singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
kama Mbowe, Mnyika, Lema,Msingwa na Lissu wanalivyompamba lowassa na kusafisha kwa dodoki kwa ufisadi wakeWaambie wamiliki wa kipeperushi hiki kiitwacho"RAIA Tanzania"wamechelewa,kama walitaka Magufuli autambue uwepo wao walipaswa wafuate nyenendo za Jamhuri,lakini uandishi huu wa staili ya Uhuru,Mzalendo,JamboLeo na HabariLeo,hawana jipya zaidi ya uchumia tumbo unaotokana na kunyimwa fursa za kupiga hela pale Lumumba.
Waandishi wa habari wa magazeti jamii ya Raia Tanzania ni janga kwa Taifa.Hatuwezi kuendelea kama Taifa kwa kuwa na waandishi wa aina hii wanaoishia kujibanza Mwenye"kwapa za mabwana zao waliowatuma"ili waambulie 'harufu ya uturi' kutoka kwao.
Badala ya kuwa wakweli kwa Taifa lao,wameamua kuwa wanafiki kwa kutumia kalamu zao kuwapamba waharifu wa kidemokrasia.Wameamua kuimba nyimbo zinazowapendeza watawala badala ya kuusema Ukweli ambao ndiyo ungekijenga kipeperushi chao katika jamii ya wapendahaki.Wasishangae kukuta kijarida chao kinaishia kusomwa kwenye ofisi za viwavijeshi tu tena kwa kupokezana kijarida kimoja,maana wanaoshinda kwenye majengo hayo sikuhizi wamepigika vibaya kiasi cha kukosa hata hela ya kununulia kikombe cha Kahawa.
kama Mbowe, Mnyika, Lema,Msingwa na Lissu wanalivyompamba lowassa na kusafisha kwa dodoki kwa ufisadi wake