Siri ya ushindi wa Rais Magufuli katika vita ya kiuchumi na ufisadi ni CCM imara, madhubuti na yenye uthubutu bila kusahau Imani yake kwa CAG

FPT

JF-Expert Member
Mar 23, 2017
1,201
1,839
Kupigana vita ya kiuchumi na ufisadi inahitaji kuwa na kiongozi jasiri, mwenye hofu ya Mungu na mzalendo. Tanzania imeingia katika vita hivyo tukiongozwa na Rais Magufuli mwenye kila nia ya kushinda vita hizo kwa ajili yetu watanzania

Vita hizo ni vita dhidi ya unyonyaji na mifumo kandamizi katika jamii husika na hilo tumeliona kipndi hiki cha Uongozi wa Magufuli, wale waliokuwa wanataabika na kuteseka kwa ukandimizwaji na unyonywaji wakitetewa kwa nguvu zote na hivyo ndivyo vita ya kiuchumi na kifisadi inavyopiganwa kwa ajili yetu

Yatasemwa yote lakini uhusika wa CCM katika vita si wa kutiliwa mashaka, hii ni vita ya CCM imeanzishwa na mwana CCM na kiongozi wa CCM, uimara na umadhubuti wa CCM katika kuhakikisha nchi yetu inafuata misingi ya utawala bora ndio silaha kubwa anayoitumia Rais Magufuli kushinda vita hiyo.

Ni nani asiyeona umuhimu wa CCM katika vita hii? Kujitoa muhanga kwa mawaziri, wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya ambao ni wanaCCM ni moja ya sababu ya uhusika wa CCM katika vita hiyo. Bila CCM imara, madhubuti na yenye uthubutu ingekuwa ni ngumu kufika tulipofika na kuanzisha vita tusiyoweza kushinda ila tumewza kwa sababu CCM chini ya uongozi wa Mwenyekiti wetu wa CCM imetupa sababu ya kuweza, imewapa sababu viongozi wa CCM kuweza.

Unaachaje kutaja uhusika wa CAG katika vita hiyo? CAG amekuwa mstari wa mbele kuibua madudu mbalimbali ya kifisadi ambayo serikali ya Magufuli inapambana nayo. Je, utatenganisha vipi uzalendo wa CAG na uzalendo wa Rais Magufuli katika hali hiyo? Uzalendo wa CAG ndicho kipimo cha uzalendo wa Rais katika kupambana na ufisadi na uhujumu uchumi

Vita ya kiuchumi na kifisadi ni vita ya kila mtanzania lakini uhusika wa CCM na CAG kama wapambanaji hodari wa vita hiyo si wa kutilia mashaka. Kuwepo kwa CCM na CAG kumemrahishia Rais Magufuli kazi ambayo ingeweza kuwa ngumu.

Hii ndio CCM ambayo ipo tayari kuifia nchi na wananchi katika vita ngumu. Kwa maslahi mapana ya taifa letu na muendelezo wa hii vita, CCM itapambana kwa jasho na damu na kuhakikisha tunashinda badala ya watanzania na kuwanufaisha watanzania.

Wajibu wetu watanzania ni kuhakikisha CCM inachaguliwa kwa kura nyingi na kwa sababu vita ni muendelezo na CCM kuendelea kuwepo ndio ishara ya vita hizo kuendelea. Hatuna tumaini la kuamini hii vita itafanywa na nani badala ya CCM , tumaini pekee tulilonalo ni kwamba vita hii itafanywa na CCM pekee na iliyo imara, madhubuti na yenye uthubutu. Hii ndio CCM mpya .
 
Hilo dekio limechafuka tayari. Uhitaji kufikiri Kwa niaba ya watu timamu.
 
Sasa hapo vita gani mnapambana nayo wakati mmekaa na mafisadi wote katika chumba kimoja halafu nje mnasema mko vitani jamani mnadhani watanzania ni wajinga. Hivi wale waliotajwa kwenye ripoti ya Prof. Osoro wamehakamtwa Sasa kama bado ni vita ipi unayoizungumza.
 
Back
Top Bottom