Kuisoma ni jambo moja kuichambua je ; anaweza? Angalijua kuichambua angeilifanyia mizengwe, tushukuru uelewa wake kuwa mdogo, kwani mambo mangapi kayafanyia mizengwe aliyokuwa na uelewa nayo? Hata kura anazifanyia mizengwe. Kumbuka CAG wakati anamkabidhi taarifa hii alimwambia ni nzuri mabaya yamepungua kuliko mwaka uliopita. Akauliza swali kuwa ina maana pesa zisizoonekana zimeibiwa? CAG akamjibu wakati mwingine ni kutoweka vizuri viambatanisho vya malipo baada ya ukaguzi hua watendaji wanavipata tena viambatanisho na kutuonyesha. JK alikuwa na hakika ya kuwa taarifa ya CAG inamfagilia. Uchambuzi wa wabunge makini wa CCM na CDM kwa pamoja ndio ulioibua yaliyojili. Usimsifie bure JK kama mtu mwenye mapenzi pofu anayemwita mwenye chongo kuwa kengeza