Mwiba
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 7,607
- 1,744
Kwa utajiri tulionao ,hiyo mishahara na posho ni vijisenti tudogo tu, sema kitu kimoja ambacho sisi hatukielewi ni mapato ya serikali hizi za CCM ,tunayoona pale bungeni ni mapato hewa mapato halisi hayaonyweshi ndio maana ukaona wanajipangia mishahara na marupurupu minono wakijua kuwa haitahatarisha kitu, maana kama feza ingekuwa haitoshi mahesabu yao yasingekubaliana na wangeambizana kuwa tukifanya hivi mahesabu ya bajeti yatakwenda upande ,ila uhakika walionao kwa fedha inayopata Tanzania basi ni wazi kabisa kuwa wanajua wanalolifanya na jinsi ya viongozi tulionao ambao wapo kwa faida ya maslahi binafsi hilo kwao si jambo kubwa ,Tanzania Fedha ipo tena nyingi sana lakini inaliwa kijanja na kuchukuliwa na wachache.Fikiria tu marupurupu hayo yote na mshahara anaolipwa raisi vipi ataweza kuwajibika katika mambo muhimu na kuyafuatilia wakati hana wasiwasi wa kuathirika ,kifedha ,kuna ule msemo unaosema mwisho wa mwezi ananyoosha mkono tu na kupokea mshahara wake ,sasa nyinyi mkilima msilime hayamuathiri kabisa ,mkilala kiza au na taa yeye hata habari hapati ,mkikatana viungo mkiuwana ili kuibiana yeye amekaa mguu juu,malizaneni hukohuko ,mradi mwisho wa mwezi jambo la muhimu fedha yake anahamishia nje.Maana BOT haziwekeki zinaweza kuchotwa na wajanja wa makampuni hewa.