Siri kubwa kuliko zote kuhusu dunia yetu tambarare

JE Dunia ina umbo gani?


  • Total voters
    524
Mimi nawaambia dunia ni shimo....!
-----
Wala siyo flat. Kulijua hili, ni kupanda vindege vidogo wakati wa clear sky (hakuna mawingu) na kindege hicho kiruke futi zaidi ya elfu 25 katika eneo la bahari. Chungulia dirishani na utazame chini karibu kabisa na usawa wa ndege hiyo. Kisha anza kutazama hapo na kuelekea upande wa upeo wa macho yako kwa msitari fikirishi ulionyooka. Kwa haraka utagundua dunia ni shimo. Tena shimo la mviringo.

Kama ni suala kupiga kura, juu ya post ya kwanza ongeza kipengere kingine cha dunia ni shimo.
hahahahhaa usirudie kupanda Bombadier.....vioo vyake vina shida
 
Mkuu umenifurahisha sana kwenye introduction, unalazimisha tukuone mtu fulan hv uko nondo wakat hata kingereza chenyewe tu. .ni cha kuunga unga anyways copy and paste zako tumezipata. .umechagua somo zuri la kutushirikisha..tu mekusoma
 
Mtoa post hakika ungezaliwa ukiwa kwenye gari linalotembea na ambalo halisimami... basi upeo wako ungekuambia miti na vyote vilivyopo nje ya chombo hicho navyo vinatembea lakini opposite direction.... hapo ndio jua linapowafanya Wajinga.

Sehemu ambayo sayansi inawashinda wale wote mnaoipinga ni kwamba haina kiongozi kama vile sheikh au papa, una haki zote za kufanya experiment ya jambo lolote unalotaka ili ujiridhishe na ikiwezekana na wwe uje na tafiti yako inayosema vinginevyo lakini ikiwa na proof.. wana sayansi siku zote wanakinzana ili kuboresha na sio kupigana... ndio maana kuba awards kwa ajili ya kuwafanya watu wajitume kwenye tafiti ili kujibu maswali ya why??? ..... sayansi haipo kwa ajili ya kueleweka na watu wote ndio maana inaonekana ngumu sana kueleweka...
Kitu kingine Antarctica inapatika kusini mwa dunia.. lakini kama kuna ukingo kuzunguka dunia basi ukingo huo ungekuwepo mashariki, magharibi na kaskazini... je hauwezi kwenda australia kwa kupitia magharibi (yaani kupitia congo, Angola, amerika ya kusini) na kurudi ulipotoka.... je tutaona ukingo??
 
ukiamini dini ya fedha jua umeisha,hilo la usiku na mchana ni ushahidi tosha kuwa dunia ni tufe,hawa freemason wasituchanganye,mtu aliyeko marekani akitaka kwenda japani akielekea magharibi hafiki japani?mambo mengine hayatakiwi kutuchukulia muda kabisa.
 
Kama dunia inazunguka kwanini kila cku naona nyota hizo hizo haibadiliki kwa zaidi ya miezi 5
Mkuu haupo serious kama kweli unachunguza nyota utajua zinabadilika pia unaweza fuatilia mienendo ya sayari ambazo tunaweza kuziona toka huku duniani
 
Kama dunia inazunguka kwanini kila cku naona nyota hizo hizo haibadiliki kwa zaidi ya miezi 5
Mkuu haupo serious kama kweli unachunguza nyota utajua zinabadilika pia unaweza fuatilia mienendo ya sayari ambazo tunaweza kuziona toka huku duniani
 
Mkuu haupo serious kama kweli unachunguza nyota utajua zinabadilika pia unaweza fuatilia mienendo ya sayari ambazo tunaweza kuziona toka huku duniani
Brother, usipende kuamini mafundisho yote ya mzungu, nilijiwekeza muda kufuatilia nyota, na nikachagua nyota kadhaa zikizokaribina. Amini usiamini nyota hazibadiliki, only they change angle..kwa maana..kwa muda huo huo utaojiwekea kuzifatilia...leo utaziona nyuzi 90..baada ya siku kadhaa utaziona 110, Mara 60 Mara 40...lakini utaziona. Trust me..
 
Kama dunia inazunguka kwanini kila cku naona nyota hizo hizo haibadiliki kwa zaidi ya miezi 5
Ulitaka zibadilike baada ya muda gani??? Siku moja? Siku tano? Wiki? Mwezi etc....

Wazee wa zamani walikuwa wanaangalia patterns za nyota na hivyo kuweza kujua wako kwenye majira gani... kwani kila pattern huwa inajirudia baada ya mwaka mmoja.... kama kungekuwa hakuna mabadiliko kwenye nyota je wangewezaje kujua majira ya mwaka???

Hata hivyo nyota unazoziona leo zilikuwa sehemu hiyo miaka kadhaa iliyopita ukiondoa nyota ya jua ambayo ndio iko karibu.. inachukua dakika 8 mwanga wa jua kufika dunian, kwa maana hiyo kila unapoliona jua basi tambua kwamba lilikuwa hapo dakika 8 zilizopita....
Ukilitoa jua, nyota ya karibu kabisa mwanga wake unachukua miaka 4 kufika duniani, kwa maana hiyo nyota hiyo unapoiona basi ilikuwa hapo miaka 4 iliyopita.....kuna uwezekano mkubwa kwamba kuna nyota tunaziona leo lakini hazipo tena kwa wakati huu (ghost stars), zilishakufa.
 
Hapana kinachozunguka ni dunia na siyo jua,

Halafu mbona ukiwa nje ya dunia kila kitu kiko wazi aisee,actually hauko makini
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom