Siri ya Spika kuhairisha Safari yafichuka

Shukurani

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
251
11
Sitta atoboa siri kupiga 'stop' mjadala

Na Reuben Kagaruki

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bw. Samwel Sitta, ametoboa siri ya kusogeza mbele mjadala wa Ripoti ya Richmond bungeni hadi atakaporejea nchini kutoka ziara yake nchini Marekani Ijumaa ijayo.

Bw.Sitta alitoboa siri hiyo Dar es Salaam jana alipozungumza na gazeti hili kwa njia ya simu na kuhojiwa kuhusu suala hilo.

Mahojiano hayo yalifuatia madukuduku ya wananchi kuhoji kulikoni Spika huyo kuzuia mjadala huo muhimu unaosubiriwa kwa shauku na wananchi hadi atakaporudi.

Baadhi ya watu walikwenda mbali zaidi na kuhoji kwanini Bw. Sitta asimruhusu naibu wake, Bibi Anne Makinda amwakilishe kwenye ziara hiyo ya Marekani na yeye asimamie mjadala wa Richmond na Ripoti ya EPA ndani ya Bunge.

Akijibu hoja hizo, Bw. Sitta, alisema Ibara ya 84 ya Katiba inaeleza kuwa kunapokuwepo jambo gumu ni lazima Spika awepo na ndivyo alivyofanya, alitangaza uamuzi huo ili wananchi wajue.

"Ningeondoka nchini bila kuaga 'Editor' (Mhariri) wako angeandika 'Spika akimbia bomu la Richmond,' sasa ingeonekaneje ?"Alihoji Bw. Sitta huku akiangua kicheko.

Alisema hakuna sababu kwa wananchi kuwa na wasiwasi kutokana na kuahirishwa kuanza kwa mjadala huo kwa kuwa Katiba imempa mamlaka hayo.

"Ni jambo la kawaida la uwajibika Ibara ya 84 ya Katiba inasema kukiwa na jambo zito ni lazima Spika asimamie," alisema Bw. Sitta na kuongeza kuwa hicho ndicho amekifanya.

Alisema isingekuwa jambo la busara kusomwa ripoti hiyo akiwa nje ya nchi na wananchi wasingemwelewa. Alipoulizwa kama mjadala huo wa Richmond ni miongoni mwa hoja nzito ndio maana anataka awepo wakati ripoti ikijaliwa alijibu;

"Isingekuwa jambo zito ungenipigia simu kuniuliza?"Alihoji Bw. Sitta na kuongeza kuwa wabunge watakuwa na muda wa kutosha wa kujadili ripoti hiyo tofauti na wananchi wanavyodhani.

Akijibu hoja ya kutomwacha Bibi Makinda kwenda Marekani kumwakilisha ili asimamie mijadala hiyo nyeti ndani ya Bunge, alisema; "Mwaliko huu ni wa binafsi, nimealikwa mimi na sio mwaliko wa jumla," mialiko ya aina hiyo inapotolewa akatumwa mtu mwingine wanaotoa mialiko wanaweza kukataa au kuona mmedharau."

Alisema licha ya kualikwa yeye pia mkutano anaokwenda kuhudhuria ni mkubwa na kuna hafla itakayohutubiwa na Rais wa Marekani,Bw. George Bush, ambaye anatarajia kuanza ziara nchini Februari 16, mwaka huu.

Alisema pindi atakaporejea ripoti ya Richmond itajadiliwa kwa wiki nzima."Itajadiliwa kwa muda wa wiki nzima tutaanza tarehe 11 ni siku nyingi," alisema Bw. Sitta.

Alisema atarejea nchi Ijumaa wiki hii. Wiki iliyopita, Bw. Sitta aliwatangazia wabunge kuhusiana na kuahirisha kuanza kwa mjadala wa ripoti ya Richmond na EPA kutoka na safari yake na kuwataka wavute subira hadi atakaporejea.

Hatua hiyo ya Bw. Sitta ilipokelewa kwa hisia tofauti huku baadhi ya wananchi wakionekana kutoridhishwa na sababu iliyotolewa kuahirisha mjadala huo na wengine kujenga hisia kuwa kuna 'janja' iliyopangwa, kuficha ukweli wa mambo.

Wengine wamekuwa wakitafsiri hatua hiyo kuwa ni kusogeza siku mbele ili wabunge wakose muda wa kutosha kuchangia ripoti hiyo inayotarajiwa kuwa na msisimko wa aina yake.

Hatua hiyo ya Bw. Sitta pia ilionekana kumshangaza Naibu Waziri mmoja ambaye alizungumza na gazeti hili kwa sharti la jina lake kutochapishwa gazetini. "Sijui ni kwa nini Spika alisema hivyo!" Alisema naibu huyo kwa mshangao.
 
Shukurani,
Source ni ipi?
Pia sijaona hiyo siri ya kuahirisha safari.
 
Back
Top Bottom