SIRI ya CCM Kuudhoofisha upinzani kabla ya 2014 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

SIRI ya CCM Kuudhoofisha upinzani kabla ya 2014

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Apr 12, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Apr 12, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Habari za kuaminika kutoka kikao cha CCM Dodoma ni pamoja na ajenda ya siri ya kudhoofisha nguvu za upinzani hasa Chadema. Kuhakikisha haipenyi vijiji na hivyo CCM kuendelea kuimarisha mashina vijijini ambako kuna wapiga kura wengi wasiojua maana ya mageuzi.
   
 2. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #2
  Apr 12, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Tuna wengi tunaowafahamu na ambao wapo ndani ya vikao, hivyo kulinda siri hatuwezi kukuambia ilikovujia siri kesho watashindwa kutujulisha yanayojilia.

  Na hata Kikwete mwenyewe ameshatamka hadharani kwamba wajumbe wanajua waliyoamua kuyafanya hadi ifikapo 2014 ikiwa ni pamoja na kuongeza wanachama wapya wa ccm na kuimarisha matawi ya CCM vijijini ambako ndiko kwenye wapiga kura wengi. Soma habari ifuatayo.

  Kikwete aagiza CCM wajibu mapigo

  MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete, amewaagiza wanachama wa chama hicho wajibu mapigo ya vyama vya upinzani, na hataki wamtumie ujumbe mfupi wa simu za mkononi (sms) kuwa wametukanwa.

  Kikwete amewaambia wanaCCM kwamba, wapinzani hawana jipya, hivyo wakitukanwa nao wajibu, na amewaagiza wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho wakatekeleze kile walichokubaliana.

  "Hakuna kumtumia Rais sms kwamba jamaa wamenitukana, na wewe jibu" amesema Kikwete usiku huu mjini Dodoma wakati anafunga mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM ulioanza Jumapili.


  " Na tuliyokubaliana tunayajua, tumekubaliana, tukafanye vile tulivyokubaliana" amesema Kikwete na ameagiza kuwa yote waliyokubaliana wawe wameyatekeleza kabla ya mwaka 2014.

  Kikwete amesema, aliona CCM inahitaji kufanya mageuzi kwa kuwa aliona kuna udhaifu, na kwamba, mkutano huo umefanya maamuzi makubwa na magumu.

  "Lakini baridii kwa sababu tulijiandaa vizuri kufanya kile tulichodhamiria kukifanya" amesema Kikwete.

  "Madhumuni yangu ni kwamba, tufanye mageuzi, tujenge upya chama chetu" amesema Kikwete na kuwaeleza wajumbe hao waliyokubaliana wanayajua, wakafanye walivyokubaliana.


  Amewaagiza viongozi wa chama hicho waelekeze nguvu katika mashina na matawi kwa kuwa ndipo walipo wapiga kura wao.


  "Tunaanza safari ya kujenga upya chama chetu, tuna safari ya kujenga CCM mpya, umoja wetu, mshikamano wetu ndiyo utakaotufikisha kwenye dhamira yetu" amesema Kikwete na amewaeleza wajumbe wa mkutano huo kuwa inawezekana, kila mmoja atimize wajibu wake.


  Amesema, CCM imeamua kubadili muundo hivyo watauomba Mkutano Mkuu wa chama hicho ufanye marekebisho ya Katiba ili wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM wachaguliwe kutoka ngazi ya wilaya kwa kuwa wapo karibu na wananchi.


  Amesema, CCM pia imeamua kuunda Baraza la Ushauri litakalojumuisha wazee wastaafu wa chama hicho ili wakitaka kushiriki katika vikao wa vya juu washiriki na wakiitwa pia waende au atumwe mwakilishi, badala ya kufanya kama sasa kwa kuwa wanaitwa kushauri katika ajenda zilizoandaliwa na chama.


  Amesema, wazee katika baraza hilo wakitaka kushiriki katika mkutano wa Kamati Kuu watatoa taarifa tu na wataruhusiwa lakini pia watapaswa kuwa tayari kwenda chama kikiwahitaji.


  Amesema, kuanzia sasa, chama kitapata wanachama wapya kwa mujibu wa Katiba ya CCM, ana amekiri kwamba, chama hicho kilitetereka sana wakati wa mchakato wa kura za maoni.


  "Pale tuliteleza, limetuvuruga sana, unapata mkusanyiko ambao huna uhakika na uaminifu wao" amesema Kikwete na kubainisha kwamba, nguvu ya chama ni wanachama hivyo CCM inapaswa kuwa makini.


  Amesema, katika mkutano huo, viongozi wa CCM wamepata fursa ya kutathimini ya uchaguzi mkuu uliopita, na wamekubaliana warekebishe makosa ili chama hicho kishinde kwa kishindo mwaka 2015.


  Source: Habari leo
   
 3. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #3
  Apr 12, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Acha watu wawe na uwanja mpana zaidi kuota ndoto zenye kuwaletea wao faraja mioyoni mwao; Tanzania hakuna tena chama cha kudhoofisha vingine isipokua tu CCM chenyewe kujichimbia kaburi kwa kujipaka mafuta mgongo wa nyoka na kujishangilia ovyo kama zuzu kujivua kule gamba lenye gundi zito kiasi hiki.

  Unafiki wa Zitto wala isihesabiwe chochote kama mbinu kwani Nguvu ya Umma tayari inayo data zote na kazi ni rahisi sana hapo wala kusiwe na taabu kulitatua hivi karibuni.

  CCM wala haipo jirani na kujivua gamba mbaka kwanza kiwe kimeunga mkono kwa dhati kabisa kuundwa kwa katiba mpya ya wananchi ndipo wala mtu atakielewe, kubadilisha tu sura za watu badala ya misingi ya utawala ni kule CCM kujiangamiza jumla nchini!!!!!!

   
 4. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #4
  Apr 12, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,908
  Likes Received: 12,060
  Trophy Points: 280
  Kagamba ketu rahisi sana kukatoa hakuna haja ya kwenda dodoma ignore ili asipate exposure asahaulike then flash out.
   
 5. M

  Mr.Mak JF-Expert Member

  #5
  Apr 12, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 2,635
  Likes Received: 496
  Trophy Points: 180
  lakini ni kweli cdm haina mtaji wa wapiga kura vijijini. halafu hata hao vijana unaowakuta upinzani huko vijijini ni vijana ambao kununuliwa na mafisadi ni rahisi mno.
   
 6. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #6
  Apr 12, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Its a good note for chadema to work on
   
 7. K

  Kifoi JF-Expert Member

  #7
  Apr 12, 2011
  Joined: May 12, 2007
  Messages: 836
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 60
  Hakuna siri yoyote siri kubwa ni TUME ya Uchaguzi kuwa NI CCM watupu hii ndio siri. jegine ni porojo baada ya mbege
   
 8. d

  demokrasia Member

  #8
  Apr 12, 2011
  Joined: Apr 6, 2011
  Messages: 52
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  huko vijijini wanakataka kwenda watakuwa wanaenda kuhonga watu hela kama kawaida yao.
   
 9. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #9
  Apr 12, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  The beautyful ones are not yet born in ccm (A.k. Armah) They have just put new wine in an old bottle. Blanders will persist and ccm will eventually die a natural death. CCM Have reached a point of no return. Wanaosema chadema haina wapiga kura vijijini watuambie majimbo ya maswa mashariki na magaribi,meatu, ukerewe,karatu, kwa kahigi, biharamulo,mbozi, na mpanda,yako wapi?
   
 10. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #10
  Apr 12, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  CCM haiwezi kuudhoofisha upinzani kwa sababu kwa sababu zifuatazo ambazi pia nimezipost kwenye thread yangu ya NYOKA AKIJUA VUA GAMBA ANAKUWA CHURA?.

  Kwa mtu yo yote mwenye ufahamu wa kawaida anajua kuwa, Nyoka akijivua gamba hawi Chura au Mjusi, kama anasuma wala sumu yake haipungui makali. Sana sana anajipanga kutenda yale yale ya siku zote kwa kasi zaidi.Habadili chakula, wala habidili tabia, umri wa kuishi au kitu chochote. Ni yule yule Nyoka hata jina lake halibadiliki. Kilichobadilika ni ngozi tu imekuwa nzuri zaidi, mpya zaidi inayovutia.

  CCM wamebadilisha sura za secretariet, wamebadili pia baadhi ya wajumbe wa kamati kuu. Hivi kumweka mkama nafasi ya makamba kunaleta nafuu gani kwa watazania? Hawa wote walikuwa ni viongozi wa CCM na Serikali yake kabla ya uteuzi wa jana. Mkama alikuwa katibu wa wizara ya afya miaka kadhaa akikumbwa na tuhuma kibao zilizohusu dawa ya ukimwi. Magazeti yaliandika sana tu. Chiligati alikuwa waziri wa ardhi. Hakufanya lolote zaidi ya kuharibu na kurudisha nyuma kazi nzuri aliyoanzisha magufuli katika wizara ile. Je, kubadili secretariet inawafaidije watanzania? Au itawasaidiaje CCM? Ina punguzaje mikataba ya feki kama IPTL. Je, itaibuka na kauli ya kutokulipa Downs? Itatoa tamko la kuridhia mabadiliko makubwa ktk mswada wa mabadiliko ya katiba yanayopigiwa kelele kila kona wakati mkiti wake ni Rais JK aliyeuleta mswada huo? Au kumtosa Fisadi mkubwa kuliko wote RA kwenye CC wakati mfanyakazi wake wa zamani/Swahiba wake ni waziri wa Nishati na Madini (Ngeleja) kwa kupigiwa debe na RA mwenyewe kunaleta jipya gani?
  HII ni danganya toto, tatizo la CCM ni la kimfumo, halibadiliswi kwa kubadili sura za watedaji.
  My take,
  Maisha bora hayawezi kuletwa na Chama kile kile, chenye sera zile zile kikiongozwa na Kikwete yule yule aliyeleta ombwe la uongozi ktk nchi yetu, eti kwa kubadili nafasi za baadhi ya viongozi na kuwa hadaa wananchi kuwa kimejivua gamba CCM kingali na sumu ile ile ya Ufisadi
   
 11. M

  Mkwe21 JF-Expert Member

  #11
  Apr 12, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,847
  Likes Received: 464
  Trophy Points: 180
  Umenena!! Ni wale wale wanajifanya Kutuzuga!! Kwani Mukama na Makamba wote si wamekuwa katika safu ya uongozi wa Jiji? Angalia uozo unaolikumba jiji la Dar es salaam!! Tutegemee kipi kipya kwa watu Hawa? "Wacha Wafu Wazike wafu wao!!"
   
 12. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #12
  Apr 12, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,003
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  hiyo siri au habari? hata CHADEMA agenda yao kubwa nikuidhoofisha CCM, kwani ushawahi kusikia kweye mechi ya SIMBA na YANGA kuwa timu moja imetamka hadharani kujiandaa kufungwa na timu pinzani??? hizo siri zilikuwepo enzi za TANU, zilikuwepo kabla ya uchaguzi mkuu, na zitaendelea kuwepo, na vyama pinzani km CDM vitaendelea kukabiliana navyo.
   
 13. FDR.Jr

  FDR.Jr JF-Expert Member

  #13
  Apr 12, 2011
  Joined: Jun 17, 2008
  Messages: 1,335
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  ikiwa mkuu ameliona hili basi tuko pamoja, twende pamoja na tutashinda pamoja , inshallah
   
 14. e

  emalau JF-Expert Member

  #14
  Apr 12, 2011
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 1,179
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Kwani nyoka akijivua gamba huwa anabadilika ? sumu iko pale pale !!!
   
 15. N

  Nonda JF-Expert Member

  #15
  Apr 12, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Wakuu.

  Dont underestimate CCM. Hawa watu ni wazuri katika kupanga mbinu chafu.
  Nani alitegemea surprise ya CCM ya kutangwazwa washindi 2010?

  Historia inaonesha kuwa mipango yao ya kusambaratisha upinzani imefanikiwa mara zote miaka iliyopita.
  Sasa wakati tunasema CCM imekwisha ni vizuri tujitathmini na sisi wenyewe isiwe sisi ndio tumemalizika.!!!

  Mpaka sasa hakuna chama ch siasa chenye mbinu chafu kama CCM, lakini pia hakuna chama chenye nyenzo na mtaji kama CCM.

  Na wananchi wengi si wananchama wa vyama vya siasa.

  Sasa Ninyi wenye vyama isitokee kuwa caught off- guard na CCM!
   
 16. m

  motenya Member

  #16
  Apr 12, 2011
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Hakuna lolote hapo ccm ni ileile na wezi ni walewale kwa mwenye uwezo wa kufikiri huwezi kukubaliana na ujinga wa ccm wa kuwahaadaa watz, jamani sekretariet yote bado ni wezi wakuu wa mali za nchi hii kuweni makini na wala ushishangilie matukio tuangalie matokeo.
   
 17. M

  Mwera JF-Expert Member

  #17
  Apr 12, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  samir nasri nani alikudanganya eti mpanda nikijijini?naona hujafika kaka,mpanda nimjini kaka na ndio mji wakwanza ktk mikoa yote yanyandazajuu kuwa nambunge wa upinzani,labda huko kwengine ila mpanda nimji zamani nanimji wawajanja.ametoka wazirimkuu pale ila watu wamechagua mbunge wa upinzani mpanda waliamka zamani kaka.
   
 18. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #18
  Apr 12, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Lisemwalo lipo na kama halipo laja.
  Maeneo mengi ya vijijini Vyama vya upinzani hawavifahamu na havina mizizi. CCM ina mizizi huko waliyoitandaza tangu enzi za TANU. Vyama vya upinzania kama Chadema vinatakiwa kuelekeza nguvu kubwa mijijini sambamba na wanavyoeneza mizizi kwa wanavyuo.

  Wengi wameshaongelea hilo na kwa bahati nzuri kwa sasa hivi intelijensia siku hizi ni nzuri kwa vile tunajua vema mikakati yote inayofanywa na ccm. Wajumbe wa CCM kabla hawajatoka Dodoma tayari mambo na mikakati yao imeshaibuka, kwa hiyo kazi ni kujenga msingi vijijini kwa vile mijini kazi imekamilika.
   
 19. Lighondi

  Lighondi JF-Expert Member

  #19
  Apr 12, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 585
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Hii nayo point ya kufanyia kazi. Tusitumie hisia bali uhalisia.
   
 20. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #20
  Apr 12, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kuna mengi ambayo wadau hapa wanashauri na hivyo Chadema wafungue macho.
  - Uanzishwaji wa vyombo vya habari vinavyojitegemea kama gazeti na radio ili kujitangaza hiyo ni nyenzo muhimu
  - Kupenya vijiji ili kuoanzisha matawi ili raia wapate elimu ya uraia na hivyo kudhoofisha mizizi ya ccm
  - Kuwe na mtandao huru kama ilivyo jamii forums ili wananchi waweze kutoa michango ya mawazo yao.
  Maandamano pekee si siraha ya kutosha kwa vile wa mijini rahisi kuwashawishi kwa maanamano, wavijijini je?
   
Loading...