Nyambala
JF-Expert Member
- Oct 10, 2007
- 4,465
- 1,170
Nyambala tutakuwaje serious wakati wewe unaonyesha udhaifu mkubwa kwa kubeza uranium, dhahabu nk eti coal na iron ore ndio itatutoa, kama tumeshindwa dhahabu ambayo ingetutoa kama tungeisimamia vizuri tutawezaje coal na iron ore. Kwataarifa tu ni kwamba huko serikalini wengi kama sio wote wana mawazo ya kijinga kama yako na ndio maana rasilimali zetu hazitunufaishi kitu ila zinamnufaisha mwekezaji, huo ni 'ukilaza' ndugu yangu
Mkuu sielewi huo unaouita udhaifu na nilichokizungumza si kubeza bali kuweka wazi facts ila kwa sababu stori kuhusu uranium, mabomu, marekani zinasensitize na kuburudisha hadhira basi watu hawataki hata kufikiri japo hata kupay attention kwa wanaofahamu hayo mambo.
Nachokizungumza unatakiwa ukielewe dhahabu au uranium processing yake ni complicated na expensive. Mfano average ya dhahabu inyopatikana hapo Tanzania ni gramme kama 3.8 per tonne, sasa kuitoa hiyo tani km20, kuiprocess mpaka upate gold unaweza kukuta kwa bei ya sasa ya 1oz = $1600, zaidi ya nusu inaishia kwenye gharama za uzalishaji. Halafu sasa siyo kwamba kila udongo around the mine utakuwa na hiyo dhahabu ndiyo maana kuna undergrounds. Ukija kwenye Coal, say Cocking coal gharama ya uzalishaji ni around $35 - $74, kwa huko Afrtica inaweza hata kuwa nusu ya hizo estimate bei yake ni $238 per ton. Na coal ukishapata ile seam unazoa tu mitani kwa mitanni. Process ya coal sana sana ni kuisafisha, chemical inayotumika ni moja tu na wala sio gharama.
Anyways on top of that kwa sababu coal na iron ore ni bulk handing yake inahitaji alot of infrastucture, hivyo kuzalisha ajira kibao, reli kama hiyo Tazara inaweza kuwa operational kwa faida for the coming 100 years. Bandari ya kuhandle coal kama ya Mchuchuma kwa makadirio inaweza kuwa mara tano ya hiyo ya Dar es salaam. U can imagine ni watanzania wangapi wataajiriwa hapo, well maintained roads, railways bado kuna suporting contractors etc.
Mkuu angalia nchi zote zilizoendelea, Germany, USA, Japan, Australia na sasa China none has done it without coal and iron ore. That is a fact ila u can choose to remain defiant.