Siri nyingine ya Ngeleja: Wamarekani tayari wanachimba Uranium Tunduru kisiri siri? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siri nyingine ya Ngeleja: Wamarekani tayari wanachimba Uranium Tunduru kisiri siri?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Game Theory, Jul 19, 2011.

 1. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #1
  Jul 19, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Jana mbunge wa viti maalim (CHADEMA) Naomi Amy Kaihula kasema kuwa kuna kampuni ya Kimarekani inachomba Uranium kisirisiri (clandestinely) katika wilaya ya Tunduru .

  Alisema kaona kwa macho yake uchimbaji ukiwa unaendelea. Sasa cha kujiuliza mbona hili hatuna habari nalo? Mkataba wake ulisainiwa lini? environmental impact assessment ilifanywa na nani? Mkataba una worth how much? serikali inapata kiasi gani?

  Lakini sitoshangaa kusikia kama huu ulikuwa ni mchongo wa BILIONEA Jairo na dumber mwenzie Ngeleja.

  Why keep it secret? kwa nini wananchi hawajulishwi kinachoeendelea ndani ya maeneo yao? Hivi law & order iki break katika mazingira haya serikali itajibu nini?

  Habari ndio hiyo
   
 2. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #2
  Jul 19, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  Nchi ya kitu kidogooo......
   
 3. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #3
  Jul 19, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Hivi tuna SERIKALI?SERA KALI?SURA KALI?ama SIRI KALI?
   
 4. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #4
  Jul 19, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu hiyo uranium haina thamani kiasi hicho mpaka kampuni ya nje ya nchi irisk kuja kuchimba kisirisiri na after all lazima uelewe kuna masuala ya grade per ton. Jmani watanzania tunahitaji tuelimike kuhusu haya mambo sasa kama hata mbunge anaweza kuongea hii (kama ni kweli) basi tuna tatizo kubwa!!!!!! Uchimbaji industrialized si sawa na "uchoji" (uchimbaji wa sululu).

  Uranuim yenye thamani kubwa ni ile enriched ambayo hata kuna baadhi ya nchi zilizoendelea kama Australia, Canada still wanauza raw (not enriched). Sasa mtu eti kwenda Tunduru ambako hata umeme hakuna, barabara ya lami hakuna, maji hakuna, reli hakuna halafu ikafanyika hiyo mining ya uranium is just a HOAX.
   
 5. a

  arigold JF-Expert Member

  #5
  Jul 19, 2011
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 594
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 60
  [​IMG]
   
 6. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #6
  Jul 19, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Upo serious na kitu ulichoandika?
  usijaribu kuonyesha utaalamu kwa kejeli.
  Nani kakwambia Uranium inachimbwa kwa sururu Tunduru?
  Unafahamu ni makampuni mangapi yanafanya exploration ya Uranium Maeneo ya Ruvuma,....Tunduru na Namtumbo?
  Unajua yameanza lini? yameshapata lease ya ardhi ya ukubwa gani na yapo stage gani ya uchimbaji na utayarishaji wa massive extraction???
   
 7. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #7
  Jul 19, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Sasa toka lini exploration ikawa ni uchimbaji?????
   
 8. Kisoda2

  Kisoda2 JF-Expert Member

  #8
  Jul 19, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 1,240
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Duuuh!
   
 9. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #9
  Jul 19, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Tatizo naloliona kwa watanzania walio wengi ni kwamba wako obsessed mno na hiyo uranium but for a fact liganga, mchuchuma ndiyo haswaa kunaweza kufanyika serious mining ya kututoa watanzania. Coal na iron ore deposit ya pale ina thamani kuliko proven reserves zote za gold Tanzania ukichanganya na ile iliyochimbwa na kuuzwa pia.

  Wakuu Niger kuna uranium ya kufa mtu na imeanza kuchimbwa miaka kibao, vipi wamefaidika nini ulifanya comparison say hata na Equatorial Guinea au Angola. Kuna uranium kibao Namibiana imeanza kuchimbwa siku nyiingi. Ukija South Africa ya kumwaga, lakini hata siku moja SA wakiwa wanazungumzia mining industry hawaifikirii hata kuifikiria. There's huge deposits of uranium in Australia na inachimbwa miaka kibao. LAKINI "THE MOTHER OF ALL MINING INDUSTRY NI COAL NA IRON ORE".

  Wawekezaji wa coal wameliona hilo na wanajua watanzania tunapuuzia na hatujui kitu kuhusu coal, si inaitwa mkaa, hivyo hapa tutapigwa bao balaaaa!!!! Lakini kama tungekuwa taifa serious coal mining ndiyo tungeikazania kwa sasa.
   
 10. chipanga

  chipanga JF-Expert Member

  #10
  Jul 19, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 661
  Likes Received: 141
  Trophy Points: 60
  Napita tu, naenda kwenye supu hapo jirani, ntarudi.
   
 11. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #11
  Jul 19, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Wote wapigwe chini Waziri, Naoibu na Katibu lao 1.
   
 12. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #12
  Jul 19, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Mkuu Nyambala nashindwa kukuelewa unamanisha nini.
  Kwamba ni sahihi wageni kuja na kuchimba bila utaratibu?
  Kwamba kwa vile enriched uranium ndio yenye thamani kwa hiyo tuwaache wachime ili wakaenrich wao kwa vile hata Australia inafanya hivyo??
  Kama hakuna barabara maana yake hakuna uchimbaji???? Kakola, Buhemba na Nyamongo kuna barabara za juu???

  Ukituliza akili utaelewa context ya mtoa mada.
  FYI, jana mbunge wa Bahi-Dodoma kalalamika the same thing. wananchi wameporwa ardhi kisa madini ya uranium.
  Kwa upande mwingine mama Kaihula ni moja ya wamama wasomi sidhani kama amekurupuka
   
 13. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #13
  Jul 19, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu you got me wrong, nachomaanisha hiyo habari ni ya uongo period.
   
 14. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #14
  Jul 19, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu ndiyo maana nimeanza kwa kusema uranium haina bei kiasi hicho, in short kwa mazingira yale huwezi ku-make profit. Kakola, buhemba na Nyamongo zote ziko less than 100km kutoka barabara ya lami au reli. Na pia the finished product (Gold) inasafirishwa kwa ndege.

  Sababu nilizotaja ndiyo haswaa zimefanya kabanga nickel isianzishwe mpaka leo!!!!
   
 15. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #15
  Jul 19, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Mkuu kama tatizo ni authenticity ya hoja hilo ni jambo jingine ila tumeshang'atwa na nyoka don't rule it out viongozi wetu mapepe.
  Kama katibu mkuu anasanya (kama kwenye daladala) 50m kila idara unategemea jema kutoka kwake??
  Tuna mikataba na makampuni ya madini ambapo hata ukibadili sheria zako leo wao haiwagusi kama sio kulaaniwa ni nini??

  Huko Bukombe/kahama kuna kampuni inafanya exploration lakini taarifa zilifichuliwa na Raia Mwema kwamba jamaa wanajisevia utadhani nchi haina mwenyewe.

  Ila as I said: Naomi Kaihula ni mtu wa Mbeya na kaelimika sidhani kama amekurupuka
   
 16. S

  SEAL Team 6 JF-Expert Member

  #16
  Jul 19, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nguvu ya umma itumike kumwajibisha ngereja, this man should step down. Madini yanaibiwa, hakuna umeme nchini, anatumia mbinuchafu ya kuhonga viongozi wa serikali kulinda masilahi ya Mafisadi. Barua ya jana iliyosomwa Bungeni ni uthibitisho tosha kabisa kumfukuza kazi Ngereja kwa sababu alikuwa anajua deal lote.
   
 17. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #17
  Jul 19, 2011
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,053
  Likes Received: 3,977
  Trophy Points: 280
  Unapoongelea thamani ya uranium unapaswa uwe na credible sources! mwaka jana uranium (yellow cakes) price iligonga $140 per pound! Japokuwa thamani yake huwa inapanda na kushuka yaani si stable speculation zinadai bei ya uranium itaendelea kupaa kutokana na mahitaji ya Uchina! Na ndio maana makampuni mengi yanakuja kufanya exploration! Kwa sasa 1 pound ni $ 53 Market price!
   
 18. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #18
  Jul 19, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu mimi naizungumzia hii from experience, at least I make a living from that industry. And where I am now ndiyo kwa baba na mama wa hii industry. Sasa huwa inanishangaza pale ambapo kuna baadhi ya issues kuhusu mining zinavyokuwa adressed tena sometimes hata na mawaziri. Kama ile eti ndege zinatua migodini na kubeba dhahabu na kuondoka juu kwa juu.
   
 19. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #19
  Jul 19, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu hivi unafikiri kwa a medium sized uranium mining wanazalisha hizo pounds ngapi kwa siku?

  Hebu niambie hapo bongo, Niger, na wengineo mnabakiwa na kiasi gani cha kutufanya tuwe obsessed kiasi hiki???????
   
 20. TinyMonster

  TinyMonster JF-Expert Member

  #20
  Jul 19, 2011
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 235
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Ofcourse acha wachimbe.. na hakuna haja ya kumlaumu Ngeleja na wizara yake.

  Laumu majuha zaidi ya milioni nne walioirudisha CCM madarakani kwenye uchaguzi wa mwaka jana. Biblia inasema utavuna ulichopanda, na ndo kinachotokea sasa hivi.
   
Loading...