Siri Kali

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,048
The Citizen News
Posted Date:: 22.12.2007 @04:43 EAT

Govt mum on fate of BoT chief
By The Citizen reporter

Uncertainty persisted yesterday on the resignation of Bank of Tanzania Governor Daudi Ballali. Mr Salva Rweyemamu, the director of communications at the State House, still maintained that no official communication had reached the president regarding such a move by the governor. "So far we have no official communication about this matter," he said, elaborating that information about his resignation was only seen in some sections of the media. "That's what I can say," he told The Citizen yesterday.

Finance Minister Zakia Meghji also divulged no new ground on the issue, saying she wasn't aware the BoT governor had resigned. "I have no clue about what's going on," she said, promising yet another follow-up about the matter. Credible sources in the central bank were affirmative mid this week that the governor had resigned.

"The government was struggling to establish who leaked the information about the resignation of Mr Ballali," reliable sources indicated. Certain BoT officials were under pressure on the leakage, an official said, declining to be named.

"They (government) also want to establish the motive behind the leakage�we are terrified following the situation." Sharp divisions were being reported among top BoT officials, with some dejected that the governor "had been made a sacrificial lamb" to level off political pressures.

The group sympathetic with the outgoing governor says that huge payments at the central bank were done under orders of the government, not by the governor's discretion. "They used him when they were in deep financial straits but now having succeeded in their mission, the governor is becoming a liability�He has been made a scapegoat," a sad official snorted to The Citizen.

A less visible group comprising largely of non-sympathisers asserted that the governor had "failed to manage the central bank effectively during his tenure, paving the way for shady deals to take place within the institution." "The central bank's image has suffered during his leadership, with ghost projects mushrooming dramatically�He has made himself a sacrificial lamb," one of them disparagingly remarked.

Mr Ballali's resignation including details that a letter was received at the State House late Tuesday this week to that effect was top rumour in downtown Dar es Salaam. Other affirmative reports say his medical condition wasn't improving, after he was hospitalized in Boston, Massachusetts in a medical trip that has taken the better part of three months.

During a meeting with editors of print and audiovisual media, President Kikwete brushed aside suggestions that the governor had apparently found the controversy on the central bank unbearable, switching to the United States for a while.

The president affirmed that he was only aware of the governor's medical condition, and that it wasn't improving quickly enough. Some reports even suggested his health situation had declined in a 'dramatic' way.

The governor has been under pressure from opposition MPs led by Dr Wilibrod Slaa, the Chadema secretary general, whose entire political programme is focused on verifying payments at the central bank.

The bill for constructing the central bank twin towers, several times higher than putting up a similar building in New York, has used up countless hours in Parliament as far back as mid 2005 Budget session. Equally engaging is the situation in the external payments accounts, where the government pays arrears on the country's foreign debt.

With the twin towers bill put at around $400 million and EPAs payments chalking up twice as much according to internet documents, explaining all this has been a problem for the governor during the past half year.
 
Did you really need to come up with a new topic about this matter ? I thought we had this topic on here ?
 
Posted Date::12/22/2007
Maswali zaidi yamkabili Balali, serikali kuhusu BoT

Na Waandishi Wetu
Mwananchi

UVUMI kuhusu kujiuzulu kwa Gavana wa Benki Kuu Tanzania (BoT)Daudi Ballali kunazidisha maswali kufuatia pia kutokuwepo taarifa za wazi kutoka Ikulu ambako ndipo kwa mujibu wa taratibu alipo muajiri wa gavana huyo.

Taarifa za Ikulu zilizotolewa kwenye vyombo vya habari juzi zilieleza kutokuwepo na ukweli au uongo kuhusu Balali kuandika barua ya kuomba kujiuzulu. Taarifa hiyo ilieleza pia kuwa, Rais ambaye ndiye mwenye mamlaka kuhusu kukubali au kukataa kujiuzulu kwa Balali hakuwepo kufuatia kuwa likizo ya mwisho wa mwaka.

Taarifa kuhusu Balali kukimbia nchi kwenda nchini Marekani ambazo zilitolewa na viongozi wa upinzani, ambao kwa kipindi kirefu zaidi cha mwaka huu 2007 unaelekea ukingoni, walikuwa wakimtuhumu kutokana na matumizi mabaya ya fedha katika chombo hicho muhimu katika kudhibiti na kukuza uchumi wa nchi.

Mara kadhaa Balali amekuwa akikanusha tuhuma dhidi yake huku akifafanua kuwa, wanaomtuhumu wanafanya hivyo kutokana na wivu ama kufuatia kukosa baadhi ya mambo waliyotaka awafanyie bila kufuata taratibu.

Hata hivyo taarifa za ugonjwa wa Balali zinathibitisha na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Grey Mgonja na Waziri wake Zakhia Meghji Septemba 09, 2007 ikiwa ni kauli ya kwanza kabisa kutolewa na uongozi wa serikali kuhusu afya ya Balali. Taarifa zilizofuata baada ya wiki moja zilieleza pia kuwa, Gavana Balali alikuwa anaendelea vema, licha ya kwamba hazikueleza kuwa anasumbuliwa na nini.

Swali gumu linalowaumiza wachambuzi wa mambo ni kuhusu kuwepo tetesi juu ya matumizi ya fedha za BoT zinazohusishwa na kuchangia gharama za uchaguzi kwa chama tawala. Kama jibu la aina hiyo litakuwa la kweli, ni vigumu kwa Balali kuwekwa kitanzi wakati alikuwa akifanya kazi kwa maslahi ya dola.

Taarifa hizo mara kadhaa zimepingwa na uongozi wa CCM ambao umekuwa ukielezea kuwa, una mtaji mkubwa wa wanachama wenye uwezo mbalimbali hivyo hauwezi kutumia njia za panya kusaka fedha za kampeni.

Jambo la wazi ni kuwa, Balali ni mgonjwa lakini swali lingine ni hili la kuhusu uwepo wa Jakaya Kikwete nchini Marekani wiki iliyopita, safari ambayo anaelezwa kuwa alimtembelea Balali kumjulia hali.

Baada ya Kikwete kufika nchini siku mbili baadaye, ndipo kunaanza kuwepo uvumi wa Balali kuandika barua ya kujiuzulu huku akipinga kauli yake aliyowahi kuitoa Julai 12, 2007 alipowaambia waandishi wa habari kuwa hajiuzulu ng'o, baada ya kutakiwa kufanya hivyo na wapinzani.

Lakini swali lingine ni lile la kupewa wasaidizi wengi tofauti na ilivyotarajiwa kwamba Rais Kikwete angempumzisha kazi. Julai 11, 2007 kulipatikana taarifa kutoka Ikulu ikieleza kuwa Rais Kikwete ameteua Manaibu Gavana watatu ambao aliwapanga kuwa chini ya Balali.

Taarifa hii ilielezwa kama njia ya kuanza mkakati wa kumuondoa Balali lakini Ikulu ikafafanua kuwa, malengo ya rais yalikuwa kuifanya BoT kufanya kazi vema zaidi.

Manaibu Gavana walioteuliwa ni; Profesa Benno Ndulla, Lila Mkila na Juma Reli. Lakini jambo lililojionyesha wakati huo baada ya uteuzi ni hili la Balali kwenda matibabu ambayo yupo hata sasa.

Lakini jambo jinginr ni kama Rais Kikwete atapokea kujiuzulu kwa Balali huku ikitangazwa kuwa wiki ijayo ripoti ya ukaguzi wa BoT itakuwa inawekwa hadharani. Ni wazi kama Balali atahusishwa moja kwa moja na tuhuma zinazomkabili ama zile zilizoko chini yake kama Gavana atatakiwa kuwajibishwa.

Pia inawezekana Ikulu ikawa tayari na taarifa kuhusu ripoti hiyo ya ukaguzi na hivyo safari ya Kikwete Marekani ikaambatana na kumtaka Balali kujiuzulu ili kupoza mambo. Bado kuna ugumu maana ripoti hiyo inayotangazwa kutoka wiki ijayo, inaelezwa pia kuwa imekuwa ikijadiliwa kimya kimya na taasisi mbalimbali za serikali hali inayotoa maswali kuhusu usafi wake na kama itabakia ile ile iliyoandaliwa na kampuni la kigeni la Ernst&Young.

Baadhi ya tuhuma ambazo zimekuwa zikielekezwa kwa Balali na BoT ni pamoja na ujenzi wa jengo jipya la Benki Kuu (Twin towers) kwa gharama kubwa.

Baadhi ya wabunge walitaka maelezo ya kina kuhusu sababu za matumizi ya dola za Marekani 340 milioni sawa na Sh425 bilioni kujenga jengo hilo, wakati lingeweza kujengwa kwa gharama ndogo zaidi.

Tathmini ya wataalam wa ujenzi zinasema kuwa gharama za ujenzi huo ni zaidi ya mara mbili ya gharama za kujenga jengo la aina hiyo katika miji maarufu ya nchi zilizoendelea kama London, New York au Tokyo.

Pia zipo tuhuma kuhusu uidhinishaji wa malipo ya dola za Marekani milioni 200 sawa na Sh250 bilioni, kwa ajili ya miradi isiyoeleweka na kuidhinisha ada kubwa za mawakili wa kutetea kesi za Benki Kuu.

Tuhuma zingine ni kuidhinisha malipo hewa ya madeni ya nje (EPA) na matumizi ya kampuni ya Deep Green Finance ya Afrika Kusini.

MATUKIO MBALIMBALI KUHUSU TAARIFA ZA BoT


Desemba 20: Inaripotiwa kuwa Gavana Balali ameandika barua ya kujiuzulu akiwa nje ya nchi, Ikulu na Wizara ya Fedha zinasema kuwa hazina taarifa.

Desemba 19: Meghji anatetea kuchelewa kwa ripoti ya BOT.

Desemba 01: Dk Wilbrod Slaa anaelezea kukerwa na usiri wa Ripoti ya ukaguzi wa hesabu za BoT.

Novemba 29: ukaguzi wa hesabu za BoT unakamilika na inaelezwa ripoti hiyo kufika kwa mkaguzi mkuu wa mahesabu ya serikali.

Septemba 22: wafadhili wanadai ufafanuzi wa tuhuma za ufisadi zinazoihusu BoT.

Septemba 20: Hali ya Gavana Balali inaripotiwa kuendelea vizuri.

Septemba 16: Wananchi wataka msimamo wa tuhuma za BoT na nyinginezo kutoka kwa Rais Kikwete.

Sept 15: Dk Slaa wanahutubia mkutano wa hadhara Mwembe Yanga Temeke, kisha anataja orodha ya waliowaita mafisani wanaotafuna nchi, akimjumuisha na Balali.

Septemba 14: Afya ya Gavana Balali inagubikwa na utata, lakini inaelezwa kuwa yuko nje nchi kwa matibabu.

Septemba 11: Kampuni ya Ernst&Young iliyoteuliwa kupitia hesabu za BOT katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ili kubaini ukweli kuhusu ubadhirifu wa fedha, inaanza kazi.

Septemba 09: Inaripotiwa kuwa hali ya Gavana si nzuri, hivyo amepelekwa nje ya nchi kwa uchunguzi na matibabu.

Agosti 19: CHADEMA inajibu mapigo ya Spika dhidi ya Slaa na hoja ya BoT.

Agosti 18: Spika anamtuhumu Dk Slaa kuwa ameghushi nyaraka alizotaka kuzitumia dhidi ya BoT na kutishia kumshitaki.

Agosti 16: Slaa anachomoa hoja binafsi ya BoT Bungeni akidai kuwa inaonekana hakuna nia njema, hasa baada ya mbunge mwenzake Zitto Kabwe kusimamishwa baada ya kuwasilisha hoja yake iliyokataliwa na wabunge wa CCM. Anaahidi kuipeleka kwa wananchi na kwa wafadhili, lakini pia anadai kutishiwa maisha.

Agosti 12: Muda wa Balali kustaafu uliainishwa kupitia vyombo vya habari, muda huo uliainishwa kuwa ni Juni mwaka 2008.

Julai 13: Gavana Balali anakataa hoja iliyoelekezwa kwake na wapinzani waliomtaka kujiuzulu kwa manufaa ya umma. Yeye anasema hajiuzulu kamwe.

Julai 12: Balali anapunguziwa mzigo na alipewa manaibu watatu kumsaidia.

29 Juni: Serikali kupitia kwa Waziri wake wa Madini na Nishati inamsafisha mke wa Gavana Daudi Balali aitwaye Ana Muganda kuhusu tuhuma ya yeye kutumia nafasi ya mumewe na kisha kuwa mkurugenzi katika moja ya makampuni ya madini ya dhahabu hapa nchini.

27 Juni: IMF inatoa taarifa kupitia kwa Naibu Mkurugenzi wake Murilo Portugal akitaka uwazi uwepo katika suala la kuichunguza BoT.

Juni 26: Mjadala unatanuka kuhusu tuhuma za ufujaji fedha BoT na safari hii mbunge wa CCM Ole Sendeka anataka iundwe tume ya kuichunguza BoT.

Juni 25: Mbunge wa Karatu Dk Wilbrod Slaa anatoa dai Bungeni akitaka Gavana wa Benki Kuu David Balali ajiuzulu.

Juni 15 Bunge la Bajeti linakaa na Bajeti ya mwaka 2007/08 inasomwa na Waziri wa Fedha Zakhia Meghji.
 
janja yao tu wanatuchezea akili na kutaka kuhamisha mawazo yetu badala ya kudai ripoti tuelekee kujadili fisadi waliye mwambia wao ajiuzuru!

Wakati tukiwa bize kuangalia ya bilali wao huku wanabadili ripoti yote na kujisafisha!

Lakini walizoea vya kuchinja nadhani hili na BOT limenyongwa.. tutakula nao tu!
 
hii serikali yetu ishatufanya sie watoto saaana!ila za mwizi siku zote ni arobaini...now wanachezea siku za thelathini na kitu
 
Ndio maana sisi wengine tulisha suspect kwamba hawa jamaa huenda wako kutupikia hii ripoti ya Ernst hii Desemba na kuja na madudu yao. Lakini tutakomaa nao tu.
Mwaka huu hatukubali kupikiwa!
Hii ya Balali kujiuzulu ni changa la macho tu ili kutupotezea concentration na attention!
 
Kama kuna mtu anategemea lolote kuhusu hiyo ripoti itakuwa ni kichekesho. Hiyo ripoti imewafikia wenyewe na wao ndio wenye uwezo wa kuamua. Hakuna mtu atakayechukuliwa hatua, kafara atakuwa Balali tu napo kwa kujiuzulu, wale wote waliotajwa kwenye list of shame watapeta tu. Huo uchunguzi ulikuwa ni kuwazuga donar community na ku ease political tension hapa Tanzania.
Ukitaka kuami ninayosema kwanza subiri uone kama mtu yoyote ataondolewa uwaziri, subiri uone kama mtu yoyote atafikishwa mahakamani, subiri uone kama mtu yoyote anayeshutumiwa hatagombea ubunge na kushinda 2010, hii ni geresha tu. Ninachoweza kukuhakikishia ni kuwa subiri uone mwaka 2010 kama Slaa atagombea au kupita ubunge, huenda huu ndio mwisho wa yeye kuwa mbunge.
And WTANZANIA SOON WATASAHAU KUHUSU RIPOTI HIYO na watu wataendelea kula kama kawaida, let us wait and see.
 
Back
Top Bottom