela halafu nyie mnangangania kumtoa wakati mwenyewe kaenda kwa mapenzi yake Jela?

Lakini baadaye si alikubali kutoka? baada ya kushawishiwa na viongozi wa CDM na hata wakuu wa polisi waliyomtembelea. Uko wapi wewe?
 
Kwa nini usishangae Lema kungangania kwenda Jela halafu nyie mnangangania kumtoa wakati mwenyewe kaenda kwa mapenzi yake Jela?
Magwanda kila mtu ana maamuzi yake...kila siku huwa nawafananisha na gari bovu.
Leo Zitto atasema hiki, Kesho Lissu naye atakuja na lake, Slaa naye tena ataleta lake, Regia naye hatakosekana.
Kwa kifupi chadema bado ni organization amabayo individualism imetawala!
Ni chama ambacho hakiwezi kupose threat yoyote kwa serikali.
 
ipo siku...but not now! wewe unawaza kesho, sisi tunawaza leo namna ya kuendelea kujiimarisha!
Mtabaki na mawazo hayo hayo...IKO SIKU!

Mtajiimarisha tena? Hata mkitumia mapolisi na mahakimu, siku ikifika ya kuondoka mtaondoka. Kaondoka Hosni Mubarak na gaddafi, sembuse huyo wenu mkenua meno?
 
Magwanda kila mtu ana maamuzi yake...kila siku huwa nawafananisha na gari bovu.
Leo Zitto atasema hiki, Kesho Lissu naye atakuja na lake, Slaa naye tena ataleta lake, Regia naye hatakosekana.
Kwa kifupi chadema bado ni organization amabayo individualism imetawala!
Ni chama ambacho hakiwezi kupose threat yoyote kwa serikali.

Hayo wnayosema hao ni kauli za siasa -- siyo za kutoa haki ambapo haitakiwi kuwa kigeugeu.
 
Dawa ya watu kama hawa ni uchaguzi ukifanyika magamba kushindwa, itabaki kama kumpenda mke malaya ni sawa na kujiumiza moyo.
 
Back
Top Bottom