kamati ya ufundi
JF-Expert Member
- Sep 30, 2014
- 416
- 439
SIRI YA UTAJIRI WA VODACOM YATAJWA.
Zikiwa zimebaki siku mbili kufungwa kwa mauzo ya hisa za Awali kwa Kampuni ya Mawasiliano nchi Vodacom imefahamika ongezeko la ukuaji wa Mapato kwa mwaka 2016-17 kumechangiwa na wateja wa M-Pesa na Data kuwa ndiyo injini ya kukua huko kwa kasi.
Imeelezwa kukua huko kumetokana na mapato ya huduma za mawasiliano ikiwemo huduma ya muda wa maongezi ujumbe mfupi pamoja na uuzaji wa data pamoja na huduma za kifedha M-Pesa.
Imetajwa kuwa mapato ya huduma yaliongezeka kwa asilimia 1.8 kwa kipindi cha mwaka 2016-2017 ikisaidiwa na ongezeko la wateja wanaotumia kadi kwa wastani wa siku tisini.
Kwa upande wa Mapato ya Data yaliongezeka kwa asilimia 38.1 na kuchangia asilimia 12.2 ya mapato yote ya huduma katika kampuni hiyo, kukua huko kwa soko kumetokana na ongezeko la asilimia 2.8 kwa wateja wa data.
Kupitia upande wa M-Pesa mapato yalikuwa asilimia 10.5 kutokana na ongezeko la watumiaji wa M-Pesa la watumiaji zaidi ya asilimia 2.2.
Imefahamikia kampuni hiyo kupitia ubunifu wa bidhaa zake katika uhamishaji wa Fedha na malipo ya kimataifa iliyoanzishwa mwaka 2016 imeifanya kampuni hiyo kuwa Kinara kwenye soko la huduma za pesa kwa njia ya Simu ukilinganisha na mitandao mingine kwa bara la Afrika.
Chanzo hicho kiliweka wazi kuwa mapato ya M-Pesa yalichangia asilimia 24.5 ya mapato yote ukilinganishwa na Mapato ya mwaka uliopita ambayo yalikuwa ni asilimia 22.6
Imefahamika katika kipindi hichi cha MAUZO ya hisa kampuni itaendelea kujitofautisha na watoa huduma wengine kwa kuwekeza kwenye Miundombinu ya mtandao wake ili kuendelea kuwa mtandao unaotoa huduma za viwango vya juu vya mawasiliano ya kasi ya data kwa kuwavutia wateja wake katika huduma na uwekezaji katika soko la hisa nchini Tanzania.
Marina Jumanne
Habari Leo.