siri imefichuka:kumbe kamatakamata ya Tanesco ni kwa ajili ya haya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

siri imefichuka:kumbe kamatakamata ya Tanesco ni kwa ajili ya haya

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mkurabitambo, Sep 7, 2012.

 1. M

  Mkurabitambo JF-Expert Member

  #1
  Sep 7, 2012
  Joined: Feb 3, 2010
  Messages: 229
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  MAHAKAMA Kuu Kanda
  ya Dar es Salaam,
  imetupilia mbali
  maombi ya Shirika la
  Umeme Tanzania
  (Tanesco) kutaka
  isitishe utekelezaji wa
  malipo ya Sh96 bilioni
  kwa Kampuni ya Kufua
  Umeme ya Dowans
  kutokana na kuvunja
  mkataba wa kibiashara
  kinyume na sheria.
  Kufuatia uamuzi huo,
  Tanesco sasa inatakiwa
  kuilipa Dowans kiasi
  hicho cha fedha
  ambacho kwa ujumla
  kinaliongezea shirika
  hilo mzigo wa madeni.
  Tanesco kupitia
  mawakili wake Rex
  Attorneys iliwasilisha
  mahakamani hapo
  maombi mawili; kibali
  cha kukata rufaa
  kupinga hukumu ya
  Mahakama hiyo
  iliyotolewa Septemba
  28, 2011 na kuomba
  kusimamishwa kwa
  utekelezwaji wa
  hukumu hiyo.
  Katika hukumu ya
  awali iliyotolewa na Jaji
  Emilian Mushi,
  mahakama hiyo
  ilikubali maombi ya
  Tuzo kwa Dowans
  iliyotolewa na
  Mahakama ya Kimataifa
  ya Usuluhishi wa
  Migogoro ya Kibiashara
  (ICC), Novemba 15,
  2010.
  ICC iliamuru Tanesco
  kuilipa Dowans fidia ya
  Dola za Marekani
  billion 65,812,630.03,
  kutokana na kuvunja
  mkataba wa kibiashara
  kinyume cha sheria.
  Mahakama Kuu
  Tanzania ilikubaliana na
  tuzo hiyo na kuipa
  kampuni hiyo nguvu ya
  kisheria.
  Source mwananchi
   
 2. Philipo Kidwanga

  Philipo Kidwanga Verified User

  #2
  Sep 7, 2012
  Joined: Jul 12, 2012
  Messages: 2,063
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  nchi inazidi kuzama hii jk anaendelea kujichotea mpunga wake yeye na maswahaba,miaka hii mboni tutakiona.
   
 3. G

  Gasper Buberwa Member

  #3
  Sep 7, 2012
  Joined: Jul 30, 2012
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kiukweli heli deni halikwepeki kwa TANESCO ila cc wananchi tutakandamizwa sana na hao TANESCO due to monopoly market coz we dont have alternatives.
   
 4. Aleyn

  Aleyn JF-Expert Member

  #4
  Sep 7, 2012
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 10,228
  Likes Received: 13,680
  Trophy Points: 280
  Watanzania huyu Jk mpaka 2015 ni mbali sana.
   
 5. k

  kalcha Member

  #5
  Sep 8, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 79
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  True aleyn, unataka kuweka mkakati wa kumtoa kwa kukosa imani nae?
   
 6. m

  massai JF-Expert Member

  #6
  Sep 8, 2012
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  chenge huyo,mzee wa vijisenti alafu bungeni kapewa tena uongozi aeendelee kutuu miza,hii mijitu ya jahkaya hovyo kweli
   
 7. D

  Deofm JF-Expert Member

  #7
  Sep 9, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 383
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Issue ya Dowans ni ya JK na wala sio dili ya mtu mweingine yeyote, Lowasa alijaribu kuliibua katika mkutano wa halmashauri kuu ya chama chao, mkapa akashauri ipigwe nyundo. Sasa hivi chama kinahitaji fedha kwa ajili ya uchaguzi pamoja na kufufua uhai wa chama hicho matawini. kwa hiyo fidha hizo naamini ni mgawo wa mapacha watatu pamoja na chama chao.
   
 8. ngalelefijo

  ngalelefijo JF-Expert Member

  #8
  Sep 9, 2012
  Joined: Jun 26, 2012
  Messages: 1,800
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  si mlimchagua eti ana sura nzuri, na bado.................................
   
 9. C

  CHOMA Senior Member

  #9
  Sep 9, 2012
  Joined: Aug 22, 2012
  Messages: 117
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kufa hatufi lakini cha moto tutaendelea kukiona.2015 itakuwa kama mwongo mmoja.
   
 10. Tripo9

  Tripo9 JF-Expert Member

  #10
  Sep 10, 2012
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 2,168
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Mbona siku hizi kila kitu ni habari?! Kwani mtu/kampuni ikidai chake ni tatizo. Shirika liwe na madeni, lisiwe na madeni linapodai madeni yake kutoka kwa wateja wake au kuwashughulia wanaojiunganishia umeme kinyemela, hiyo ni haki yake ya kimsingi kabisa.
  Wassalam
   
Loading...