Siri nzito iliyofichika kwa Prof. Assad (CAG aliyepita)

Papaa Muu

JF-Expert Member
Nov 6, 2018
243
292
1572931972006.png

Prof Assad alitumika kimkakati kuidhoofisha serikali ya Rais Magufuli hakuwa mzalendo kama ambavyo wengi waliaminishwa. Juma Assad (Personal) aliamua kukitumia kitu chake cha kuwa CAG Katika kutekeleza mipango mikakati ya wanasiasa na ndiye mtu pekee aliyebakia kama target muhimu ya kuibua mijadala iliyobeba chini, unafiki na uzandiki dhidi ya Rais Magufuli, nyuma yake watendaji wote waliokuwa Katika Ofisi ya CAG hawamuungi mkono na 90% ya wafanyakazi Katika Ofisi ya CAG walisusia pia kumpa ushirikiano wa kiutendaji kwa sababu alikuwa habebi maazimio ya Ofisi ya CAG bali alikuwa anabena maazimio ya Prof Juma Assad na genge la boss wake aliyemteua.

Nani asiyefaham kuwa Zitto Kabwe ndie aliyempelekea ile hoja (ya kipumbavu) juu ya 1.5T? Nani asiye fahamu kuwa wakati Bunge wameingia kwenye mgogoro na Prof Assad yeye pia alikuwa na genge lake likiingozwa na Maalim Seif, Zitto Kabwe, Jusa wakitaka kuwaaminisha watanzania kuwa kuna pesa zimeibiwa? Nani asiyefahamu kuwa wakati wa mgogoro ule ambao spika Ndugai alisema wazi hatoshirikiana na Prof Assad ila atashirikiana na Ofisi ya CAG, Ofisi ya CAG nilitoa ushirikiano 100% kwa bunge hadi kupelekea Prof Assad kuitisha kikao cha siri akoshusha shutuma dhidi ya watendaji walioko chini yake Katika Ofisi ya CAG??

Anasema yupo nje kikazi? Hayupo nje kikazi baada ya hii taarifa ya Leo ambayo #Kigogo hakuipata imepelekea kutoka tension na wapo Katika kikao Kizito hapa hapa Dar es salaam Kabla ya kuelekea Pemba/Mombasa ambapo huko Zitto Kabwe, Fatuma Karume, Jusa na magenge yao wanamuandalia hoja za kisiasa kuja kijitetea Katika hili tunamngoja aje hamtoamini atailaani siku aliyozaliwa na mwanamke its matter of time!
 
Umeandika upuuzi,CAG ndiye aliyeonesha kuwa 1.5 T zilitumika kinyume na bajeti iliyopangwa na bunge!Ikumbukwe CAG hukagua matumizi ya fedha yaliyoidhinishwa na bunge!
Sasa unaposema Zitto ndiye aliyemwambia CAG juu ya 1.5T,unakuwa na maana gani kama sio uzuzu?Kwani Mkaguzi ni Zitto au CAG!
 
Ugonjwa wa uwendawazimi humfanya mtu aamini ana uelewa kuliko walio wazima. Waulize ndugu na marafiki zako wanakuonaje.

Maelezo mengi but no content. Porojo tupu.

Kama huna uwezo wa kujenga, soma za wenzako, angalao utaelimika.

Hivi unadhani kuna mwenye akili atakayezingatia hizi hadithi za kufikirika?

Heshima, weledi, ujasiri na uadilifu wa Prof. Assad haulinganishwi na hawa wazalendo wa kinadharia. Prof. Assad ni kipimo kizuri cha uzalendo wa kweli.
 
CCM mmeshavuliwa nguo mchuchumae tu hivi mmetuonaje watanzania mtu aliyeshindwa kazi mnamuweka tena awe CAG kivuli tena rais alishasema mtu aliyeshindwa kazi hawezi kumpangia kazi nyingine leo tena yamekuwa haya
Ccm ata mje na hoja gani sasa watanzania hawamwamin tena rais kwa ufisadi anaouficha
 
Mbona Prof Assad hayajui hayo hebu tumia hekima na maarifa kusikiliza majibu ya Professer. Nanukuu

"Sfahamu na sinawahi kufikiri kama ningeweza kutengeneza adui wakati wa utekelezaji wa majukumu yangu nikiwa katika ofisi hii.

Huenda waliotengeneza uadui kwangu ni wale waliokuwa wanakwenda kinyume na misingi yake ya kazi.

“I have never intentionally made an enemy, Sijawahi hata siku moja kufikiria ninatengeza uadui, inawezekana kuna watu niliwakwaza lakini ni kwa sababu ya kutosimamia misingi ya kazi,”

Hata hivyo nafikiri kusameheana ni muhimu sana kwa watu wote,”
 
Kwa hiyo unamaanisha hakuna Tr 1.5 ambayo matumizi yake hayajajulikana mpaka leo?Mkuu usitake watu wakuporomoshee matusi asubuh asubuh maana watu wanaugulia moyoni.
Izo 1.5 T zimebaki propaganda mitandaoni lakini pale Bungeni walishindwa kuthibitisha, Zitto alitaka kujaribu kutumia ripoti ya CAG kumchafua JPM lakini alishindwa vibaya pale Bungeni. JPM yuko vizuri na mzarendo Halisi kutokea katika familia za kawaida kabisa.
 
Nimemfurahia sana huyu Auditor sijui ni kada wa chama gani maana anayemfanyia kazi za auditing ni Zito Kabwe ambaye ni mchumi na mwanasiasa lakini Auditor huyu anatwambia taarifa zake zianaminika zaidi kuliko za CAG!!!!!!!!!!!!!!!!!
I LOVE MY TZ and my Lovely political PARTY
 
Papaa Muu

Takataká tupu. Mkifanya maovu mnatafuta upuzi wa kujihalalishia
Kwako ni takataka lakini kwa waelewa kama sisi tumejua undani wa Prof. na siri iliyojificha kwake na ndio maana wasaka tonge kina Zitto Kabwe wanapiga kelele sana kwa CAG mpya yote ni kutofurahishwa na uteuzi wa Kichere
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom