Siri ya spika makinda kukwepa kugombea ubunge yaanikwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siri ya spika makinda kukwepa kugombea ubunge yaanikwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Felixonfellix, Feb 28, 2012.

 1. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #1
  Feb 28, 2012
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  [h=3][/h]
  [​IMG] Spika Anne Makinda
  ZIKIWA zimepita siku chache toka mbunge wa jimbo la Njombe kusini Anne Makinda ambaye ni spika wa bunge kutangaza kutogombea ubunge tena katika uchaguzi mkuu mwaka 2015,mtandao huu wa Francis Godwin Mzee Wa Matukio Daima waibuka na siri nzito za mbunge huyo kuiogopa nafasi hiyo tena.

  Baadhi ya wana CCM na mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa(Chadema) wameanika siri hiyo ya Makinda kutangazwa kuto gombea kuwa ni kutokana na kuogopa kuja kung'olewa kwa aibu katika nafasi hiyo kutokana na uwezo wake mdogo wa kuwatumikia wapiga kura wake .

  Huku wana chama wa CCM wa jimbo la Njombe kusini wakidai kuwa Makinda walianza kumchoka kutokana na kushindwa kufanya mambo ya kimaendeleo katika jimbo hilo na hivyo kusababisha jimbo hilo kuwa ngome ya chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA).

  Kwani wamedai kuwa pamoja na jimbo hilo kuongozwa na mbunge Makinda ambaye pia ni spika wa bunge ila kasi ya maendeleo katika jimbo hilo haipo na kama jimbo halina mbunge kutokana na mbunge wao huyo kuonekana kuegemea mambo ya kitaifa zaidi huku jimboni kwake mambo yanakwenda kombo .

  "Hatukutegemea jimbo la Ludewa ambalo mbunge wake Deo Filikunjombe ni kijana mchanga katika siasa kufanya mambo makubwa katika jimbo hilo kwa kipindi kifupi toka alipoingia madarakani uchaguzi wa mwaka 2010 .....huku mbunge wetu spika Makinda akishindwa hata kutengeneza barabara za jimboni kwake na kuwa barabara mbovu kuliko hata za wilaya ya Ludewa na zile za wilaya ya Makete" alisema John Sanga mkazi wa Njombe mjini

  Alisema kuwa zamani jimbo la hilo la Njombe kusini bendera za vyama vya upinzani zilikuwa za kutafuta ila ukipita leo katika jimbo hilo la Makinda utitiri wa benderea za Chadema vijijini na mjini unaweza kufikiri ni ngome ya Chadema.

  Sanga alisema kuwa hatua ya mbunge wao huyo kuwa mbunge wa kwanza wa CCM kutangaza kutogombea ni baada ya kuona hali ya upepo wa kisiasa kwake kuwa mbaya zaidi na hata akiwa katika ziara zake jimboni wananchi wamekuwa hawamkubali kivile.

  Hata hivyo alisema jimbo la Njombe kusini ambalo mbunge wake Makinda limeendelea kuwa nyuma kimaendeleo na kupitwa na jimbo la Ludewa ambalo mbunge wake Fikunjombe ameendelea kufanya mambo makubwa katika jimbo hilo ukilinganisha na mbunge wao Makinda ambaye amekuwa ni mtalii katika jimbo hilo .

  "Tunamshangaa sana mbunge wetu Makinda kwa uamuzi wake wa kutangaza kutogombea .... kiukweli hata asingetangaza msimamo wetu wapiga kura wa jimbo la Njombe kusini japo hatukuweka wazi ila ilikuwa ni kumpiga chini katika kura za maoni sisi kwa sasa mbunge wetu ni kamanda wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Njombe Deo Mwanyika ambaye amekuwa akiendelea kuhamasisha maendeleo jimboni "

  Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchugaji Msigwa alisema kuwa Makinda ni sawa na mfa maji ambaye kimsingi haishi kutapa tapa kwani kauli yake ya kuwa wabunge nusu walitaka kujiuzulu kwa sakata la posho ni uongo mtupu na kuwa yeye ametumia kisingizio cha posho kuweza kueleza nia yake ya kutogombea ubunge ila ukweli Makinda amebanwa sana na Chadema katika jimbo lake.

  Mbunge Msigwa alisema moja kati ya mikakati ya Chadema ni kuhakikisha inachukua majimbo mengi zaidi katika mkoa wa Iringa na moja kati ya majimbo ambayo ni rahisi zaidi kwa Chadema kushinda ni pamoja na jimbo hilo la Makinda ambalo wapiga kura wa jimbo hilo hawataki kabisa kusikia Makinda wala CCM.

  "Makinda asijitetee kuwa anajiuzulu kwa ajili ya kupisha wanachama wengine kuongoza ama kwa ajili ya posho ya wabunge ....anapaswa kusema wazi kuwa jimbo hilo limemshinda kutokana na kushindwa kutimiza ahadi zake kwa wapiga kura wake"

  Chanzo: Francis Godwin wa Iringa na matukio
   
 2. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #2

 3. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #3
  Feb 28, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Apumzike tu
   
 4. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #4
  Feb 28, 2012
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,549
  Likes Received: 4,675
  Trophy Points: 280
  RIP Gaucho
   
 5. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #5
  Feb 28, 2012
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Habari yenyewe imekaa ki-VINEGA VINEGA tu
   
 6. J

  JACADUOGO2. JF-Expert Member

  #6
  Feb 28, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 930
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  R. I. P Anna Makinda!
   
 7. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #7
  Feb 28, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,315
  Likes Received: 2,601
  Trophy Points: 280
  siasa mchezo mchafu
   
 8. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #8
  Feb 28, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Kwa hapa kwetu naona nafasi ya mbunge kuleta maendeleo ndogo sana wataishia kuikumbusha tu serikali lakini hawataweza kufanya mambo makubwa.
   
 9. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #9
  Feb 28, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  hivi huyu bibi kaolewa naomba anaemjua vizuri anipe details zake...
   
 10. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #10
  Feb 28, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,943
  Likes Received: 1,268
  Trophy Points: 280
  umenifanya nicheke kwa sauti ndani ya basi. Wanafanana nini na Ronaldinho, meno, macho au nywele?
   
 11. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #11
  Feb 28, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Kwani unataka kumposa?
   
 12. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #12
  Feb 28, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,943
  Likes Received: 1,268
  Trophy Points: 280
  mi napenda asife hadi atakapoona tanzania mpya
   
 13. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #13
  Feb 28, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Hajaolewa... Ila ana mtoto binti wa miaka 30 plus.
   
 14. S

  Shembago JF-Expert Member

  #14
  Feb 28, 2012
  Joined: Aug 20, 2011
  Messages: 332
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Afadhali huyo katangaza wengine wasubiri aibu 2015! Kimbunga kilichowapitia 2010 safari ijayo ni mara 10
   
 15. T

  TEMILUGODA JF-Expert Member

  #15
  Feb 28, 2012
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 1,367
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Hali halisi inaojionesha kwamba katika jamii yoyote ile ili iweze kuendelea panatakiwa pawe na kiongozi mwenye umri wa miaka 60 and above katika kila wafanyakazi 10 wenye umri kati ya miaka 20-59.Kwa mantiki hiyo nahisi Anna Makinda amegundua 2015 Mkoa wa Iringa na Njombe watafanya mabadiriko kisiasa kwa kuchagua Vijana kwenye Ubunge kwani Deo Filikunjombe ameonyesha njia na imani ya wananchi kwa vijana.WABUNGE WA KALENGA,MAKETE,NJOMBE MASH,MUFINDI KAS,KILOLO,ISMANI NANYI MTANGAZE HIVYO JAPO MNAMAJUMBA KWANI ZAHAMA LAJA.MTU UKISTAFU NENDA KAPUMZIKE LEAVE ENERGETIC AND ACTIVE CITIZENS TO SERVE ELDERS AND CHILDREN.MWINALYO!
   
 16. M

  MAJANI YA KUNDE JF-Expert Member

  #16
  Feb 28, 2012
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 213
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kwa hulka ya Wanawake wa kabila la wabena ni kashfa mtoto wa kike kzalia nyumbani bila kuolewa tafsiri yake ni kuwa hakulelewakatika misingi na tamaduni za kibena ama atakuwa anatoka kwenye ukoo wa wachawi,wavivu ,wakorofi,wagomvi na mwisho atakuwa anatoka kwenye ukoo usio na heshima ,kwa alivyo Makinda si rahisi kuolewa enzi zetu ukitaka kuoa ukionyesha nyumba Wazee watakujibu kibena ''Khakha si vwakutolwa aho have.vwakali,vwahavi ,ama vwagata.''tafsiri yake ni kuwa hao si wakuolewa hao ni wakali,wachawi,ama wavivu kufikiri hao.
   
 17. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #17
  Feb 28, 2012
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Alichokuwa anakitaka Anne ni kupata nafasi ya kuhudumiwa na serikali mpk anaingia kaburini.Nafasi hiyo ameipata ndo maana ameamua kuwaachia wengine.Hiyo inaitwa mission completed!
   
 18. p

  politiki JF-Expert Member

  #18
  Feb 28, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  chadema mna Golden chance kwa maana Makinda kutogombea maana yake ni kwamba hatafanya lolote kuanzia sasa mpaka 2015 kwahiyo hii ni nafasi yenu sasa kujiimarisha na kupita kila kona na kitabu cha ahadi za makinda na kuwakumbusha wananchi ulaghai wa CCM.
   
 19. L

  Ludewa JF-Expert Member

  #19
  Feb 28, 2012
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 215
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwani huyo Filikunjombe mnayemsifia amefanya nini cha pekee?
   
 20. n

  nketi JF-Expert Member

  #20
  Feb 28, 2012
  Joined: Feb 15, 2012
  Messages: 555
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tuzoo aliyopewa na kikwete inayolalamikiwa na watz wote sidhani km wana iringa wangeweza kumpa............haiwezekani kwani kuna wanaostahili kihalisi na sio yeye anliyestahili ili baadaye awafurahishe ccm na serikjali yake awapo bunneni tofauti na mzee wa speed and standard mh.six
   
Loading...