Kamende
JF-Expert Member
- Mar 1, 2008
- 416
- 45
Amani iwe nanyi wapendwa mnaotembelea jukwaa hili tukufu.
Nimechagua kuanzisha mjadala juu ya nguvu ya CCM kutokana na jinsi ambavyo kwa sasa wanayatumia mamlaka waliyo nayo kuchezea mustakabali wa nchi. Imekwisha kuwa bayana sasa kwamba uwepo na ukubwa wa mafisadi unatokana na ukubwa wa chumba walichowekewa na CCM. Iko bayana pia kuwa ukubwa wa rushwa hapa Tanzania unatokana na namna CCM inavyoenenda na kuendeshwa. Kwa hiyo ni muhimu kabisa kujadili nguvu yake inakotoka ili kuinusuru nchi yetu na makucha ya uovu huu unaowatesa sana wananchi wetu.
Katika Biblia yuko Mtu mmoja alijulikana kama Samson. Mtu huyu alikuwa na nguvu nyingi sana. aliheshimiwa kama mnadhiri wa Mungu. ( Mtu mwenye siri/nadhiri na Mungu) Samson alifanya maajabu mengi.
Akiwa askari wa jeshi la Israel Samson alitumia mfupa wa taya la bweha kuwaua askari 1000 wenye silaha. Samson alimrarua Simba vipande vipande kuanzia mdomoni, Samson alienda msituni akakamata bweha 300 akawafunga wawili wawili na kuweka kidakwa cha moto kwenye mikia yao wakapita katika mashamba ya wafilisti wakayachoma moto yote. Samson alikutwa kwa kahaba mmoja huko Gaza, askari wa kifilisti wakafunga lango la kuingia mjini ili wamsubiri hadi asubuhi wamuue. Usiku wa manane Samson akaamka akaling'oa lango la jiji na miimo yake na komeo lake akavibeba kutoka Gaza hadi mlima unaoelekea Habron. Hapo ni kama umbali wa Ubungo na Chalinze na lango alilolibeba lapata uzito wa tani 4 hivi.
Kwa ajili ya hoja yangu kwa CCM nije kwenye siri ya nguvu za Samson. Kijana huyu Shujaa wa ajabu alimpenda binti mmoja mzuri sana wa Kifilisti aitwaye Delila. Wafilisti walimtumia Delila kuchunguza siri ya nguvu za Samson. Ndipo Samson alipotoboa siri ya nguvu zake kuwa ni nywele zake. Mungu alimwekea Samson nguvu nyingi kwenye nywele zake. Kwa nadhiri kati ya Mungu na Samson, Samson hakutakiwa kunyoa nywele zake.
Zikinyolewa tu: Kwisha kazi yake Samson.
CCM!!
Nguvu yake iko wapi?
CCM!!!:- chama pekee ambacho kina Ofisi kubwa (complex) ya makao makuu. mikoa yote ya Tanzania, kina maofisi wilaya zote, kata zote na vijiji na mitaa mingi sana Tanzania na kila ofisi ina watendaji wanaolipwa mishahara. Ni chama chenye vitegauchumi vingi sana; vikiwepo viwanja vya michezo, viwanja vya kuegeshea magari, maofisi, nk.
CCM ni chama kinachoshindaga chaguzi zote za urais toka mfumo wa vyama vingi uanzishwe nchini. Kimekuwa kikipata idadi kubwa ya wabunge kila uchaguzi. Kimefanikiwa kupata mapenzi ya wafanyabiashara wengi, wasomi wengi, na wanachuo pia. CCM inakisiwa kuwa na wanachama wasiopungua 4,000,000.
Kama mchambuzi wa siasa ni hatari kuacha mambo kana kwamba yanatokea tu yenyewe. Lazima kila jambo linalotokea lichunguzwe limetokea wapi.
Hebu tuangalie kwa kiasi chanzo cha nguvu za CCM na pengine kwa kufanya hivyo tuweze kusaidia kupatikana kwa jibu kwa nini Vyama vya Upinzani havijaweza kuiadabisha CCM.
Nguvu ya CCM ya kwanza inatokana na Uozo ulioko kwenye katiba ya nchi yetu. Katika katiba ya nchi yetu kuna vipengele vingi vinavyokinzana. Kifungu kimoja kinatoa haki na kingine kinapora hiyo haki.
Nguvu ya pili ya CCM inatokana na dharau yake kwa maelekezo ya tume ya Jaji Nyalali wakati tukiingia katika mfumo wa vyama vingi vya siasa. katika mchakato wa kuingia katika mfumo wa vyama vingi vya siasa Tume ya Jaji Nyalali ilitoka na ushauri kuwa mali/vitega uchumi vyote ambavyo CCM ilipata kabla ya kuundwa kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa viondolewe kwenye miliki ya chama na kumilikishwa serikalini. Lakini CCM ilifanikiwa kuwalazimisha watanzania waingie kwenye mfumo wa vyama vingi vya siasa bila ushauri huu kutekelezwa na hivyo kubakia kuwa chama giant mbele ya vyama vingine vya siasa.
Nguvu ya Tatu ya CCM iko kwenye kukosa kwake aibu kutumia dola kujiimarisha. CCM imekuwa ikitumia Mamlaka ya Mapato na jeshi la Polisi kupambana na wafanyabiashara wanaoonyesha kushabikia upinzani na kuwawekea kuinga wale wanaoidhamini CCM.
Nguvu ya nne inatokana na watanzania kutojua haki zao za kiraia. Watanzania wengi hawajua haki zao. Hawajui wajibu wao, majukumu yao wala hawajui mamlaka walizo nazo. Hii inainclude hata wasomi wetu wengi. Watu hawa wasiojua haki na wajibu wao wanatawalika kirahisi sana na kijinga tu. Wakipewa haki yao fulani wanafikiri wapewa fadhila.
Nguvu ya Tano ya CCM inatokana na umasikini wa Tanzania na watanzania. CCM imemasikinisha wananchi. Hawa masikini hawawezi kufurukuta wakati wa uchaguzi kwani wanapewa bakhshishi kidogo tu wanatoa ridhaa ya kutawaliwa tena. Sera mbaya za CCM na utekelezaji wake mbaya umewapa nafasi waporaji wa rasilimali za nchi kuunyonya uchumi wa nchi na kuwaacha wanachi hoi kwa umasikini. Masikini hana nguvu ya kudai haki zake: Anaweza tu kuomba chakula cha siku!
Nguvu ya Sita ya CCM iko kwenye Ndoa baina yake na wafanyabiashara wasio waadilifu. Wafanyabiashara wasiopenda kufuata taratibu takatifu za biashara wanabebwa na CCM kwa masharti ya kufandhili shughuli za chama na kuwafadhili viongozi wa chama. Wengi wa wafanyabiashara hawa ni wale wenye asili ya kiasia.
Nguvu ya saba ya CCM iko kwenye tamaa ya kila mtu kutaka kupata fursa kwa njia ya mkato. Wasomi wengi wanataka kupewa madaraka kirahisi, hawataki kuyasotea, wazazi kadhaa wanataka watoto wao wasomeshwe kirahisi kwa kupata upendeleo bila ya wao (watoto) kutunisha musuli. wafanyakazi kadhaa wanataka promotion za upendeleo: watu hawa wote hawana njia nyingine zaidi ya kujiunga na CCM.
Nguvu ya nane ya CCM iko kwenye matumizi mabaya ya dhana ya AMANI tuliyo nayo nchini na namna tunavyotunza amani za majirani zetu. CCM imekuwa ikiwarubuni kwa mafanikio makubwa wananchi kuwa yenyewe ndiyo inayolea amani ya nchi. watanzania hawajaweza kuona kuwa amani tuliyo nayo ina mushkeli. wanafikiri kuwa tuna siasa nzuri sana. hawajui kuwa wenzetu wanaopigana walikuwaga na siasa nzuri kuliko sisi hapo kabla ya kufikia kupigana. Neno amani limewapumbaza watanzania wengi. Wanaogopa hata kudai haki ya kawaida tu wakihofia kuwa kwa kufanya hivyo watasababisha amani kuvunjika.
CCM imefanikiwa kufunikiza watanzania katika jungu la ujinga kwa muda mrefu sasa.
Nimeandika hapa ili kuwaamsha wenye akili na wanamikakati wote kufanya kila linalowezekana kupambana na ghiliba za CCM vinginevyo watatawala milele. Hofu yangu si tu kule CCM kutawala millele, ila ni kwa kuwa nina uhakika kuwa CCM haiwezi kuachana na mafisadi. CCM imewekeza nguvu zake katika uovu kwa hiyo haiwezi kupambana na uovu.
Hii ndiyo sababu naichukia CCM
KIGUMU CHAMA CHA MAFISADI!!!
Ulingo uko wazi .........