Story of Change Siri iliyopo nyuma ya Biashara ya 'kujiuza' - Athari na hatua za kuchukua

MoseeYM

Senior Member
Jul 19, 2021
125
250
YANAYOENDELEA ZINAKOFANYIKA BIASHARA HIZI
Uchunguzi wangu umebaini kuwa maeneo ambayo biashara hizi zimekuwa zikifanyika hasa ndani ya jiji la Dar es Salaam, wahusika wamekuwa wakitumia bangi na vilevi vikali kwa kile ambacho wamekuwa wakidai hufanya hivyo ili ‘kujitoa ufahamu’ wasione aibu wafanyapo mambo hayo, mathalani maeneo ya Sinza- Africa sana ambapo nyakati za usiku vibanda vingi hufunguliwa ambapo watu hao hujaa. Tunaweza kusema kwa tafsiri rahisi, biashara hii imekuwa ikiambatana na uuzwaji wa bangi na pengine hata aina nyinginezo za madawa ya kulevya suala hili linaweza kuwa chanzo mojawapo cha kuundwa kwa ‘magenge’ mbalimbali ya uhalifu.

Maeneo mengine wanaojihusisha na biashara hizi,wamekuwa wakidai kuporwa wakiwa njiani au wakiwa ndani na wanaowaita ‘wateja’ wao ambao kwa tafsiri nyingine ni ‘vibaka’ ambao huwa wakizunguka zunguka maeneo hayo wakitafuta riziki kwa kupora watu. Baadhi yao Wanadai kupigwa, kupokea vitisho au kunusurika kuuawa na wengine kuuawa wakiwa kwenye maeneo hayo ya ‘kazi’. Wanaouawa kesi zao hushindwa kufika mbali kutokana na ukweli kwamba wanakuwa ni watu ambao hawajulikani na wenyeji wa maeneo hayo, mathalani, mmojawao na wanaojihusisha na biashara hii alidai kuwa kuna ‘mwenzao’ mwenye asili ya kinyarwanda aliuawa maeneo hayo, lakini hakutambulika alipokutwa ameuawa.

JITIHADA ZINAZOFANYIKA, UTHABITI NA UDHAIFU WAKE

Zipo jitihada mbalimbali ambazo zimekuwa zikifanywa na serikali katika kupambana na suala hili kwa sabau sheria za nchi zinatambua kuwa ni biashara haramu. Hivyo mara kadhaa askari huzungukia maeneo yanayosadikika biashara hizi kufanyika na kukamata wahusika.

Uchunguzi umebaini kuwa siku ambazo askari huamua kusaka’’ vijiwe’ vya biashara hii maeneo huwa kimya na biashara huwa haziendelei au hata kama zinakuwa zinaendelea ni kwa kiasi kidogo sana na kwa usiri mkubwa sana. Hivyo, hakuna budi jitihada hizi ambazo huoneshwa na askari polisi kuwa ni mwendelezo wa kila siku kwenye maeneo hayo kwani zinaweza kusaidia kupunguza uhalifu wa aina nyingine ambao unawezekana kuwa ukitendeka maeneo hayo.

Kwa upande mwingine askari ‘sungusungu’ wamekuwa na msaada kwa baadhi ya maeneo ambako shughuli hizi hufanyika kwani huwakamata wahusika na kuwawajibisha kisheria.Japokuwa mbali na jitihada hizo ,uchunguzi wa siri wa mwandishi umebaini kuwa shughuli zimekuwa bado zikiendelea kwenye maeneo hayo kutokana na baadhi ya sungusungu wasio waaminifu kupokea ‘hongo’ ya pesa kutoka kwa wahusika ili kutowabugudhi wakati wakiendelea na biashara zao.Hili limepelekea biashara hii kuonekana kana kwamba ni ‘sugu’ kwa maeneo hayo.

MAGONJWA YA NGONO
Uchunguzi wa siri wa mwandishi kupitia mahojiano na baadhi ya wahusika ,umebaini kuwa wengi wao wanaishi na maambukizi ya virusi vya UKIMWI. Jambo hili linaonekana kuchukuliwa si tatizo kwa wahusika kutokana na kuamini kile wanachokiita ‘matumizi ya kinga’ hivyo kudai haiwezi kuwaathiri wao ,ijapokuwa wataalamu wa afya wanadai kuwa matumizi ya kinga hayatoi uhakika wa asilimia mia moja.kwani pia hutegemea matumizi.sahihi ya kinga.

Taarifa za karibuni kutoka UNAIDS imeonesha kuwa 37% ya wanaojihusisha na biashara za 'kujiuza' katika nchi ambazo hazijahalalisha,wanaishi na maambukizi ya VVU. Hii ni sawa na mmoja kati ya wanne wanaojishughulisha na biashara hizi anaishi na maambukizi ya VVU. Takwimu za maambukizi ya VVU kwa mwaka 2019 nchini zilionesha kuwa kuna maambukizi mapya 58,000. Maambukizi ya magonjwa mengine ya ngono yameonekana kukua hadi kufikia 5%,Huku ripoti ya WHO ikionesha kuwa huchangia kushuka kwa uchumi kwani gharama za matibabu huwa kubwa,lakini pia waathrika wakubwa ni vijana ambao ni tegemeo kwa uchumi wa nchi.

MAGONJWA MENGINE

Homa ya Ini.

Wataalamu wa afya wanadai kuwa kushiriki tendo la ndoa na mpenzi zaidi ya mmoja ni mojawapo wa vyanzo vikuu vya Ugonjwa wa homa ya ini (Hasa kirusi B na C ),ambavyo huchangizwa na jasho au majimaji.Kwa hivyo 'wanaojiuza' na 'wanunuaji' wapo katika hatari kubwa ya kupata ugonjwa huu.ikumbukwe kuwa njia ya kupata ugonjwa huu ni rahisi kuliko hata VVU ,kwani hata jasho huweza kuwa kisababishi.

UVICO-19

Tangu mwishoni mwa mwaka 2019,Dunia imekuwa ikikabiliwa na janga la ugonjwa wa Virusi vya Corona.Hapana shaka,kuwa wanaojihusisha na biashara za 'kujiuza' wapo katika hatari kubwa ya kupata maambukizi,kutokana na biashara ambayo huifanya huhusisha moja kwa moja migusano na 'wateja wao.Mbali na kuwepo na ugonjwa huu mpya ,bado biashara hizi zimekuwa zikifanyika,huku wahusika wakionekana kupuuzia'.Hakuna takwimu zinazoonesha kundi hili limeathiriwaje na ugonjwa huu,lakini haitii shaka kuwa kundi hili ni miongoni mwa makundi yaliyo katika hatari zaidi ya kupata na kuusambaza ugonjwa huu ,endapo biashara hizi zitaendelea

MTAZAMO WA KIMAADILI
Katika jamii yetu ya Tanzania ,suala la mabinti ama wanawake ' kujiuza' halikubaliki kwani ni kinyume na maadili.Suala la kuoa au kuolewa huonekana kuwa ni jambo la kheri na ustaarabu, kwani huonesha watu hao wamehalalishwa na hakuna mahusiano mengine yanayoruhusiwa nje ya mpango wa ndoa, kufanya hivyo huonekana ni kosa. Tafsiri rahisi ni kwamba, kuoa au kuolewa ni mojawapo ya njia ya kuondoa hali ya kuwa na mahusiano mengi ya 'kingono' (Ukiachana na sababu nyinginezo za lengo la ndoa).Viapo vya ndoa za kidini pia huashiria kukataza mahusiao ya kimapenzi nje ya ndoa

NINI KIFANYIKE?
Jamii ya maeneo ambako biashara hizi hufanyika.Ina nafasi kubwa sana ya kuzuia kufanyika kwa biashara hizi,kwani kuna athari kubwa kwao kuacha ikiendelea kufanyika.Watoto wadogo wakiendelea kuliona likifanyika kuna hatari ya kutengeneza kizazi kisicho na maadili cha baadae.

Ni muhimu wazazi na walezi kushirikiana kulea watoto kimaadili na kuwajengea uwezo wa kufanya maamuzi sahihi hata kama wao hawapo. Kwani imeonekana wengi mwa mabinti ambao hufanya biashara hizi,wanafanya kwa uhuru kwa vile ndugu ama wazazi wao wapo mbali.

Ipo haja ya askari polisi na askari jamii (Sungusungu) kufanya doria mara kwa mara maeneo ambayo yamekuwa yakisadikika kufanyika biashara hizi.Kwani imeonekana siku ambazo doria kali hufanyika.Biashara hizi husimama.Lakini pia askari ambao hupokea 'hongo' kuacha biashara zifanyike ni muhimu wakachukuliwa hatua za kisheria.

Ipo haja kwa serikali ama taasisi za kibenki kutoa mafunzo zaidi ya kijasiliamali, lakini pia kutoa mikopo yenye riba nafuu kwa vijana hasa wa kike ni muhimu wakapewa kipaumbele. Hii itasaidia kupunguza kujiingiza kwenye biashara hizi.

Taasisi za kidini pia zina nafasi kubwa ya kukabiliana na suala hili,kwa kulikemea na kutoa elimu mara kwa mara kwa vijana kupitia semina na mafundisho mbalimbali yanayohusu vijana.
 
Upvote 12

The only

JF-Expert Member
May 19, 2011
5,970
2,000
Ndugu yangu@mkorea
Niposema biashara hii ni tatizo ,Ni kweli ni Tatizo.

wanaofanya wenyewe, ukiwauliza muongoni mwa majibu watakayokupa ni yafuatayo:
(1):Hali duni ya kimaisha ,imenifanya niingie huku.Kwa sababu napata hela ya kodi,Chakula na mambo mengine.
(2).Sipendi watoto wangu waje kuifanya (Kwa wenye watoto).
(3).Nafanya ili nipate mtaji,nikiupata naacha.Sio nzuri ,siwezi Fanya maisha. Yangu yote.

Waweza soma hii pia;


ATHARI KWA MALEZI YA. FAMILIA.
Miongoni mwa wanaojihusisha na biashara hii ,alidai kuwa baadhi yao ni watu wenye watoto wanaotegemea malezi yao,anadai kuwa hufanya jambo hilo kwa siri ili watoto wao wasifahamu.Wengine huwadanganya kuwa wameajiriwa kama wahudumu wa kwenye mahoteli,hii inaweza kupelekea kukosekana kwa malezi ya kutosha kwa watoto jambo linaloweza kupelekea mwendelezo wa kizazi kisichokuwa na maadili.
Point
 

kamwamu

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,806
2,000
Ukibaka 30 jela.Oa tu (Ila usioe kwa mihemko tu ,kama vijana wengi wanavyofanya sikuhizi,Baada ya muda anamuona aliyemuoa wa kawaida tu,anajikuta baadae anarudi kwenye 'tasnia'...Wazuri wapo na kila Siku wanazaliwa,Bahati mbaya wote hawawez kuwa wako!..Kiufupi jenga tabia ya kuridhika).

Kwani ambao hawabaki na ambao hawaendi huko wanafanyeje?

Ukiona kuna kitu unashindwa ,lkn kwenye kitu hicho hicho wapo wengi wanaofanikiwa jitafakari wapi unakwama.
Natumaini utafanikiwa ukianya hivyo
Binadamu tuko tofauti, matamanio yako kwa mwenzio ni machukizo. Kuna walio oa au kuolewa lakini hawaridhiki na wenza, na wengine wanaona hawawezi. Kuna watu hawawezi ishi na mume au mke, usiwahukumu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom