Siri usiyoijua kuhusu ndoto na tafsiri zake

Kwanza nianze kwa kuelezea ndoto maana yake,

Ndoto ni mkusanyiko wa matukio ambayo binadamu huyaweka kichwani kwake ambayo humjia bila zuio (involuntary) kwenye ubongo wakati akiwa amelala,matukio haya huwa hayaeleweki na saa nyingine huwa kinadharia zaidi mfano kuota unapaa wakati kiualisia haiwezejani.kiujumla sayansi imeshindwa kuja na jibu kamili kuhusu ndoto ,na matokeo yake wameishia kutoa tafsiri hiyo .

Ukija kwenye dini ndoto huwa ndio njia maalumu ambayo ulimwengu wa Roho hutumia kuwasiliana na binadamu,hapa sasa ndio nataka tuanze.

Kibibilia Mungu hutumia matukio tuliyoyaifadhi au kumbukumbu za vitu tulivyoifadhi moyoni ,ili kutengeneza codes za mawasiliano kati yake yeye na sisi .

Sasa kuna mambo kadhaa ambayo huwa ukiota lazima ujue kufungua hizo codes ,ni maarifa rahisi ila inahitaji uwe mcha Mungu na mwerevu.

Mfano
1:Ukiota unapaa angani :ndoto ya namna hii ukitaka kuifahamu lazima ujue kwa nini Mungu katumia anga,anga maana yake ni ulimwengu wa Nuru ,ardhi ni ulimwengu wa Giza ,hivyo ukiota unapaa ni taadhari kutoka kwa Mungu kwamba uache kutembea kwenye ulimwengu wa Giza ,hamia ulimwengu wa Nuru.nikuhakikishie ukifanya hivyo hutakaa uote tena kupaa sure.

2: Kuota unafanya mapenzi ;codes za ndoto hii ni mbili kulingana na mazingira yako,mfano ukiota unafanya mapenzi na ukiamka unajihisi mchovu na mara nyingine kama mwanaume unahisi umemaliza ,basis ujue kuna pepo wachafu wanakuchezea.
Ila ukiota unafanya mapenzi na ukiamka hakuna ishara yoyote nikimaanisha uchovu au uchafu basi ndoto hii huwa ni njema code ya mapenzi ni pesa maana ni kipi kinapendwa zaidi ya mapenzi kama si pesa hivyo ukiota unafanya mapenzi ni ishara ya kupata pesa,kama unayefanya naye humjui basi utapata pesa kwenye vyanzo usivyotarajia. Kama umeota unafanya mapenzi na MTU unayemjua basi ujue utapata pesa zaidi kwenye vyanzo vyako vya kiuchumi unavyovijua.

3;Kuota uko darasani ,na kufanya mitihani.Hii ndoto code yake ni hivi jiulize ni nini hukupa wasiwasi kama kama kipindi uko shule hasa wakati wa mitihani kama kukosa pesa wakati wa matatizo,hivyo ndoto hii ukiota ni onyo kutoka ulimwengu wa roho kwamba kuna matatizo makubwa yatakujia na yanahitaji pesa hivyo unahitaji kuweka akiba ya pesa ,upunguze matumizi la sivyo hilo tatizo litakuaibisha.

4;Kuota kusalitiwa kimapenzi ; code yake ni hivi ni nini huumiza moyo na kuuvunja moyo kama usaliti wa kimapenzi? jibu ni msiba.hivyo kama umeota mwenzi wako anakusaliti na kiuhalisia si kweli basi ni ujumbe wa kifo kwa huyo uliyemuota either yeye ,familia yake watakumbwa na tukio la msiba hivyo Muombee huenda bado ulimwengu wa Roho haujaidhinisha hilo janga.

Ntaendelea kesho...............pia ukumbuke somo la ndoto lilikuwapo tangu zamani Yusuph alisoma kupitia vitabu alivyoiba mama yake RHaheli wakati anatoka kwa baba yake aliyekua mganga na mtabiri alijulikana kama Laban ,
Danieli alisomea huko uajemi enzi za utumwa

Na binadamu huota zaid ya ndoto 20 kwa siku ,ndoto yenye ujumbe huwa unaikumbuka vema na huwa inaushtua moyo.nyingine huwez kuzikumbuka maana huwa kazi yake ni kuufanya ubongo ufanye kazi vizuri ,hivyo siyo ndoto zote ni ujumbe unatakiwa uwe mwerevu wa kusoma mazingira na hali yako.
Ingekua hivyo basi ingekua balaa kweli kweli
 
Mimi nimeota nipo shule na nilikuwa nataniana na wenzangu kuhusu maswali ya shairi, Mimi nikatania kuwa utakuta swali linasema mstari wa pili katika ubeti wa 50 na ngapi huko unasemaje au baada ya nukta Fulani yanafuata maneno gani? Yaani nikawa natania vitu ambavyo sidhani Kama vipo ,mwishowe nimecheka kicheko kitamu kweli na kicheko kile sijawahi kukicheka maishani mwangu hatimaye nikashituka (hii ndoto Ina maana gani boss?)
 
Niliota nimepata ajali ya gari nikatoka salama,nikaona gari inaendelea kunguruma ikiwa chini nikaenda kuizima nilipo lizima hapo hapo likawaka moto hii inamaana gani.maana kweli natumia gari kila siku.
 
Mbona umecheka ?

Nimeuliza swali la msingi sana
Na mleta mada hajanijibu...

Ni sawa na kumpa mtu chakula kitamu halafu akakuuliza umepika pikaje hiki chakula? Ili na mimi nikapike nile?

Ukikataa kumjibu kuna sababu zifuatazo

1. Kama ni chakula cha biashara basi unaogopa kutoa ujuzi ili kulinda soko lako

2. Kama ni chakula cha Nyumbani basi itakuwa ni uchoyo tu wa maarifa...
 
Nimeota tupo kwenye mashua tunavuka maji mara ghafla kukatokea dhoruba kubwa cjui ni baharn au mtoni lakn tuliweza kufanikiwa kuvuka na kifika ng'ambo salama ckumbuki kama kwenye ndoto hyo nilikuwa nahofu wakat wa dhoruba hiyo.
 
Mwaka jana kati sikumbuki ni mwezi gani ila kati ya june-august hivi. Kuna ndoto niliota aisee niliogopa kuwahadithia watu, maana kama kakichekesho wewe sasa ukutane na wazito hivyo ukae nao ah wapi sikuipa umuhimu.

NDOTO YA KWANZA

Niliota nipo sebleni mimi Hayati Magufuli (R.I.P) na Lowasa sikua muongeaji hata huko ndotoni baada ya muda Lowasa akatoka ndani nikajikuta nina kisu nikamchoma nacho Magufuli tumbuni nikakivuta kutoka upande a kwenda upande b (mf. kutoka kushoto kwenda kulia) sikuumia wala kushtuka wala kuona kuumizwa na tukio hilo huko ndotoni ndipo nikashtuka kurudi mwilini. Hii naikumbuka vyema.

Ndoto nyingine ya pili ni hii;

Usiku wa kuamkia jana.

Niliota nipo na mdada(namjua) mmoja hivi mahali kwenye watu gafla nikamshikana mkono nikaanza kumkimbia nae tunaelekea pori flani hivi ila tukafanye ngono. Tukafika huko, nikawa namchezea mwili wake ile hali ya kuiba iba sasa shughuli ikawa kufanya nae ngono anataka na mimi nataka ila hatufanikiwi kufikia lengo...
Baada ya muda kidogo nikashtuka.

Nini hasa maana ya hizi ndoto.?
 
Naota sana harusi mkuu,tena sherehe kubwa na watu wamejaa wamependeza saa zingine wameshona hadi sare ila katika ndoto zote maharusi siwaoni ila tu tunasherehekea,ndoto hii nmeota mara tatu ndani ya miezi miwili hii
 
Huwa gari kwa zamani wengi walikua wakiota farasi ila kwa nyakati hizi za maendeleo farasi amekua replaced na gari ,baiskel,pikipik,na vyombo vingine ,ukiota gari maana yake ni wakati ,hivyo ndugu yangu inaonesha uko nje ya wakati yaan kuna mambo unafanya ambayo si wakati wake ,sijajua ni mambo gani ila ulimwengu wa roho unakuasa urudi kwenye line ,gari kuingia ndani ni msisitizo mkubwa na ndio maana ukaota pia mara mbili ,embu jaribu kwenda na wakati ,uko nje ya mda either unayofanya hayaendani na umri wako ,au kipato chako,au hadhi yako ,au majukumu yako ,rudi mara moja maana kuna hatari mbele
Elimu ya kutafsili ndoto ni ngumu sana anyway mkuu jitahidi kusoma maana nimesoma unayoyaandika ni machache ambayo uko sawa acha kuwalisha wenzako matango poli
 
Toa wewe tafsiri kama unaona kaz nyepes ,binadamu siku zote hujiona wajuaji hata Mungu akishuka mtampinga tuu. To a fact zako ueleweke unasema kama wadada wa uswahilin yaan hiyo tunaita mipasho ,na mwanaume kuwa na mipasho ni dhahiri una matatizo yamekusibu si bure .Na ukitaka naweza kukujulisha nini haswa huwasumbua watu kama nyie kwenye akili zenu,hili ni somo pana sana,maana nakuona uko mtupu kabisa umeamua kujiandikia tuu,ila una tatizo kubwa sana usipoangalia litaathiri mpaka imani yako,na maono yako,Kaa na Mungu mkuu la sivyo .......
 
Kuota unapaa! Wakati huo upo angani unarushwa na wachawi, kitandani pamebaki kitu kinachofanana na wewe! Wanakuchezea na kukurudisha .
 
Pia epuka kula ukashiba sana kipindi cha usiku maana ndoto zake hazielezeki unaweza.
 
daah mkuu hii ni kweli kabisa siwezi kusema nimepata mafanikio 100% ila ukilinganisha kipindi cha miaka miwili nyuma na sasa hivi nimepiga hatua na hii ni kutokana na kazi nzuri niliyopata na cheo ambacho ninacho kwa sasa.,,nazidi kuomba Mungu nifanikiwe zaidi
Ndio umeambiwa usitusahau wenzio kwenye mafanikio yako sasa.
 
Kwanza nianze kwa kuelezea ndoto maana yake,

Ndoto ni mkusanyiko wa matukio ambayo binadamu huyaweka kichwani kwake ambayo humjia bila zuio (involuntary) kwenye ubongo wakati akiwa amelala,matukio haya huwa hayaeleweki na saa nyingine huwa kinadharia zaidi mfano kuota unapaa wakati kiualisia haiwezejani.kiujumla sayansi imeshindwa kuja na jibu kamili kuhusu ndoto ,na matokeo yake wameishia kutoa tafsiri hiyo .

Ukija kwenye dini ndoto huwa ndio njia maalumu ambayo ulimwengu wa Roho hutumia kuwasiliana na binadamu,hapa sasa ndio nataka tuanze.

Kibibilia Mungu hutumia matukio tuliyoyaifadhi au kumbukumbu za vitu tulivyoifadhi moyoni ,ili kutengeneza codes za mawasiliano kati yake yeye na sisi .

Sasa kuna mambo kadhaa ambayo huwa ukiota lazima ujue kufungua hizo codes ,ni maarifa rahisi ila inahitaji uwe mcha Mungu na mwerevu.

Mfano
1:Ukiota unapaa angani :ndoto ya namna hii ukitaka kuifahamu lazima ujue kwa nini Mungu katumia anga,anga maana yake ni ulimwengu wa Nuru ,ardhi ni ulimwengu wa Giza ,hivyo ukiota unapaa ni taadhari kutoka kwa Mungu kwamba uache kutembea kwenye ulimwengu wa Giza ,hamia ulimwengu wa Nuru.nikuhakikishie ukifanya hivyo hutakaa uote tena kupaa sure.

2: Kuota unafanya mapenzi ;codes za ndoto hii ni mbili kulingana na mazingira yako,mfano ukiota unafanya mapenzi na ukiamka unajihisi mchovu na mara nyingine kama mwanaume unahisi umemaliza ,basis ujue kuna pepo wachafu wanakuchezea.
Ila ukiota unafanya mapenzi na ukiamka hakuna ishara yoyote nikimaanisha uchovu au uchafu basi ndoto hii huwa ni njema code ya mapenzi ni pesa maana ni kipi kinapendwa zaidi ya mapenzi kama si pesa hivyo ukiota unafanya mapenzi ni ishara ya kupata pesa,kama unayefanya naye humjui basi utapata pesa kwenye vyanzo usivyotarajia. Kama umeota unafanya mapenzi na MTU unayemjua basi ujue utapata pesa zaidi kwenye vyanzo vyako vya kiuchumi unavyovijua.

3;Kuota uko darasani ,na kufanya mitihani.Hii ndoto code yake ni hivi jiulize ni nini hukupa wasiwasi kama kama kipindi uko shule hasa wakati wa mitihani kama kukosa pesa wakati wa matatizo,hivyo ndoto hii ukiota ni onyo kutoka ulimwengu wa roho kwamba kuna matatizo makubwa yatakujia na yanahitaji pesa hivyo unahitaji kuweka akiba ya pesa ,upunguze matumizi la sivyo hilo tatizo litakuaibisha.

4;Kuota kusalitiwa kimapenzi ; code yake ni hivi ni nini huumiza moyo na kuuvunja moyo kama usaliti wa kimapenzi? jibu ni msiba.hivyo kama umeota mwenzi wako anakusaliti na kiuhalisia si kweli basi ni ujumbe wa kifo kwa huyo uliyemuota either yeye ,familia yake watakumbwa na tukio la msiba hivyo Muombee huenda bado ulimwengu wa Roho haujaidhinisha hilo janga.

Ntaendelea kesho...............pia ukumbuke somo la ndoto lilikuwapo tangu zamani Yusuph alisoma kupitia vitabu alivyoiba mama yake RHaheli wakati anatoka kwa baba yake aliyekua mganga na mtabiri alijulikana kama Laban ,
Danieli alisomea huko uajemi enzi za utumwa

Na binadamu huota zaid ya ndoto 20 kwa siku ,ndoto yenye ujumbe huwa unaikumbuka vema na huwa inaushtua moyo.nyingine huwez kuzikumbuka maana huwa kazi yake ni kuufanya ubongo ufanye kazi vizuri ,hivyo siyo ndoto zote ni ujumbe unatakiwa uwe mwerevu wa kusoma mazingira na hali yako.
Niliota tunachimba Kaburi pembeni ya kaburi la Ndugu yangu, halafu nikakutana na Mifupa ya Ndugu yangu inaporomokea kwenye Kaburi tunalochimba la karibu.
Naomba tafsiri yake Mkuu!

Mpaka leo inanitesa maana ilinistua saana.
 
Elimu ya kutafsili ndoto ni ngumu sana anyway mkuu jitahidi kusoma maana nimesoma unayoyaandika ni machache ambayo uko sawa acha kuwalisha wenzako matango poli
Ni kweli kabisa hata mimi naona mengi anaenda chaka
 
Baba yangu jana aliota kuwa nimezungukwa na maaskari, na mimi nikaota nimemeza nyama iliyokuwa imekaangwa kwenye mafuta bila kuitafuna. Nikaota tena kuna sehemu nilikuwa nimekaa ghafla nikajihisi kama kuwashwa flani hivi, kuja kucheki nikaona kama kinyonga flani hivi kikiwa kimevimba hatari
 
Toa wewe tafsiri kama unaona kaz nyepes ,binadamu siku zote hujiona wajuaji hata Mungu akishuka mtampinga tuu. To a fact zako ueleweke unasema kama wadada wa uswahilin yaan hiyo tunaita mipasho ,na mwanaume kuwa na mipasho ni dhahiri una matatizo yamekusibu si bure .Na ukitaka naweza kukujulisha nini haswa huwasumbua watu kama nyie kwenye akili zenu,hili ni somo pana sana,maana nakuona uko mtupu kabisa umeamua kujiandikia tuu,ila una tatizo kubwa sana usipoangalia litaathiri mpaka imani yako,na maono yako,Kaa na Mungu mkuu la sivyo .......
Nimeota chui ama simba anataka kuni shambulia
 
Mkuu habari Mimi huwa naota nimekunja miguu napaa hewani kunakundi lawatu linanikimbiza hao watu siwa jui.huwa wananikimbiza hawanikamati Ila wao hawapai angani Mimi tuu ndo huwa napaa nikiwa nimekunja miguu.
 
Huwa gari kwa zamani wengi walikua wakiota farasi ila kwa nyakati hizi za maendeleo farasi amekua replaced na gari ,baiskel,pikipik,na vyombo vingine ,ukiota gari maana yake ni wakati ,hivyo ndugu yangu inaonesha uko nje ya wakati yaan kuna mambo unafanya ambayo si wakati wake ,sijajua ni mambo gani ila ulimwengu wa roho unakuasa urudi kwenye line ,gari kuingia ndani ni msisitizo mkubwa na ndio maana ukaota pia mara mbili ,embu jaribu kwenda na wakati ,uko nje ya mda either unayofanya hayaendani na umri wako ,au kipato chako,au hadhi yako ,au majukumu yako ,rudi mara moja maana kuna hatari mbele
Kuota uko uchi mbele za watu na unapambana kuijisitiri ila unashindwa hadi ukishtuka unaona kama nikweli. Hii imekaaje Mkuu!!?

Pia kuota kila mara uko kwenye kipindi cha mitihani na unakua hujajiandaa,unakua na hofu mpaka ukishtuka inakua kama kweli vile,nayo vipi?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom