Ukijua siri zao utajua kama maoni unayotoa yatazingatiwa au yataachwa kwa maagizo ya serikali. Kwa mfano kuna huyu Humphrey Polepole ambaye ameingia kama mwakilishi wa asasi za kiraia. Huyu mkutano wa kupendekeza jina lake kule Dodoma ulivurugika, pamoja kusaidiwa na Ikulu baada ya ya mkutano wake na Kikwete bado alishika nafasi ya tatu. Mapendekezo ya asasi za kiraia wa kwanza alikuwa John Ulanga, wa pili Profesa Ruth Meena wa TGNP lakini Kikwete amewaacha wote akamchukua huyu.
Msimamo wake unajulikana kabla kwa kuwa mara zote alivyozungumza na vyombo vya habari kuhusu muswada mbovu wa sheria ya katiba uliokataliwa na asasi za kiraia yeye alitofautiana na wenzake na kuunga mkono. Uchaguzi ule wa Dodoma tulishuhudia NGO zenye utii kwa serikali zikieleza kuwa haziwataki wanasheria kama Wakili Harold Sungusia wa LHRC kwenye tume ya katiba kwa kuwa atakwenda kupingana na serikali. Hivyo wakataka Kikwete amchague Polepole kutoka TYC ili NGO ambazo zimekuwa zikichochea wananchi nchini kuhusu katiba zisipate uwakilishi wenye nguvu ndani ya tume.
PM
Huyu Humprey Pole pole ni Fisadi ametafuna fedha nyingi sana za wafadhili zilitolewa kwa asasi anayoongoza Tanzania Youth Coalition (TYC) kwa ajili ya kukuza ajira na ujasiriamali miongoni mwa vijna kiasi cha wafadhili mbali mbali kusitisha misaada kwa asasi hiyo.