Siri nzito yafichuka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siri nzito yafichuka

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mtoto wa Mkulima, Nov 19, 2007.

 1. Mtoto wa Mkulima

  Mtoto wa Mkulima JF-Expert Member

  #1
  Nov 19, 2007
  Joined: Apr 12, 2007
  Messages: 687
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Siri nzito yafichuka

  2007-11-19 08:23:47
  Na George Ramadhan, PST Mwanza


  Fedha nyingi za halmashauri zinazotengwa kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo, zimedaiwa zimekuwa zikitumika kuwakirimu viongozi wa serikali hasa Mawaziri wanapozitembelea halmashauri hizo.

  Kufuatia hali hiyo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Bw. Mizengo Pinda, amezipiga marufuku halmashauri zote nchini kutumia fedha za namna hiyo kuwakarimu viongozi wa serikali.

  Bw. Pinda alitoa agizo hilo lililotolewa mwishoni mwa wiki na kuwataka Wakurugenzi wa halmashauri nchini kuhakikisha kwamba fedha hizo zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa tu.

  Alikuwa akifunga mkutano wa kitaifa wa programu ya kujenga uwezo kwa wadau wa utawala bora katika serikali za mitaa.

  Alisema ni jambo la kushangaza kuona kwamba, Mkurugenzi wa Halmashauri akitumia fedha nyingi kuwakarimu viongozi wa serikali, huku watendaji wakiwa hawana mafunzo ya kutosha kutekeleza majukumu yao.

  `Kwa nini Mkurugenzi atumie Shilingi milioni tatu kuhakikisha waziri au kiongozi mwingine wa serikali anakula na kulala vizuri badala ya fedha hizo kutumika kugharimia mafunzo ya wataalam wake,` alihoji Waziri Pinda.

  Aliongeza kuwa, Wakurugenzi wanapaswa kuwekeza kwa wataalam wao kwa kuwagharimia mafunzo yote muhimu ili waweze kuleta ufanisi katika halmashauri na hivyo kuongeza tija.

  Aidha, alisema ni muhimu kwa Wakurugenzi kuwanunulia watendaji wao vitendea kazi, hususani watendaji wa vijiji na kata ili waweze kutekeleza shughuli za maendeleo kwa urahisi zaidi.

  `Mkurugenzi hawezi kunishawishi kuwa eti hana uwezo wa kumnunulia mtendaji wa kijiji baiskeli, hawa ndio wahamasishaji wa maendeleo lazima muwawezeshe,` alisema.

  Aliongeza kuwa, kwa kuwanunulia vitendea kazi, watendaji hao watafurahi kwa kutambua kwamba mabosi wao wanawajali, lakini pia watazalisha zaidi.

  SOURCE: Nipashe
   
 2. Sura-ya-Kwanza

  Sura-ya-Kwanza JF-Expert Member

  #2
  Nov 19, 2007
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 561
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  kabla hujakula ngege unakula ndagaa!
   
 3. Sura-ya-Kwanza

  Sura-ya-Kwanza JF-Expert Member

  #3
  Dec 29, 2007
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 561
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Sijui hii imefikia wapi?
   
 4. Kana-Ka-Nsungu

  Kana-Ka-Nsungu JF-Expert Member

  #4
  Dec 30, 2007
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,260
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 135
  Hii nayo ni rushwa,gharama za chakula na malazi za hao viongozi ziko included kwenye posho zao za safari lakini kwa kuwa Wakurugenzi wengi ni wabovu wanaona njia pekee ya kuwafunga midomo wakubwa ni 'kuwanunulia bia na kuwachomea mbuzi' and believe me it works.
   
Loading...