Siri ya hatima au kifo

Mashaurijr

JF-Expert Member
Oct 8, 2016
636
1,017
Kwenye maisha tunaishi tukiwa hatuijui hatima yetu ya maisha itakuwaje. Hili ni fumbo kubwa ambalo Mungu pekee ndiye anajua
.Wengine tunaweza kuwa na virusi vya ukimwi , kansa ,vidonda vya tumbo , kisukari au presha tukafikiri ndio hatima yetu ila hatima yetu ikawa sio hiyo labda ni ajali au kuuwawa n.k. kama wale ndugu 17 waliokufa kwa ajali korogwe Tanga usishangae huenda kati yao kuna aliyekuwa na virusi vya ukimwi, presha , kansa au gonjwa lolote hatari na alifikiri hatima yake itakuwa ni huo ugonjwa. Laiti kama hawa ndugu wangeijua hatima yao basi wasingesafiri siku ile. Ila ndio hivyo hakuna mwenye uhakika wa hatima yake nini.
Hatima haikimbiwi. Kuna watu wengi maarufu Duniani walikwisha fikwa na hatima zao wakati wasioutarajia licha ya kujipatia huduma nzuri za matibabu uangalizi mkali , ulinzi mkali lakini bado hatima haikuogopa chochote ikawafika na kuwapindua mfano mzuri ni msanii maarufu Michael Jackson aliyekuwa amepania kufikisha miaka mia akaishia kuondoka mapema bila hata kukaribia . Osama bin laden mtu aliyeitisha mpaka marekani na sio kuitisha tu na akaishambulia lakini bado hatima yake ilifika akauwawa. Hata Remi ongala aliyeimba kifo kifo nacho hakikusikia sauti yake nzuri kikamchukua.

Je? Kuna maisha baada ya hatima?. Tukijika kwenye Dini mbili Ukristo na Uislamu vyote vinaelezea maisha baada ya hatima au kifo sijajua kuhusu Dini nyingine . Dini hizi mbili zinaelezea maisha ya peponi au mbiguni na jehanam au ahera. Ila yote kwa yote ni imani hakuna udhibitisho wa kimwili japokuwa tunapaswa kuamini . Kuamini maisha mazuri baada ya hatima kidogo imepunguza woga wa kuifikia hatima na watu kuendelea kuishi kwa imani . Hata ikiwafika hatima kwao ni sawa japokuwa niwachache wanaweza kuwa na imani kali kiasi hicho.

Usipoifuata hatima yako bila kujua . Hatima yako itakufuata pia bila wewe kujua .Mfano Mdogo .Maisha yako unaweza ukawa umeishi dar es salaam miaka 20 siku moja ukapata nafasi ya kwenda mbeya kwa wiki moja . Ukiwa mbeya ukakutana na mwanamke na akakuambukiza virusi vya ukimwi na hatima yako ikawa ni virusi vya ukimwi. Hatima unakuwa umeifuata mwenyewe Mbeya na ni kama ilikuwa imepangwa tayari lazima kwenye maisha yako utaenda mbeya kuifuata hatima yako hata kama utaishi miaka mingapi Dar es salaam.

Duniani tutapita. Hatima itafika. Hakuna wa kujisifu ataishinda hatima.Tupendane na tusaidiane , tuache ubinafsi maisha ni mafupi sana kila mtu ana haki ya kufurahi kwa kipindi hiki kifupi tulicho hai kabla hatujafikwa na hatima . Pia ni vyema kuandaa maisha ya tunaowaacha watoto wetu wasiishi kwa mateso Duniani wakiisubiri hatima ili kuharibu kabisa mnyororo wa umaskini katika familia zetu
 
Ponda mali kufa kwaja, Waiter leta Gambe Dunia tunapita ....

Tomorrow never comes....
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom