Siri na michezo michafu ndani ya ICT

Kilongwe

JF-Expert Member
Feb 7, 2008
423
115

Kwa original Post: AfroIT.com

Je upo kwenye maandalizi ya kujikita kwenye huu ulimwengu wa ICT? ICT kama fani nyingine inahitaji maandalizi na uchunguzi wa kina kabla ya kujikita kwani bila kufanya hivyo unaweza kujikuta umedumbukia mahali pasipokufaa au umeingia bila maandalizi.Kila fani ina siri zake ambazo zitakuwezesha kukabiliana nayo na hatimaye kupata mafanikio,hivyo leo nitakupa baadhi ya siri ambazo wewe kama mwana ICT au kama unajiandaa kuingia kwenye fani ya ICT zinaweza kuwa na msaada wa kutosha.​

Kwa wale ambao wapo kwenye huu ulimwengu wa ICT basi watakuwa na mengi ya kuongezea,hivyo basi AfroIT inakukaribisha kuongezea siri za mafanikio ndani ya ulimwengu wa ICT,ingawa kuna baadhi zinaweza kuwa na matumizi kwako binafsi,ila kuna baadhi kati yaozitakuwa na msaaada kwa jamii nzima ya Kitanzania.​

1.Mshahara ni mkubwa kulinganisha na fani nyingine,ila waajiri huwatumia wana ICT kikamilifu.
images(2).jpg

Ukweli usiopingika ni kuwa,makampuni mengi huwalipa wana ICT kiwango kikubwa cha mshahara kulinganisha na waajiriwa wengine,hii inaweza kuwa ni ulimbo ambao utawavutia wengi kunasa kwenye
hii fani,ila machungu yanakuja pale unapopokea simu saa kumi na mbili asubuhi ndani ya wikiendi ukitakiwa kwenda kazini kurekebisha mambo.Ukimuuliza muajiri,yeye husema sasa unategemea
tusubiri hadi jumatatu? je mshahara mkubwa tunaokulipa hujui unatokana na mambo kama haya? Hivyo ukweli unabakia kuwa lipa mshahara mkubwa na mtumie ipasavyo.​

2.Lawama zisizokuhusu.

Ukiwa ndani ya ICT lawama zisizokuhusu ni kitu cha kawaida,unakuta bosi anaanza kulalama kuwa umefanya nini kwenye kompyuta yake kwani hawezi kutumia internet,kumbe tatizo ni yeye mwenyewe kafuta programu au kiunganishi cha internet,mambo yanakuwa magumu zaidi pale sheria za kampuni zinapowabana wafanyakazi na wewe kama mwana IT unatakiwa kuhakikisha sheria zinafuatwa,hapo utapokea lawama na hata matusi(jamaa ni mnoko utafikiri kampuni ni ya baba yake),lawama kibao kumbe wewe unafuata sheria na kanuni za kampuni.​

3.utapata misifa na kupondwa kwa sekunde.

Si unakumbuka jinsi jamaa walivyokuona wewe ni balaa baada ya kuwatatulia wafanyakazi tatizo doogo la kupiga picha kioo cha kompyuta9screen) ambapo hapo zamani walikuwa wanatumia kamera kupiga picha screen halafu kuweka picha kwenye kompyuta,ila leo ukawaonesha jinsi ya kufanya kwa kutumia komandi moja tu?​

Utasikia misifa kibao dah,jamaa ni noma,kumbe ni kitu kidogo mno.Ila baada ya sekunde jamaa kashindwa kuprint barua yake kwakuwa network imeleta matatizo na baada ya kukuita umehangaika bila ufumbuzi,utasikia,jamaa ni kilaza,hakuna kitu pale kwani kampuni inapoteza pesa tu.Ila baada ya sekund tena ukamuonesha ni jinsi gani anaweza kufuta kumbukumbu kwenye kompyuta yake na bosi asiweze jua alitembelea tovuti gani,misifa itaruudi tena.dah jamaa ni noma.Hivyo ndani ya ICT ni mwendo wa misifa na mipondo kwa kwenda mbele.​

4.Vyeti vya IT vitakusaidia pindi unapotafuta kazi.

Tuliwahi kuzungumzia juu ya nini bora,cheti au ujuzi? Ukweli usiofichika ni kuwa jamaa wa HR wengi huzimia watu wenye vyeti,kwani wenyewe husema mtu mwenye cheti inaonesha jamaa yupo makini na mambo yake pia ana moyo wa kujiendeleza hivyo kama atakuja kwenye kampuni yetu basi atakuwa na mchango mkubwa.Hivyo basi kuwa na cheti kutakusaidia katika kupata kazi lazima sio lazima kukusaidia katika kujiendeleza kifani kwani kuuna baadhi ya vyeti ni mwendo wa kubeba kwa kwenda mbele.
5.Watu watakugeuza kuwa kituo cha msaaada.

Kama wewe ni mwana IT angalau hata kwa miezi kadhaa,utakuwa ni shuhuda wa kutosha ni jinsi gani rafiki na hata majirani walivyokugeuza kituo cha msaada wa vifaa vyao.Ukiwa kwenye huu ulimwengu basi simu hazitaisha,leo utasikia kompyuta yangu imevamiwa na virusi kesho huyu atakupigia simu usiku mnene eti anataka kuongea na kaka yake aliye nje ya nchi ila internet inamletea matatizo.Kuna baadhi yao ambao wanafahamu na kujali msaaada wako wanaweza kukulipa kwa kazi yako ila wengi kati yao wataleta urafiki na kujuana.​

6.Kusukumiziana mizigo.

sio-mim.jpg
kweli usiofichika ni kuwa hakuna mtu anayejua kila kitu au asiyefanya makosa,wengi wa wataalamu wa ICT hupenda kusukumizia lawama kwa wengine pindi mambo yanapoenda mlama,hii inawasaidia wao kujiweka kwenye mazingira mazuri.Nakumbuka kuna siku nilitakiwa kuunganisha application moja na oracle,ila binafsi sikuwa na utaalam mzuri wa oracle,basi nilichokifanya ni kuanza kusema,Ah,hawa jamaa ni ovyo sana ,inakuwaje wanatengeneza programu ambayo haiwezi kutumia database ya oracle,basi nikamuambia manager tutumia MS SQL.Akanielewa na baada ya hapo ikabidi niende kuisoma oracle kwa undani kwani moyoni niliumia kwakuwa nilikuwa najua kuwa tatizo halikuwa kwa programu bali ni mimi binafsi oracle kwangu ni kimeo.
7.Wateja wengi hupenda kuongopewa.

Wana IT wengi ni kama madaktari,inakuwaje mgonjwa anakuja hospitali anasema anasikia kizunguzungu,ila ulipomfanyia uchunguzi wa juujuu ukagundua ni mambo ya uchovu tu,mgonjwa hawezi kukuelewa kama utamuambia nenda kapumzike bila dawa yoyote,inabidi umpe aspirini na kumuambia aende kupumzika.Hii ni sawa na sisi wana ICT.
Kuna siku jamaa walinipigia simu usiku wa manane akilalamika kuwa ni siku yapili wateja wake router yao haifanyi kazi na yeye hajui la kufanya,nikamuuliza maswali kadhaa na kukundua ilikuwa ni kuzidiwa(full buffer memory),nimakwambia aizimwe na kuiwasha upya,baada ya hapo mambo yakawa mwake,sasa chukulia tatizo dogo kama hili endapo walimuita expert kuja kufanya kazi,je mteja atakuelewa kama umetatua tatizo harakaharakakama hivyo? Hapo unatakiwa kuanzisha debug na minamba namba kibao kutokea,unaiacha kwa muda kama nusu saa huku ukimuambia mteja asikuge kitu kwani sasa unaweka mambo sawa,hii inamfanya mteja kuona kweli umefanya​

8.Elimu na Utaalam

imagesCAPOK28H.jpg
Je haujawahi kusikia watu wakibishana juu ya ni nani mtaalamu kuliko mwingine,kuna wakati unaweza kukuta mwana ICT mwenzako akikuponda ili kujijengenea heshima,hii inatokea sana makazini pindi anapoona unakubalika au kufanya mambo mazuri.Kwani wengi wetu tumekuwa na imani potofu kuwa kama mtu ana degree nyingi basi atakuwa anajua zaidi ya yule mwenye degree chache,kitu ambacho sio lazima kiwe na ukweli haswaa kwenye haya mambo ya ufundi.
Labda nikupe mfano ambao umewahi kunitokea mimi binafsi,kuna rafiki yangu mmoja niliwahi kumsaidia kutatua tatizo la kompyuta yake,baada ya muda jamaa akawa hawezi kwenda online,akamuita jamaa mmoja toka Kenya ambaye alikuwa nachukua degree ya pili aje kumsaidia,jamaa alivyofika na kuhangaika kwa masaa kadhaa,bila utatuzi(inaonesha alikuwa anaoteaotea)akasema unajua nini,huyu jamaa aliyekutengenezea kompyuta yako alikuwa hajui anachokifanya,baada ya rafiki yangu kumuambia huyu jamaa aliyenisaidia naye sio mbaya jamaa akaanza kujibebea mno akisema mimi nimefanya kazi miaka mitatu tena sasa nachukua degree yangu ya pili na mengine meeengi, mwisho wa siku akasema nitarudi kwani hii kazi inahitaji kama masaa matano.Nitakuja jumamosi na kulitatua huku akimwaga madongo kibao.
Kwakuwa jamaa alikuwa ananiamini alinipigia simu tena,nilipoenda nilitumia komandi moja tu "ipconfig" na kugundua kuwa jamaa DHCP server yake ina matatizo kwani anapewa default gateway siyo.Nikatatua na jamaa kufurahi na kurudisha imani kwangu huku nikamuonesha jamaa kuwa elimu na ujuzi ni vitu tofauti ingawa vina uhusiano.​

Je una siri gani au jambo gani ambalo limewahi kukutatiza ndani ya ICT? Ulipambana nalo vipi? Ungana na wana AfroIT kwa kutoa maoni yako hata kwa uchache wake.
 
Ukweli usiopingika ni kuwa,makampuni mengi huwalipa wana ICT kiwango kikubwa cha mshahara kulinganisha na waajiriwa wengine,hii inaweza kuwa ni ulimbo ambao utawavutia wengi kunasa kwenye
hii fani,ila machungu yanakuja pale unapopokea simu saa kumi na mbili asubuhi ndani ya wikiendi ukitakiwa kwenda kazini kurekebisha mambo.

Hii sehemu ambayo mtu huyu wa ICT mpaka leo hajaleta remote access naona kosa litakuwa lake mwenyewe huyu fundi wa ICT.

Siku hizi ambazo watu wanaongelea kufanya kazi kutoka nyumbani ukiwa huna system ya remote login nitakushangaa.

Of course hata kama una remote login kuamshwa ungodly hours bado ni karaha tu, lakini at least huhitaji ku commute.
 
Sehemu ya 2 na ya 5 ni vichekesho vitupu, kama huna moyo wa uvumilifu unaweza kujikuta unakorofishana na baadhi ya watu... Ukweli ni kwamba hii taaluma ni ngumu sana tofauti na baadhi ya watu wanavyoichukulia kuwa ni kazi rahisi...
 
9. WANA ICT WAKIGONGANA NA TATIZO HALIJAJULIKANA
Kampuni mbili zina share resources na kila kampuni ina ICT personnel wake. Mambo yanakuwa mambo pale ambapo wote wawili hawajui chanzo cha tatizo na pressure kutoka kwa mabosi inaongezeka. Kila mmoja atajaribu kuonesha system zake ziko safi na kuwa kuna uwezekano mkubwa tatizo liko upande mwingine

Wakati huohuo moyoni anaomba isitokee tatizo likawa upande wake. Mara nyingi unakuta each side inakuwa defensive na data zingine wanakuwa wanafichiana, ilimradi tu kukwepesha tatizo. Hii hupunguza ufanisi katika ku resolve tatizo na kuongeza down time. Kikubwa ni kuwa mwisho wa siku resolution inayotolewa ktk report inakuwa too vague kumshika mtu yeyote responsible...Mambo ya ICT haya!
 
2.Lawama zisizokuhusu.

Ukiwa ndani ya ICT lawama zisizokuhusu ni kitu cha kawaida,unakuta bosi anaanza kulalama kuwa umefanya nini kwenye kompyuta yake kwani hawezi kutumia internet,kumbe tatizo ni yeye mwenyewe kafuta programu au kiunganishi cha internet,mambo yanakuwa magumu zaidi pale sheria za kampuni zinapowabana wafanyakazi na wewe kama mwana IT unatakiwa kuhakikisha sheria zinafuatwa,hapo utapokea lawama na hata matusi(jamaa ni mnoko utafikiri kampuni ni ya baba yake),lawama kibao kumbe wewe unafuata sheria na kanuni za kampuni.

Jamaa mmoja alikuja na laptop yake nimrekebishie kwani ilikuwa sloo. Nikamwambia laptop yako ni ya zamani sana, memory spid, ram na hd ni ndogo. Ni bora akanunua nyingine sababu yee anataka kuweka program nyingi za kisasa lakini hakunielewa. Nikamwekea win xp sp3, matokeo yake mashine ikawa sloo zaidi, akaanza kunilaumu.
 
Ungemwekea 98 au 95 kabisa ingekuwa fasta tu! Angelalama ungemwambia kwa specs zako hapo ndo kwenyewe :lol:

Mkuu hapa umenifurahisha,hapo napo lawama zingeanza kwani angesema angalia kaniwekea hii kitu haina muonekano mzuri tena ni ya zamani mno.Angalia rafiki yangu anatumia W7.Huyu IT aliyeniwekea aendi na wakati.Na mengine kibaaaaao.
 
Mkuu hapa umenifurahisha,hapo napo lawama zingeanza kwani angesema angalia kaniwekea hii kitu haina muonekano mzuri tena ni ya zamani mno.Angalia rafiki yangu anatumia W7.Huyu IT aliyeniwekea aendi na wakati.Na mengine kibaaaaao.
Dawa ya wabishi wasio na shukrani ni kuwapa mambo sahihi kama hayo. Technically correct badala ya polically correct
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom