Siri ya Marekani kuingilia Uchaguzi mkuu wa Tanzania

Albert Einstein

JF-Expert Member
Aug 24, 2017
384
560
Habari wajumbe,

Hivi karibuni Marekani kupitia kikao cha 116 cha Bunge la Congress ilipitisha Azimio la kuitaka Tanzania kufanya uchaguzi huru na haki.

Azimio hili lilibeba kichwa cha habari kinachosomeka kama ifuatavyo:

"Urging the Government of Tanzania and all parties to respect human, civil, and political rights and ensure free and fair elections in October 2020,and recognizing the importance of multi-party democracy in Tanzania."

Ukitazama kichwa cha habari cha azimio lile utaona limetaja serikali ya Tanzania na vyama vyote vya siasa nchini, lakini ajabu kilichoelezwa ndani kinailenga serikali ya Tanzania peke yake. Hapa ndipo sisi watanzania tunapaswa kujiuliza maswali, kuna siri gani imejificha?

SIRI NI HII

Ukweli ni kwamba Marekani inaumizwa sana na jinsi serikali ya Tanzania chini ya Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ilivyoweza kuyabana makampuni makubwa ya uwekezaji ( Multinational Companies kwa kifupi MNCs) mfano kampuni ya Barrick Gold Mine ambayo kwa miaka mingi yaliifanya Tanzania kama mahali pa kuchota rasilimali bure bure. Hili linawauma mno.

Kuna watu wanaweza kusema Barrick ni ya wacanada, wakatazame wanahisa (shareholders) wa Barrick ni kina nani? Fidelity Management and Research Group (FMR) ni mwanahisa mmojawapo wa Barrick. FMR inatoka Boston. Vanguard Group inatoka Pennsylvania. Haya ni baadhi ya makampuni yenye hisa Barrick.

Suala la demokrasia ni kichaka ambacho Marekani imekuwa ikitumia kuficha mipango yake. Kwa nini nasema ni kichaka? Ili kuelewa hili ijue demokrasia halisi ya Marekani kutokea Djibouti.

Nani anaifahamu Djibouti?

Djibouti inaongozwa na Rais anaitwa Ismail Omar Guelleh tangu mwaka 1999 wakati huo Rais Magufuli hata hajawa Waziri kamili wa Ujenzi. Rais Guelleh maarufu kama IOG anaongoza Djibouti mpaka leo hii kwa zaidi ya miaka 20 sasa.

Mwaka 2010 Bunge la Djibouti liliondoa ukomo wa kumruhusu Rais Guelleh kugombea kwa mara ya 3 baada ya kumaliza awamu zake mbili za miaka mitano mitano kwa mujibu wa Katiba ya Djibouti mbele ya macho ya Wamarekani hali iliyozua maandamano na watu kupigwa.

Hapa tunapaswa kujiuliza, "Kama Marekani inapigania Demokrasia, kwa nini waliacha Katiba ya Djibouti ikachezewa?"

Djibouti ni miongoni mwa nchi za Afrika ambazo demokrasia haina nafasi kabisa lakini Marekani imekaa kimya miaka yote. Tumeshawahi kujiuliza ni kwa nini?

Kama hatujui jibu basi tutazame website ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani www.state.gov kwenye kipengele cha "US-Relations with Djibouti" tutakuta maelezo haya "The Djiboutian government is supportive of US interests."

Kwamba, "Nchi ya Djibouti inaunga mkono maslahi ya Marekani" au kwa lugha nyingine "Djibouti inalinda maslahi ya Marekani." Ni maslahi gani hayo? Kujua maslahi gani hayo msome DG Jamieson hapa chini.

Akiwa Kapteni wa Jeshi la Afrika Kusini katika kamandi ya Majini (SAND) DG Jamieson aliandika andiko la kiutafiti mwaka 2009 akitathmini uwepo wa kamandi kubwa ya kijeshi ya Marekani Afrika (AFRICOM) pale nchini Djibouti.

Andiko hili lilikwenda kwa jina la "AFRICOM: A threat or opportunity for African security?" yaani "AFRICOM: ni kitisho au fursa kwa usalama wa Afrika." Wasomi wetu, vijana wa kitanzania mnaweza kulisoma ili muwaelimishe na wengine pia.

Katika hitimisho lake Kapteni Jamieson alibaini mambo makuu mawili, mosi Marekani imeweka base ile ya kijeshi ya AFRICOM kwa lengo la kuongeza ushawishi Afrika na pili kulinda maslahi ya makampuni ya mafuta ya kimarekani ambayo yanachimba mafuta arabuni na kandokando mwa bahari (Offshore) na si kitu kingine. Hivyo kwa kifupi kwa mujibu wa Jamieson AFRICOM haiisaidii Afrika katika usalama hata kidogo.

Hivyo kwa Marekani ni sahihi kwa nchi ya Djibouti kutokuwa na demokrasia kwa sababu tu inalinda maslahi ya makampuni ya Marekani.

Kimsingi "maslahi ya makampuni ya Marekani" ndiyo sababu inayofanya Marekani iipende Djibouti na kuisifia huku ikiichukia Tanzania ya sasa. Huu ndiyo ukweli.

Kuthibitisha hili rejea Azimio lililopitishwa na Bunge la Congress kuna paragraph inasomeka hivi:

Whereas some United States companies operating in Tanzania have reported harassment, corruption, and lack of respect for contracts and business operations, which threatens future United States business investment and trade partnerships;

Azimio linadai kuwa baadhi ya makampuni ya Marekani yaliyopo Tanzania yameripoti kubughudhiwa, rushwa, kutoheshimiwa kwa mikataba na uendeshaji biashara hali ambayo inatishia uwekezaji wa makampuni ya Marekani Tanzania.

Tujiulize, kudaiwa kodi ambayo ni haki yetu watanzania ni kubughudhiwa?

Au kuzuiwa kwa mchanga wenye madini yaani makinikia kwa faida ya watanzania ni kutoheshimu mikataba?

Au huku kuibuka kwa Laizer kuwa bilionea ni rushwa?

Waseme kweli!

Ukweli ni kuwa Marekani wanaumizwa sana na hizi Bilioni 700 zinazolipwa na Barrick baada ya kubanwa kimkataba. Tena inawauma zaidi kwa sababu walileta wataalamu wa majadiliano (negotiations) 40 na wakashindwa, hii inauma zaidi. Huu ndiyo ukweli mchungu ambao Marekani unawakera sana, hawataki tu kusema kweli na kamwe hawatosema hadharani.

Ukitaka kuona wameumizwa na hizi bilioni 700 zinazolipwa rejea makubaliano ya azimio lile la Congress limeeleza ifuatavyo:

(3) urges the Government of Tanzania to foster a robust, market-led business environment conducive to continued United States trade and investment in Tanzania, including respect for the legal and contractual rights of United States companies operating in Tanzania;

Kwamba, "Tanzania iiwekee Marekani mazingira mazuri ya kufanya biashara Tanzania."

Ni mazingira gani mazuri wanayotaka Marekani ikiwa Tanzania tayari inatekeleza mpango kazi wa kuweka mazingira mazuri ya kibiashara (Blueprint) ikiwemo ujenzi wa miundombinu, kupitia mikataba, na kuweka mfumo bora wa masoko tangu mwaka 2015.

Tuulizane kwa pamoja "Ni mazingira gani mazuri wanayomaanisha Marekani?"

Au mazingira ya kunufaika wao Marekani peke yao tu halafu sisi Tanzania hatunufaiki kisha baadae watuletee madawati waandike "Kutoka kwa watu wa Marekani" ilihali ni hela yetu iliyopatikana kiujanjaujanja?

Na hili napenda lieleweke wazi kuwa ni hela yetu kwa sababu ardhi yetu ndiyo inatumika kuwanufaisha raia wa Marekani.

Kuthibitisha hili kuwa ni hela zetu, Slaughter (2009) alipata kuandika "How US multinational companies strengthen the US economy" kwa Kiswahili "Ni namna gani makampuni makubwa ya Marekani yanaimarisha uchumi wa Marekani."

Katika kitabu hiki Slaughter anasema:

U.S. multinational companies are, first and foremost, American companies. As a group, U.S. multinationals perform large shares of America’s productivity-enhancing activities that lead to high average compensation for American workers.

Kwa kifupi alichoeleza Slaughter ni kuwa wafanyakazi wa Marekani wanafidiwa na hela inayopatikana kutoka katika makampuni makubwa mfano wa Barrick, je si hela yetu hiyo?

Sasa hii ndiyo sababu halisi ya kuingilia uchaguzi wa mwaka huu. Marekani imeona Tanzania imefumbua macho kutoka usingizini hivyo inajaribu kutumia kichaka cha Demokrasia ili kuhakikisha anapatikana mtu atakaelinda maslahi ya Marekani kama alivyo Guelleh pale Djibouti ili wafanyakazi wa Marekani waendelee kunufaika na madini ya watanzania.

Nasema ni demokrasia kwao ni kichaka cha kuficha mipango yao kwa sababu hata tafiti zinaonesha wazi.

Rejea utafiti uliofanywa juu ya mfumo linganifu wa Marekani uliochapishwa na Taasisi ya Kifalme ya Masuala ya Kimataifa ya London kama nilivyonukuu hapa chini:

A study of the inter-American system published by the Royal Institute of International Affairs in London concluded that, while the US pays lip service to democracy, the real commitment is to “private, capitalist enterprise.” When the rights of investors are threatened, democracy has to go; if these rights are safeguarded, killers and torturers will do just fine.

Tafsiri pana hapa ni kwamba; "Wakati Marekani inahubiri demokrasia, mkazo halisi upo kwenye makampuni yao ya kibepari. Pindi wanapoona kile wanachoita 'haki' za wawekezaji wao zikiwa hatarini basi demokrasia haina budi iondoke katika nchi hiyo, na ikiwa 'haki' hizo zitalindwa basi kiongozi anaweza kukaa madarakani atakavyo na wala hawatojali suala la kutokuwepo kwa demokrasia."

"Tujiulize ni haki zipi za makampuni ya Marekani zimebanwa kiasi kwamba wajidhihirishe waziwazi kuunga mkono mgombea fulani kwa sababu tu ameonesha kuyahakikishia makampuni ya Marekani kunufaika na rasilimali zetu?" Tujiulize kwa makini?

Au tujiulize ni makampuni gani ya sekta binafsi ambayo yanabanwa Tanzania ikiwa Taasisi ya Sekta Binafsi Nchini TPSF imeipongeza serikali ya awamu ya Tano kwa ushirikiano?

Nawashauri watanzania wenzangu tuwe makini sana tusije tukajikuta tunaingizwa walipo Libya hivi sasa kwa sababu za ulafi wa baadhi yetu.

Watu watumie wasaa huu kujiuliza, ikiwa Marekani inasapoti demokrasia Tanzania kwa nini hivi sasa imeacha Libya wakiuana ikiwa walidai hakukuwa na demokrasia? Lengo lao ni lipi?
 
Habari wajumbe,

Hivi karibuni Marekani kupitia kikao cha 116 cha Bunge la Congress ilipitisha Azimio la kuitaka Tanzania kufanya uchaguzi huru na haki..

Propaganda ya kizee sana, ni hivi 2/3 ya watanzania hawakupiga kura, na hiyo 1/3 iliyojitokeza yote haikuwapa kura wakora wa ccm. Tumeona kwa macho yetu kura za wizi, na ushenzi mwingi sana ili ccm watangazwe washindi.

Mmejua kuwa mko madarakani bila ridhaa ya umma, saa hii mnakuja na propaganda mfu ili kulinda ule ushindi wenu wa kihayawani wa juzi. Kwa taarifa yako ule haukuwa uchaguzi, bali maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura.
 
Habari wajumbe,

Hivi karibuni Marekani kupitia kikao cha 116 cha Bunge la Congress ilipitisha Azimio la kuitaka Tanzania kufanya uchaguzi huru na haki...
Safi kabisa, ila watakaokuja huku wale wa kujielewa ni wachache sana, sana sana. Kifupi, Mzungu awe wa East au West, hawezi kuishobokea nchi yako kama haina rasilimali au maliasili za kumuongezea utajiri.

Jiulize tu kwanini Malcolm X aliwaita hawa watu Devils?!
Ni mashetani ya ukweli, kwanza pesa na mali, mengine ni kifumba macho tu...
 
Wacha ujinga, inatajwa serikali kwasababu yenyewe ndio yenye dhamana ya kusimamia utawala bora na mengine yote, zile kura feki kwenye mabegi mnajidai vipofu hamkuziona, Marekani alisema yote hayo kwenye tamko lake kwasababu alishaona dalili za wazi za uminywaji wa haki za binadamu Tanzania na utawala bora.

Msilete propaganda zenu za kishamba wanataka rasilimali zetu, hao wamarekani hawategemei rasilimali zetu, tayari wana akiba zao za kutosha na hata wakitaka kuongeza kuna maeneo mengine duniani wanaweza kuzipata, msiongee uongo kama vile Tanzania ndio nchi pekee yenye mafuta na gesi duniani.

Mjifunze kukubali mkiambiwa ukweli, kuna uminywaji mkubwa sana wa haki za raia Tanzania, hilo lilianza kabla hata ya uchaguzi na mpaka baada ya uchaguzi, wapo waliobambikiwa kesi za ugaidi kwasababu tu walipigania haki zao na vyama vyao, wako jela mpaka leo bila kosa lolote, halafu mnaleta hoja zenu mfu za rasilimali, mnaonesha wazi mlivyo na tabia za ubinafsi.
 
Wacha ujinga, inatajwa serikali kwasababu yenyewe ndio yenye dhamana ya kusimamia utawala bora na mengine yote, zile kura feki kwenye mabegi mnajidai vipofu hamkuziona, Marekani alisema yote hayo kwenye tamko lake kwasababu alishaona dalili za wazi za uminywaji wa haki za binadamu Tanzania na utawala bora...

Povu lote hilo la nini? The author wasn’t trying to please you. You can write your own analysis to maximize your pleasure!
 
Povu lote hilo la nini? The author wasn’t trying to please you. You can write your own analysis to maximize your pleasure!
Nafanya navyotaka mimi sio unavyotaka wewe, you better shut up.

Msilete upotoshaji wenu wa kijinga hapa, hili sio jukwaa la wajinga, huu upuuzi mkachati kwenye magrup yenu lumumba.
 
Habari wajumbe,

Hivi karibuni Marekani kupitia kikao cha 116 cha Bunge la Congress ilipitisha Azimio la kuitaka Tanzania kufanya uchaguzi huru na haki...
Wote tunaelewa kuhusu Marekani kupigania maslahi ya marekani.

..........
Kuua
Kutesa
Kunyanyasa
Kuiba
Jaribu pia kunyanyua mdomo wako dhidi ya hayo.
 
Hoja hi naweza kusema hivi pia.
- kuna makampuni yenye hisa za wamarekani ambayo yanaoparate tz na tuliyaruhusu wenyewe.

- Mkibaka demokrasia mnaweza kuzusha vurugu nchini na kuathiri utendaji wa makampuni halali ya wa marekani yanayo operate Tz

Kwanini wa marekani waache kusisitiza democracy ili kulinda amani kwa makampuni yao na Tz kwa ujumla?
 
Habari wajumbe,

Hivi karibuni Marekani kupitia kikao cha 116 cha Bunge la Congress ilipitisha Azimio la kuitaka Tanzania kufanya uchaguzi huru na haki...
U.S. Urges Djibouti to Free Opposition Heads, Condemns Violence

By

Michael Gunn

December 24, 2015, 2:59 AM EST

The U.S. called on Djibouti to immediately release opposition leaders and condemned violence in the Horn of Africa nation, where at least seven people died this week at a religious ceremony.

“We urge the government of Djibouti to respect its citizens’ rights to freedom of expression and peaceful assembly and association, and to exercise restraint,” State Department spokesman John Kirby said in a statement.


 
Hivi wewe na huyo Jiwe wenu mna ubavu wa kupingana na Marekani akiwaamulia? Hata hao mabodyguard wa kihutu unafikiri watafua dafu. Ujue hawajaamua, wakitaka wanakuja wanambeba huyo Jiwe wenu Mara moja uliza alichofanyiwa jenerali Noriega.
Jibu kwa hoja siyo mhemko
 
Hizi shule zenu sijui ni zipi, yaani nchi yenye 22 trillion dollar uchumi ionee wivu yenye ukimwi! Du.

Yaani wewe hata miaka 1000 na jiwe wako hamuwezi kufika huko.

Tatizo lako kama ka inchi ni magonjwa, umasikini, na ujing, lol
Vyanzo vya hiyo trion 22 inatoka africa
 
Propaganda ya kizee sana, ni hivi 2/3 ya watanzania hawakupiga kura, na hiyo 1/3 iliyojitokeza yote haikuwapa kura wakora wa ccm. Tumeona kwa macho yetu kura za wizi, na ushenzi mwingi sana ili ccm watangazwe washindi...
Ushauri mzuri mngesusia kama serikali za mtaa lakini tamaa ya ruzuku imewasukuma na haya ndio matokeo yake mmekataliwa na watanzania kwa sababu ya kuhubiri udini, ukabila na vurugu zisizo na msingi!
 
Back
Top Bottom