Siri ya Meya Kinondoni kugombana na Mkurugenzi

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
14,045
20,408
RC Amos Makalla amewakutanisha Meya wa manispaa ya Kinondoni Songoro Mnyonge na Mkurugenzi wake Sipora Liana. Vyombo vya habari vikaripoti kuwa mgogoro umeisha šŸ¤£.

Je, nini kiini cha mgogoro huo unaodaiwa kumalizwa na Makalla?

UTANGULIZI: Songoro mnyonge ni Diwani wa CCM akitokea Mwananyamala Msisiri, na amejenga nyumba yake kwenye bonde pale karibu na mahakama ya kinondoni na na wanao pafahamu panaitwa BWAWANI-NI ENEO LA SERIKALI, siyo kiwanja ila kavamia kajenga na nyumba yake huzungikwa na maji kila wakati na utaiona ikionyeshwa na ITV , amejenga nyingine Tegeta kwahiyo kipindi cha Mvua hukimbilia Tegeta. Ni kati ya madiwani waliofuja na wanasadikika kupiga sana fedha za miradi japo hana elimu yeyote.

Sipora Liana ndio master mind, wakala wa SATAN kuiba, kuengua, kuandika barua feki dhidi ya wapinzani, ni SUKUMA-GANG,

1. Kulitokea udanganyifu kwenye malipo ya ukusanyaji wa taka. Wenyeviti wa mitaa wakishirikiana na watendaji walikusanya fedha lakini wakatoa risiti zenye figures pungufu. Mkurugenzi akaagiza wakamatwe. Lakini katika hali ya kushangaza watendaji wakachiwa, wakabaki wenyeviti na wajumbe peke yao. Ikaonekana ni double standards. Kwanini kosa wafanye wote lakini wengine waachiwe na wengine washikiliwe?

Wenyeviti wakiwa rumande wakawalilia madiwani wao. Madiwani wakamhoji Mkurugenzi. Akajibu kuwa watendaji walipewa dhanana. Lakini jambo la kustaajabisha Wenyeviti walipoomba dhamana walinyimwa. Mkurugenzi anadaiwa kutoa maelekezo wasitoke hadi sikukuu ya Eid ipite.

Meya akaingilia kati. Akamwambia Mkurugenzi ni kosa kuweka watu ndani siku 5 bila kuwapeleka mahakani. Kama wanatuhumiwa kula pesa za taka wafunguliwe mashtaka na wapelekwe mahakamani. Otherwise wapigiwe hesabu walipe waachiwe. Kukatokea mabishano. Mgogoro ukatiwa ndimu.

2. Mwaka jana Halamshauri hiyo ilitenga Bilioni 1.5 kujenga vyumba vya madarasa ktk shule mbalimbali. Lakini Baraza la madiwani walipokagua walikuta shule nyingi ujenzi haujakamilika. Shule moja walikuta ujenzi upo kwenye hatua ya msingi. Wakatahamaki kwa sababu ujenzi huo unatakiwa kukamilika kabla mwaka mpya wa fedha yani July 1.

Wakamuuliza Mwalimu mkuu akajibu kuwa hajaletewa fedha kutoka Halmashauri. Mkurugenzi aliposikia hivyo akampigia simu mwalimu huyo na kumpa vitisho. Mwalimu akamrekodi na kumtumia Meya. Meya akamuuliza Mkurugenzi kwanini unatisha walimu? Je mwalimu huyo alifanya kosa gani kusema hajapelekewa pesa?

Mkurugenzi akaeleza kuwa Mwalimu huyo alimletea dokezo juzi, hivyo kulaumiwa kwa kutopeleka hela ni kumuonea. Lakini nyaraka zinaonesha kuwa dokezo lipo ofisi ya Mkurugenzi tangu mwezi April. Kama alipewa dokezo April lakini anasema ni "juzi" je alitaka apewe lini ili aone hajaonewa? Mgogoro ukaendelea.

3. Mkurugenzi ametoa tuhuma kuwa Halmashauri ina genge la wezi. Tuhuma hizo ni za mara kwa mara. Meya akamwambia si jambo la busara kila wakati Mkurugenzi kulalamika. Ni vizuri ataje hilo genge la wezi na tuhuma zao ili wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria. Lakini kulalamika kwamba kuna genge la wezi halafu huchukui hatua yoyote si sahihi. Mgogoro ukazidi.

4. Mkurugenzi kujihisi yupo juu ya Meya alisema "mimi natekeleza maagizo kutoka juu, kwenye mamlaka iliyoniteua". Meya akamwambia sheria ya serikali za mitaa no.8 ya mwaka 1982 inamtaka Mkurugenzi kutekeleza maagizo ya baraza la madiwani, sio mamlaka ya uteuzi. Mkurugenzi kusikia hivyo akapanic na kusema "nina sms ya maelekezo kutoka juu nitaisoma mwisho wa kikao" Meya akamuuliza unamtisha nani? Mgogoro ukazidi kukolezwa moto.

MyTake:
Ni bahati mbaya sana kwamba Wakurugenzi wengi hawajui mipaka ya utendaji wao. Kuna wakurugenzi wana-behave kama maDC, wengine kama mameya, wengine kama maDAS, wengine kama wenyeviti wa CCM wilaya. Yani kila mmoja na akili zake zinavyomtuma. Wakurugenzi wachache sana wanaowaheshimu wenyeviti wao wa halmashauri/Mameya na kujua kwamba hao ndio maboss zao. Kuna wakurugenzi hudhani wanaweza kutoa amri hata kwa vyombo vya dola . Futuhi.!

Sipora alipokua Mkurugenzi wa jiji alimsumbua sana Meya Isaya Mwita. Na kwa kuwa Isaya alitokana na Chadema basi Sipora hakumpa nidhamu anayostahili. Alimburuza na wakati mwingine walibishana hadi kwenye vikao. Kuna siku Sipora alimwambia Isaya "mimi ndiye boss wa jiji la Dar" Nikacheka sana. Nikasema kumbe huyu mama hajui Meya ni boss wake šŸ¤£.

USHAURI.
Kuna haja ya kufanya marekebisho ya sheria ili Wakurugenzi waajiriwe katika level za halmashauri. Tumpunguzie Rais mzigo wa kufanya teuzi. Nafasi za Ukurugenzi zitangazwe na Halmashauri husika, watu wenye sifa waombe. Baada ya usaili atakayeajiriwa anaripoti kwa baraza la madiwani kama mamlaka yake ya kazi na nidhamu. Awajibike kwa maslahi ya halmashauri husika. Kwa kufanya hivyo itapunguza migogoro na itasaidia halmashauri nyingi kupiga hatua za kimaendeleo.
 
#MyTake:
Ni bahati mbaya sana kwamba Wakurugenzi wengi hawajui mipaka ya utendaji wao. Kuna wakurugenzi wana-behave kama maDC, wengine kama mameya, wengine kama maDAS, wengine kama wenyeviti wa CCM wilaya. Yani kila mmoja na akili zake zinavyomtuma. Wakurugenzi wachache sana wanaowaheshimu wenyeviti wao wa halmashauri/Mameya na kujua kwamba hao ndio maboss zao. Kuna wakurugenzi hudhani wanaweza kutoa amri hata kwa vyombo vya dola . Futuhi.!
Mwenyekiti wa CCM Wilaya huyu ana madaraka gani katika Serikali anapaswa kufanya nini ?
 
Baada ya usaili atakayeajiriwa anaripoti kwa baraza la madiwani kama mamlaka yake ya kazi na nidhamu
Kama hivi tu hao madiwani wanakomba fedha nyingi za miradi je itakapofika wakaajiriwa na halimashauri itakuwaje? Naafikiana nawe kazi za ukurugenzi ziwe za kuomba na siyo kuteuana kirafiki, kiimani na kiitikadi, ila isiwe kupitia halmashauri, tutaumia sana na waombaji wataumia sana
 
Swali,hela walizokusanya kwa wananchi zilipatikana?au kila mmoja alitumia mabavu ya nafasi yake.
Waandishi wahabari waruhusiwe kushiriki vikao vya mabaraza mwanzo mwisho,ili wananchi tujue no diwani yupi yupo pamoja na shida za wananchi.
 
hata wakiripoti sukuma gang inaendelea kusema ni wapinzani hao.
 
RC Amos Makalla amewakutanisha Meya wa manispaa ya Kinondoni Songoro Mnyonge na Mkurugenzi wake Sipora Liana. Vyombo vya habari vikaripoti kuwa mgogoro umeisha šŸ¤£...
Kwakuwa tayari Mkuu wa Mkoa mpya wa Dar es Salaam Amos Makalla ( Mzee wa Masebene ya Congo DR ) ameshawapatanisha inatosha na hizi Ngojera zako za Majungu na Umbea wala hatuzitaki na baki nazo tu Rohoni Kwako na Moyoni Mwako pia sawa?
 
Mkurugenzi wa halmashauri anatakiwa aajiriwe na halmashauri.Kuteuliwa wakurugenzi na mamlaka nyingine ni dosari kubwa sana ya katiba tuliyo nayo.
 
huyo mama mkurugenzi ni tatizo sana na hajielewi kabisa ni vyema mama Samia Suluhu Hassan kampuunzisha.

Yaani kila anapokwenda kufanya kazi anagombana na madiwani ukifuatilia historia yake.

kila anapokwenda kufanya kazi lazima ataleta mgogoro
 
Usitusemee wote. Sisi wengine tunazitaka hizi ngojera.
Kwakuwa tayari Mkuu wa Mkoa mpya wa Dar es Salaam Amos Makalla ( Mzee wa Masebene ya Congo DR ) ameshawapatanisha inatosha na hizi Ngojera zako za Majungu na Umbea wala hatuzitaki na baki nazo tu Rohoni Kwako na Moyoni Mwako pia sawa?
 
Hao waliowachagua hao madiwani wakomba pesa ndio waliona wanawafaa.

Back
Top Bottom