Siri ya wabunge viti maalumu Chadema yavuja | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siri ya wabunge viti maalumu Chadema yavuja

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Kishongo, Oct 27, 2010.

 1. Kishongo

  Kishongo JF-Expert Member

  #1
  Oct 27, 2010
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ORODHA ya majina ya wateule wanaosubiri kuapishwa kuwa wabunge wa viti maalumu kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ambayo uteuzi wake ulikwama katika njia ya demokrasia za ndani ya chama hicho, imevuja ndani ya chama hicho.

  Majina 105 ya wateule hao waliopatikana kwa njia ya ushauri wa mtaalamu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam baada ya njia ya kura kushindikana, yamo ya wake, watoto na ndugu wa vigogo na viongozi wa chama hicho.

  Njia ya kura ilishindikana kutokana na kuibuka kwa makundi ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe, wakati wa uchaguzi wa wabunge hao kupitia wajumbe wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha).

  Katika uchaguzi huo, ilibainika kuwa baadhi ya wajumbe wa Baraza hilo walikuwa mamluki na baadhi ya wagombea kutoa kauli za kuulaumu uongozi kwa kutaka kuwapa ulaji wagombea wa viti maalumu wanaowataka.

  Lawama hizo zimejidhihirisha kwani katika orodha hiyo, mbali na watoto na ndugu wa vigogo wa chama hicho, pia wabunge wote wa viti maalumu wa Chadema waliomaliza muda wao, wakiwamo wanaogombea katika majimbo ya uchaguzi, wamerudishwa katika orodha hiyo na kupewa nafasi za juu.

  Wabunge waliomaliza muda wao walioko katika orodha hiyo ni Lucy Owenya ambaye ni mtoto wa mgombea ubunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo; na ni wa kwanza, jambo linalomhakikishia ubunge ikiwa uteuzi utafanyika kwa kufuata wa kwanza mpaka wa mwisho.

  Wengine ni Mhonga Ruhwanya (namba 3), Halima Mdee (5), Grace Kiwelu (9) ambaye ni mkwewe Ndesamburo, Anna Komu (13) na Susan Lyimo (10).

  Pia yumo Rose Kamil Sukum (19) ambaye ni mke wa mgombea urais wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa. Aidha, kwa mfumo huo wa Chadema, wagombea ubunge ambao wamo miongoni mwa majina hayo, watajihakikishia ‘ulaji’ bungeni endapo watashindwa katika majimbo hayo.

  Wagombea hao wa majimbo walioko katika orodha hiyo ni Mdee wa Kawe, Leticia Nyerere (16), Kwimba; Regia Mtema (11), Kilombero na Sukum, Hanang. Wengine ni Christina Lissu Mughiwa (20) na Paulina Slaa Narcis (84).

  Orodha hiyo pia imewataja Easther Matiko(2), Anna Mallac (4), Paulina Gekul (6), Conjesta Rwamlaza (7), Susan Kiwanga (8), Christowaja Mtinda (12), Mwanamrisho Abama (14), Joyce Mukya (15), Naomi Kaihula (17), Chiku Abwao (18), Raya Hamisi (21), Philipa Mturano (22) na Mariam Msabaha (23).

  Wengine ni Rachel Mashishanga (24), Sabrina Sungura (25), Rebecca Mngodo (26), Cecilia Pareso (27), Subira Waziri (28), Leticia Musore (29), Helen Kayanza (30), Rosana Chapita (31), Mona Bitakwate (32), Evarim Mpangama (33), Asha Kayumba (34), Hija Wazee (35), Mary Martin (36), Sophia Mwakagenda (37), Bupe Kyambika (38), Magreth Mangowi (39), Esther Daffi (40), Jane Pesha (41), Aikande Kwayu (42) na Helga Mchomvu (43).

  Pia orodha hiyo iliwataja walioteuliwa kuwa ni Rebecca Magwisha (44), Neema Msuya (45), Anastazia Manyanda (46), Selina Nguma (47), Bertha Matanwa (48), Christina Ngola (49), Lydia Mwaipaja (50), Zaituni Lubinza (51), Adelastela Kilindi (52), Hawa Mwaifunga (53), Loyce Iboma (54) na Rita Kanoro (55).

  Aidha wamo Monica Saile (56), Saida Othman (57), Edith Malale (58), Zainab Bakari (59), Rehema Makoba (60), Hadija Lyellu (61), Mary Komba (62), Rosale Lyimo (63), Omega Makundi (64), Marieth Chenyege (65), Veronica Ngale (66), Monica Mutasigwa (67), Judith Elyawoni (68), Rose Makara (69), Cecilian Ndossi (70) na Catherine Sakaya (71).

  Wengine ni Ruth Bujiku (72), Deshmaki Mnenei (73), Juliet Lushuli (74), Ulycess Muro (75), Matilda Kokutoma (76), Tibandelage Kalinga (77), Mtende Hassan (78), Anna Turuka (79), Gibe Masanja (80), Victoria Kihumbi (81), Sabaha Mohamed (82), Pendo Ngonyani (83), Theresia Sanga (85), Somoye Namachachi (86), Mariam Mtamike (87) na Selina Nyambalya (88).

  Wengine waliotajwa ni Zabib Vuma (89), Rose Moshi (90), Stella Masanja (91), Julie Mutashaga (92), Upendo Peneza (93), Rebecca Njiku (94), Asha Kasoni (95), Asha Akida (96), Anna Linjewile (97), Magdalena Utouh (98), Rehema Makupa (99), Mary Nyakabona (100), Happy Mgoko (101), Halima Katundu (102), Tatu Mselem(103), Salima Salum (104) na Time Suleiman (105).

  Kwa mujibu wa chanzo chetu ndani ya chama hicho, orodha hiyo iliwasilishwa Septemba 30 katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Kaimu Katibu Mkuu, John Mnyika.  [FONT=&quot]COMMENT:[/FONT]
  [FONT=&quot]
  Iwapo ndani ya Chadema hali ni hiyo, Mhe Slaa akitinga ikulu si watatoana ngeu katika kupanga safu ya cabinet, nk? Kutakuwa na serikali kweli hapo?
  [/FONT]
  [FONT=&quot]Fursa zinagawanywa kwa kuzingatia undugu, ukabila, urafiki etc - What a shame?[/FONT]
  [FONT=&quot]Zaidi ya 75% ya wateule wanatoka Kilimanjaro na Arusha - hii ndiyo falsafa ya Mwalimu Nyerere anayoihubiri Dr Slaa?
  [/FONT]
  [FONT=&quot]Mnachosema ni kingine na mnachotenda ni kingine.

  Ukabila na undugu utaimaliza Chadema ... na ni aibu kwa Tz.
  [/FONT]
  [FONT=&quot]Kwa hili, inaonekana Chadema baado saaana, hakijakomaa kisiasa, na HAWANA UWEZO wa kukamata dola.
  [/FONT]
  [FONT=&quot]Mungu iepushe Tz kuongozwa na chama cha aina hii
  [/FONT]
   
 2. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #2
  Oct 27, 2010
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Nini chanzo cha taarifa hii?
   
 3. Kishongo

  Kishongo JF-Expert Member

  #3
  Oct 27, 2010
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Gazeti Habari Leo
   
 4. Al Zagawi

  Al Zagawi JF-Expert Member

  #4
  Oct 27, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,721
  Likes Received: 242
  Trophy Points: 160
  washabiki wa chadema hawatopendezwa na habari hii na si ajabu wakaja na visingizio vya ki-CCM kuwa wanapakwa matope ili wasichaguliwe...

  kitu wanasahau ni kuwa watanzania wana macho, masikio na pua...kila iwavyo watu watajua na watachukua hatua...

  kama hivi chama kishaanza kuitwa cha wachaga na jamii nyingine kutoka kaskazini...ikiwa juhudi za makusudi hazitofanyika kupambana na hali hiyo kivitendo basi hiyo lebo itawaganda chadema na watahukumiwa kama ilivyohukumiwa CUF kuwa chama cha waislamu...bahati mbaya ni kuwa chadema kitaishia kuwa chama cha wachaga na kwa kutazama majina..cha wakristo...

  ikiwa chadema itajiachia basi huo utakuwa mwisho wake na kamwe hakitoweza kutawala kama hakina uungwaji mkono kutoka makundi yote ya kijamii katika tz...

  mwisho wa yote beneficiary wa hali zote hizi ni CCM na ni kwa mtaji huo CCM hawana wasiwasi wa ushindi na hivi vishindo vya Slaa ni kama mawimbi ya bahari tu..hayawazuii wasafiri kuendelea na safari zao...
   
 5. L

  Lorah JF-Expert Member

  #5
  Oct 27, 2010
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 1,193
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  hahahahah poor you, vipi CHICHIEM, kura za maoni walichukuliwa kina nani....
  na wa CCM viti maalumu mbona na wapenzi wa waheshimiwa wote na hatujaongea????
  vipi wakurugenzi wengi ni waleeeeeeeeeeee

  bora wangechanganya kama hao wa Chadema kila mmoja aweke wake wangeoneana aibu sasa wote nyimba ndogo za mtu mmoja ndo maana hamna kitu kinaenda kwa manispaa zetu....

  yanakula hela eti kisa kifaa cha baba...... majukumu yanaendeshwa kwa sweeeeeeetie eti hizi hela nifanyeje....

  TIME FOR CHANGE >>>>>>>>>>>>>>> wale wengineeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
   
 6. Al Zagawi

  Al Zagawi JF-Expert Member

  #6
  Oct 27, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,721
  Likes Received: 242
  Trophy Points: 160
  full of crap...hata copying ni shida...pppuuuu!!!
   
 7. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #7
  Oct 27, 2010
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,030
  Likes Received: 3,231
  Trophy Points: 280
  Tufanyaje sasa?
   
 8. ChaMtuMavi

  ChaMtuMavi JF-Expert Member

  #8
  Oct 27, 2010
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 333
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wajukuu mnasahau kuwa "VITA NI MBINU"
   
 9. Kishongo

  Kishongo JF-Expert Member

  #9
  Oct 27, 2010
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwa hiyo kama CCM wana dosari zinazofanana na hizo Chadema waige au waepuke?...HII NI AIBU SANA KWA CHADEMA.
  Toa ushauri wa kujenga chama na siyo kulinganisha uchafu wake na mapungufu ya chama kingine.
   
 10. d

  dotto JF-Expert Member

  #10
  Oct 27, 2010
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  MAJINA HAYAWEZI KUWA SIRI KWA KUWA YAKO NEC: HATA HIVYO HII TAARIFA HAIWEZI BADILISHA CHOCHOTE!! CCM:tape:
   
 11. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #11
  Oct 27, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  crap o malt
   
 12. Mpasuajipu

  Mpasuajipu JF-Expert Member

  #12
  Oct 27, 2010
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 838
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  :nono:Mie nadhani wamechaguliwa kwa sifa na siyo upendeleo hivyo si busara kuanza kuhoji undugu au ukabila. Maana hata CUF walidai chama cha waislam lakini mbona wakristo wamo pia. Jamani tuelekeze nguvu tarehe 31 kuchagua CHADEMA siyo kabila au kitu kingine. tusianze kujichanganya tukakosa mwelekeo.
   
 13. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #13
  Oct 27, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  Hawa CCM sasa wanahaha. Wameenda kuiba orodha hii kutoka NEC ili waitumie kupotosha umma.
  -Si kweli kuwa watu wa Kilimanjaro ni wengi kuiko maana nimehesabu wamekuwa 12 kati ya 105.
  -Inaonekana mgawanyo wa kanda umezingatiwa maana naona kanda zote zimo hata Z'bar
  -Bado hata hii orodha kama ni ya kweli inaweza kubadilika kwa sababu kuna wagombea wa majimbo na watashinda na
  kuondolewa katika orodha hii.

  CCM acha huu
   
 14. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #14
  Oct 27, 2010
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,402
  Likes Received: 434
  Trophy Points: 180
  First of all I wouldn't buy anything from this crap because it comes from a Newspaper which ahs already lost its credibility by reporting lies; and smear politics about the opposition. They are boot lickers of the ruling party and JK.
  Second; you just jumped on it without even asking for clarity sake;

  Third I would rather say, we have another opportunity for trying a new part and a new laerdership. THese CCM thugs kept us at bay for 50 solid years; somebody's lifetime!
  Lastly; as it is for CCM and the thugs; it will pay also the same to CHADEMA if they act like CCM thugs. Let them try these five years; only 5 years.
  CCM tried for 50 years. oUR mistake will be "NOT trying a new way" thus why we have to walk this other option, DR Slaa option!!
   
 15. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #15
  Oct 27, 2010
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,420
  Likes Received: 3,770
  Trophy Points: 280
  "Adui muombee njaa"...................Ndicho ulichokitenda
   
 16. Mongoiwe

  Mongoiwe JF-Expert Member

  #16
  Oct 27, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 521
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  Ni mtazamo wa watu, nimeangalia kwa makini naona kama Orodha imebalance kwa kanda zote
   
 17. Al Zagawi

  Al Zagawi JF-Expert Member

  #17
  Oct 27, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,721
  Likes Received: 242
  Trophy Points: 160
  u must be kidding yourself...unadhani watanzania walio wengi(kwa maana ya neno wengi..usidanganyike na hii kura yenu ya maoni ya hapa JF)...wako tayari kufanya hicho hapo juu kwenye bold??????!!!!!


  unajidanganya mkuu...
   
 18. c

  cerezo Senior Member

  #18
  Oct 27, 2010
  Joined: Sep 14, 2008
  Messages: 155
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33

  Gazeti la Udaku hilo....can't take it seriously....
   
 19. Drifter

  Drifter JF-Expert Member

  #19
  Oct 27, 2010
  Joined: Jan 4, 2010
  Messages: 1,968
  Likes Received: 670
  Trophy Points: 280
  Kwa nini wasiwe tayari ilhali Chama kinachotawala sasa kimeshajidhihirisha kwamba hakina mpango wa kujinasua toka kwenye kabali ya mafisadi na mfumo wao wa ki-mafia? Kwanza "Interested Observer" ameongeza point muhimu sana kwamba "... it will pay also the same to CHADEMA if they act like CCM thugs."

  Kwenye nchi zenye demokrasia kubadili utawala kwa kigezo cha utendaji ni muhimu sana. Wananchi hawawezi kung'ang'ania uozo kwa kuogopa kujaribu chama mbadala kinachotoa matumaini ya kurekebisha mfumo mbovu unaotupeleka kusikotakiwa. Na uzuri wa yote ni ule uwezo wa wananchi kuking'oa madarakani Chama tawala kinachojisahau - sio CCM tu; chochote kitakachofanikiwa kushika madaraka. Kwa hivi sasa DINOSAURI huyo ni CCM!
   
 20. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #20
  Oct 27, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  ..........ni la nani...............
   
Loading...