SoC01 Siri inayoweza kukusaidia kama unashindwa kuanza jambo lako

Stories of Change - 2021 Competition

Kibenje KK

JF-Expert Member
May 28, 2016
267
380
Miaka mitano iliyopita nilipata wazo la kugeuza taaluma yangu ya ualimu na passion ya usomaji, kujifunza na kufundisha kuwa ajira. Nikawa na mpango wa kufundisha Kwenye radio, TV, semina, makongamano, vyuo na taasisi mbalimbali na kuzalisha podcast zangu.

Nikamshirikisha rafiki yangu mmoja niliyemuamini juu ya wazo langu. Akanishauri na kusema ni wazo zuri lakini sio vyepesi kama ninavyofikiria. Akasema hii kazi inahitaji sana uzoefu, uwe na pesa za mtaji kama ofisi uvae vizuri, uwe na laptop na projector za kufundishia.

Akasema, unapaswa pia kuwa na watu wa kukusaidia na bao ni wataalamu wa mambo ya mitandao na connection. Kiukweli nilitoka hapo nimeishiwa nguvu. Baada ya wiki niliamua kuwa nashare baadhi ya jumbe mitandaoni.

Watu taratibu wakaanza kupenda mafunzo yangu na idadi kuongezeka huku wakiniita kufundisha sehemu zao bure kwa miaka kadhaa mpaka Kuanza kulipwa. Inawezekana ningesubiri kuwa na ofisi, laptop, suti za kutosha leo ningekua sijafanya chochote.

Nilivyoanza sasa nimejuana na watu muhimu, watu wengi wananifatilia, mitandaoni na nimetembea redio na TV mbalimbali na kufundisha sehemu nyingi Tanzania.

“UKISUBIRI UWE NA KILA KITU NDIO UANZE, HUTAANZA KITU".

Watu wengi hunifuata, wana vipaji au mitaji midogo ya kuanza biashara na hawajui wafanyeje. Hata kazi za kuajiriwa huziwezi kukuta uko nyumbani tu.

Huwa nawaambia watu "Namna ya kufanya utajua ukiwa unafanya" ANZA. Uzoefu,connection, ujuzi utajua ukishaanza kufanya. Huwezi kufika unapopatamani kwa kufikiria tu. Anza kwenda. Anza na mtaji ulio nao,anza na watu ulionao, anza na vitu ulivyonavyo, anza na followers ulionao.

Anza na ngazi ya kwanza, kisha endelea kupanda mpaka juu.Unachokitaka utakipata ukianza.

Tuanze taratibu.

Nadhani ata wewe una ushahidi kuna mambo hukujua kama unayaweza mpaka ulivyoanza.

ANZA.
 
Back
Top Bottom