TECHMAN
JF-Expert Member
- May 20, 2011
- 2,651
- 1,125
Nadhani hujanielewa kabisa na kwa hili la mahakama ya kadhi huta nielewa kama utasimamia misimamo ya dini yako dhidi ya dini nyingine.
Mwaka 2005 Waislam waliahidiwa kupewa mahakama ya kadhi kwa kutumia ilani iliyowekwa na awamu ya 3 iliyokua inaongozwa na Rais mkristo tena wa kanisa katoliki na waziri mkuu akiwa kanisa la kiluteri.Na makada wengi wakiwa ni maaskofu wa makanisa hayo ambao walimwita kikwete na CCM kuwa ni chaguo la mungu .Sijui huyo mungu hakuona mbali au ilikuaje!!!Leo hii maaskofu hao hao wanapinga ilani ya chama chao na mungu wao.!!Unafiki ndio stahiki yao kuitwa!!
Kuhusu kuogopwa kwa waislam nadhani sio hoja yangu.
Hoja yangu ni misingi ya kuimarisha amani.
Hatuwezi kutumia CCM kuwafanya waislam kuwa sehemu ya kupata kura tu halafu wanapodai kutekelezwa kwa ilani na ahadi iliyotolewa iwe ni kuwaogopa.
Hili suala limekua ni sababu tu ya CCM kujipatia kura na kuwagawa watanzania kwa kuwadanganya waislam kuwa chama chao kimeshaanza mchakato wa mahakama ya kadhi hiyo wakichagu chama kingine basi wajue huo mchakato utakwisha.
Leo hii kanisa ndio limekuwa adui wa mahakama ya kadhi.
Na watu badala ya kuibana serikali ili ilete maendelea kwa watu wake na kuongeza fursa za ajira zikiwemo kuanzisha mahakama ya kadhi wao wanaweka mapingamizi ya mahakama ya kadhi.
Kwa waislam wameona hiyo ndio fursa kwao yamaendeleo!!!Mnashangaa nini sasa!!
Wakristo nasema pelekeni mswada bungeni wa kupatiwa ruzuku za kuwalipa mapadri na wachungaji mishahara kwani wanatoa huduma za kijamii na kuhamasisha upendo na Amani!!
Hapa napo hujanielewa.
Kaka 1000 digits nimekuelewa sana, kama ni CCm ndo wamekuwa wakiwa ahidi na kuwa hadaa waisilamu kwa muda wote huo, basi mahakama ya kadhi iwekwe kwenye katiba ya CCM na si katika ya nchi ya Tanzania, hatuwezi tukakubali kila upumbavu wa CCM ukawagharimu Watanzania wote, CCM na viongozi wake wote waliopita na waliopo wanatakiwa kujibu hili kwa waisilamu. It has nothing to do with Tanzania as a nation.
"You can fool some people some times but you cant fool all the people all the time" Mwaka 2005( kutokana na maelezo yako). Waisilamu walidanganywa na wakakubali kuiweka serikali ya CCM madarakani, mwaka 2010, wakakubali tena wakarudia makosa, na sasa bado tunawaona wengi tu wakiunga mkono CCM iliyo wadanganya na wengi wako teyari kuipigia kura CCM tena mwaka huu.
Kwanini wewe uwaonee huruma watu wasio jionea huruma, watanzania lazima tukubali kuteseka kwaajili ya shingo zetu ngumu kwa kukubali wenyewe kuiweka CCM madarakani mwaka 2010, na kama kunaupumbavu wa maisha na wahistoria ambao watanzanzania wataufanya ni kuirudisha CCM madarakani tena mwaka huu 2015. Itakuwa ni kilio na kusaga meno.