Technician
JF-Expert Member
- Mar 30, 2010
- 841
- 222
Siri ya kuachwa Chiligati yatajwa.
*Makamba upepo si mzuri ndani ya CCM.
*Kamati kuu kukutana D'Salaam kesho.
*Msekwa naye atoboa, ajenda ni moja.
Na John Daniel.
HATIMAYE siri ya kuachwa kwa aliyekuwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika Baraza jipya la
Mawaziri, Bw. John Chiligati, imefichuka.
Siri hiyo imetajwa kuwa ni kuandaliwa kwa Bw. Chiligati kurithi mikoba wa Katibu Mkuu wa sasa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bw. Yusuf Makamba, anayetakiwa kupangiwa kazi maalum au kupumzika kabisa siasa.
Vyanzo vyetu vya habari kutoka ndani ya CCM vimeeleza kuwa Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete kupitia vikao husika vya chama hicho ana mpango kumpa nafasi hiyo, Bw. Chiligati kutokana na sababu mbalimbali kubwa ikiwa ni uwezo wa kuhimili kuweka sawa makundi yote na ushirikiano mzuri ndani ya chama.
Sababu nyingine iliyotajwa ni uzoefu wake ndani ya chama hicho pamoja na kushughulikia nyufa zilizotokana na Uchaguzi Mkuu ambapo ushindi wa CCM ulipungua ikilinganishwa na mwaka 2005.
"Mmekuwa mkiandika sana kuondolewa kwa Mhe. Makamba katika nafasi yake lakini safari hii habari hizo ni za kweli, chama kinahitaji mabadiliko ya Katibu Mkuu kama mtendaji mkuu.
Anayeandaliwa kuchukua nafasi yake muda wowote kuanzia sasa ni Mhe. Chiligati, anaonekana kuwa ni mzuri na mtu mwenye msimamo wa kati, anayemudu makundi yote, mwenye uhusiano mzuri na waandishi wa habari, anaweza kukisaidia chama kundoa nyufa za Uchaguzi Mkuu,"kilisema chanzo chetu.
Ilielezwa kwamba tayari Rais Kikwete amejiandaa kuwasilisha hoja hiyo katika kikao maalum cha Kamati Kuu (CC) kinachotarajiwa kufanyika kesho mjini Dar es Salaam kama ajenda ya mengineyo kutoka kwa Mwenyekiti.
Vyanzo vyetu vilieleza kuwa Rais Kikwete ameamua kubaki na ajenda hiyo mkononi mwake na kuhusisha wazee wachache ndani ya chama hicho bila kutaja sababu za kufanya hivyo.
Hata hivyo duru za kisiasa zimeeleza kuwa huenda uamuzi huo unatokana na kutaka kukwepa makundi na mgongano wa kimaslahi kuhusu suala hilo.
Majira ilipomtafuta Makamu Mwenyekiti wa CCM, Bw. Pius Msekwa ili kupata ufafanuzi wa suala hilo hakuwa tayari kuzungumzia taarifa hizo kwa kile alichoeleza kuwa hawezi kuzungumza kitu ambacho hakijaamuliwa na vikao rasmi vya chama hicho.
Alisema CCM si mali ya mtu mmoja hivyo maamuzi ya kumwondoa Katibu Mkuu na masuala yote yanayohusu chama hicho huamuliwa na kikao na si mtu mmoja huku akimtaka mwandishi wa habari hizi kumweleza kwanza alikopata taarifa hizo za kuenguliwa kwa Bw. Makamba.
Hata hivyo alipoulizwa kama ana taarifa za kikao cha CC cha kesho na ajenda zake, alikiri kwamba ana taarifa na kikao hicho huku akieleza kuwa kinatarajiwa kuwa na ajenda moja tu ya kupitisha majina ya wagombea umeya katika manispaa na majiji.
"Usipende kuandika habari za kufikirika, hayo ni maneno ya mitaani, hayana ukweli wowote wala hao waliokwambia hawawezi kuthibitisha, siwezi kuzungumzia jambo ambalo halijatoka kwenye kikao, maadili ya CCM ni kwamba taarifa inayotolewa ni ile iliyoamuliwa na kikao.
"Ni kweli kutakuwa na kikao cha Kamati Kuu tarehe moja Desemba hapa Dar es Saalam, tayari tumepewa ajenda ya Kamati Kuu, ni moja tu ya kupitisha majina ya wagombea umeya, kama ipo nyingine mimi sijui na si kweli, ni maneno ya uwongo tu,"alisisitiza Bw. Msekwa.
Alisema Katibu Mkuu mwenyewe, Bw. Makamba ndiye aliyewapa ajenda hiyo moja ya CC na kusisitiza kuwa baada ya Uchaguzi Mkuu hakuna kikao kilichoketi kujadili suala lolote kuhusu mabadiliko ya uongozi wa chama hicho.
Licha ya tetesi za kuenguliwa Bw. Makamba duru za kisiasa zilieleza kuwa Idara ya Usalama na Maadili pamoja na Kitengo cha Propaganda cha chama hicho, pia vinatarajiwa kukumbwa na mabadiliko makubwa kutokana na matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliopita.
Mbali ya Bw. Chiligati kutajwa kurithi mikoba ya Bw. Makamba pia Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo na Vijana Dkt. Emmanuel Nchimbi, anatajwatajwa katika nafasi hiyo.
Juhudi za kumpata Bw. Makamba ili kuzungumzia tetesi hizo zilishindikana kutokana kile kilichoelezwa kuwa amefiwa na yuko mkoani Tanga. Hata simu zake zote za mkononi hazikuweza kupatikana hadi tunakwenda mitamboni.
Kuondolewa kwa Bw. Makamba katika nafasi hiyo imekuwa gumzo la muda mrefu sasa, kwa mara ya mwisho ilidaiwa kuwa Katibu huyo alimsihi Rais Kikwete kumwacha ili akamilishe awamu ya kwanza ya ya miaka mitano kwa sababu mbalimbali.
SOURCE:MAJIRA