siri imefichuka.sasa afanyeje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

siri imefichuka.sasa afanyeje?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by fundiaminy, Jul 2, 2009.

 1. fundiaminy

  fundiaminy JF-Expert Member

  #1
  Jul 2, 2009
  Joined: Jun 4, 2009
  Messages: 358
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Jamaa amekuwa aki date demu kwa mda wa mwaka mzima.na ni mengi wameongea na ikafika tym ya kwenda kwa wazazi wa msichana kujitambulisha.walipofika tu,watoto wawili mapacha umri miaka minne walikuja mbio wakiita mummy.jamaa roho ilikuja mdomoni na kwa hasira akamuuliza mchumba mtarajiwa mbona hukunieleza kwamba ulizaa?kwa kweli jamaa alikuwa amempenda huyo msichana na sasa yuko kwa njia panda.asaidiweje??
   
 2. M

  Malila JF-Expert Member

  #2
  Jul 2, 2009
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Ukipenda boga penda na maua yake !!!!!!! Kwa mfano asingemkuta na watoto,halafu mara baada ya kuoana akagundua kuwa huyo mkewe anakoroma usiku kucha angefanyeje? Ashukuru kumbe mchumba wake ana uzazi.
   
 3. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #3
  Jul 2, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Apige chini mzigo..

  Kama huyo mwanamke alidanganya kuhusu watoto wake wa kuwazaa..huko mbele ataogopa nini kudanganya kuhusu makubwa zaidi ya haya?.
   
 4. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #4
  Jul 2, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,067
  Trophy Points: 280
  Kama hayupo tayari kuishi na mwanamke aliyekwisha zaa na bwana mwingine, ni vema akatafuta mwanamke mwingine.
   
 5. Akili Unazo!

  Akili Unazo! JF-Expert Member

  #5
  Jul 2, 2009
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 2,757
  Likes Received: 2,349
  Trophy Points: 280
  aendelee naye kwani hana kosa na kuzaa kwake kote si yupo mbomba kama hajazaa vile?eti!!!!?kama hakuona tofauti hiyo kabla basi aendelee na utaratibu wa kumuoa.

  Wakuu mnajua tumekuwa tukihukumu sana kwamba wachmba wetu wamezaa na mtu mwingine ebu tujiulize,kama alizalishwa akiwa form four halafu kwa uzuri wake hakutoa hiyo mimba kama wafanyavo hawa tunaowaoa tukidhani hawajazaa wakati wametoa mimba kibao huoni kuwa alifanya kitu cha busara.mi naomba sana kama shemeji yangu asimtengee na aendelee naye tu na wakubali kumalizia hatua iliyo baki kuzaa sio tatizo.
   
 6. L

  Lubaluka JF-Expert Member

  #6
  Jul 2, 2009
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 496
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Katika wapendanao uaminifu na ukweli ni nguzo moja nzito katika mahusiano. Huyu mwanamke si mkweli wala mwaminifu !!! Huwezi ficha siri kama hio..your own kids. Angemweleza ukweli mwenzi wake na wakikubaliana mambo yangekua bomba.. Je kama ameweza ficha jambo kubwa kama hilo, je hayo madogo madogo si ya hatari zaidi... Naomba jamaa amuache huyo demu na ajipanga upya.....
   
 7. D

  Dina JF-Expert Member

  #7
  Jul 2, 2009
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 2,824
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Issue yake ni kukosa kuambiwa ukweli au mzigo wa responsibility wa kulea mapacha kabla wa kwake hawajaanza kuja au hataki kabisa kuwaona hao watoto?

  Kuna ukweli kabisa wa watarajiwa kushindwa kuwa wakweli pale linapoingia suala la kuwa na watoto kabla ya ndoa. Kwa upande wa akina dada, wengine huwa na uoga kuwa je nikisema ndio utakuwa mwisho na huyu baba au vipi? Kwa upande wa akina baba, sina uhakika kama na wao wanakuwa na hisia hizi hizi au they just choose not to say...labda na wao watatusaidia mawazo. Ila kwa wawili watatu ninaowafahamu, they were proud of their watoto na kuwasemea point black! Hata hivyo, 'dhambi' si inakuja mdada akiwa na mtoto na siyo mkaka, so why the worry?

  Cha msingi, nafikiri yanazungumzika..aongee vyema na huyo dada kujua sababu za yeye kutokuambiwa ukweli. Lakini mwisho wa siku uamuzi anao yeye mwenyewe, kama anaona hilo kwake yeye ni kosa kubwa ambao halina mjadala, basi asonge mbele! Kuliko baadaye ndio liwe la kukumbushia kila anapoudhiwa na huyo mwenzi wake.
   
 8. m

  muhanga JF-Expert Member

  #8
  Jul 2, 2009
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 873
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  jamani msiwe unfair! wanawake wakiza kabla ya kuolewa inakuwa issue kubwa sana, ila wanaume wakileta watoto wa kabla na hata baada ya ndoa eti shetwani aliwapitia!!! mi naamini kuzaa si tatizo kabisa, labda umhukumu kwa kutokuwa muwazi, lakini kwa upande mwingine angesema ukweli mimi ni mama wa twins huyo mwanamume angemtaka?? kama hakuon kasoro yoyote kwa siku za nyuma hadi alipoona watoto, je haoni kama huyo mke bado ni mzuri tu kwake? mimi binafsi nilizaa kabla ya kuolewa na mume wangu alizaa kabla ya kunioa, tumeona hadi leo tuna miaka zaidi ya 10 hatujajaaliwa kupata mtoto mwingine tumebaki tunalewa mtoto wa mume, wa kwangu alichukuliwa kwa babake, tuna amani, maisha matamu, upendo na furaha tele! maisha ni vile mtakavyoamua nyie 2
   
 9. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #9
  Jul 2, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Duh hapo mkuu jamaa namshauri aaachane nae huyo binti kama wamekaa mwaka mmoja na mwanamke hakuwahi tamka kuwa ana watoto basi huyu mwanamke si mwaminifu cha msingi jamaa aachane nae mwambie kabisa apige chini atakuja kulea hata mimba ambayo si yake hivi hivi mashori wa design hii mmh! anakubambika mtoto hivi hivi. Mashori wapo na wanaendelea kuzaliwa aachane nae kabisa.
   
 10. Akili Unazo!

  Akili Unazo! JF-Expert Member

  #10
  Jul 2, 2009
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 2,757
  Likes Received: 2,349
  Trophy Points: 280

  Tusiegemee upande mmoja what if kama dada angeolewa halafu akakuta mwanaume anamtoto je reaction ingekuwa kama alivyoreact?

  kikubwa hayo ni mambo ya kukaa chini na kuongea kwani inawezekana hakuzaa kwa kutaka na inawezekana alizaa akiwa na umri mdogo au alipata mimba ila hakuitoa kama dada zetu walio wengi wafanyavyo wa kuua kiumbe kischo na makosa.

  kikubwa atulie na kuongea naye kwa kuwa hata kabla ya kwenda kujitambulisha watoto walikuwa wanaishi kwa raha.
  yeye anachokataa ni majukumu au familia kubwa au kulea watoto wa baba mwingine?
   
 11. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #11
  Jul 2, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Alipouliza hivyo ye alijibiwaje? kwa nini mchumba hakusema kama ameshazaa? Hebu tuhabarishe tujue zaidi
   
 12. Nyabwire

  Nyabwire Member

  #12
  Jul 2, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  to be frank,kitendo cha huyo msichana kumficha mchumba wake juu ya watoto ni kosa,hatuwezai kujustfy kwa namna yeyote ile.swala la kuangalia ni kama huyo jamaa yuko tayari kumsamehe ili waendelee na mipango yao,kama hayuko tayari kumsamehe,ikiwa ni pamoja na kukaa na hao watoto,sioni sababu ya kwanini waendelee kuwa wote,sababu litabaki kuwa kovu tu moyoni kwa huyo kijana.ila huyo msichana lazima ajue tu kuwa,amejipotezea uaminifu kwa huyo kaka hat akama wataamua kuoana.
   
 13. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #13
  Jul 2, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Swala kubwa siyo kupenda "boga na maua", swala lubwa ni udanganyifu uliofanyika, kwa nini huyu mama hakusema tangu mwanzo? Kama kaficha hili kuna mengine yepi kaficha? Kama kaficha hili hata kama akiolewa mumewe kila siku atakuwa na hisia kwamba inawezekana kuna kitu anafichwa, maisha gani hayo?

  I say apige chini mzigo as well, alitaka kumuoa kwa kujua hajazaa na alifichwa kwamba amezaa, hii ni sababu tosha.Uaminifu ni kitu kikubwa.
   
 14. Mtabiri

  Mtabiri Senior Member

  #14
  Jul 2, 2009
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 152
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mnapoanza mahusiano ni muhimu kuwekana sawa ili mtu akukubali ulivyo sio kufichaficha. Inawezekana basi kuamini kua kuna jamaa mwingine anaendelea kummega kwa siri, hilo pia atakuja kuligundua baada ya kuoana. Au wakishaingia kwenye ndoa atagundua kingine...kumbe mwanamke anakatabia ka udokozi. The first impression matters!
   
 15. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #15
  Jul 2, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mwanajamii habari ndo hiyo jamaa akaenda kwa wakwe kaona watoto mapacha wanamwita mama mama jamaa akashtuka kuingia getto kwa mchumba akamwambia wale watoto wangu ndio.
   
 16. Kiteitei

  Kiteitei JF-Expert Member

  #16
  Jul 2, 2009
  Joined: Jan 14, 2009
  Messages: 1,252
  Likes Received: 147
  Trophy Points: 160
  tusimlaumu sana huyu dada, yawezekana kuwa mdada alikuwa anaumia kwa hilo na huenda pia alishindwa kumwambia hivyo akaamua kumpeleka akashuhudie na kutoa maamuzi, naamini angekuwa na nia ya kuendelea kumficha huyu bwana angeweza! ingekuwa rahisi sana kupanga na wazazi wake wakawaondoa hao watoto na kuwaficha hadi watakapoondoka lakini hakufanya hivyo! hivi ni kwa nini linapokuja swala la kuwa na mtoto kabla ya ndoa kwa wanawake inakuwa dhambi/aibu isiyosameheka?
   
 17. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #17
  Jul 2, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  KOSA KUBWA LA MDADA HAPO NI KUUFICHA UKWELI! halafu bongo nyingine bwana, sasa yeye alivyojua anaenda kutambulisha mchumba na hakutaka mwanaume ajue kwanini acngefanya maarifa ya hao watoto basi hata wapelekwe mbali kwa cku hiyo ili amalize shughuli yake? khaa watu bwana gemu ya kijinga sana! haoni raha yeye kuitwa mama mpaka afiche? ukipendwa unapendwa tu hata iweje so sioni sababu ya yeye kushindwa kumwambia ukweli huyo mchumba wake, adhabu yake ni aachwe tu.
   
 18. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #18
  Jul 2, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mi wanawake waongo adhabu yao ni talaka tu pale pale uhusiano unakufa moja kwa moja kwa nini anidanganye mi siku zote ni mkweli na hii inanisababishia kukosa mashori.
   
 19. Tshala

  Tshala JF-Expert Member

  #19
  Jul 2, 2009
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 246
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Tuwe wakweli jamani huyu dada anakaribia kuolewa!! amekaa na jamaa mwaka mzima!! kweli ameshindwa kumwambia jamaa kuwa ana watoto? Your own kids mtu unashindwa kuwa proud nao??? ina maana yeye Man comes first than her own kids? Poor her. Kaka huyo dada hakufai ni mengi sana amekuficha, kuishi na mtu ambaye mwanzo tu ameweza kudanganya hivi then mtakapokuwa mume na mke?? Let her learn thru her mistakes, it seems bado anatembea na baba wa hao watoto...
   
 20. m

  muhanga JF-Expert Member

  #20
  Jul 2, 2009
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 873
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  mi naona akwepa majukumu, kusomesha twins si mchezo:):)
   
Loading...