SoC01 Siri iliyopo nyuma ya Biashara ya 'kujiuza' - Athari na hatua za kuchukua

Stories of Change - 2021 Competition

MoseeYM

Senior Member
Jul 19, 2021
134
192
YANAYOENDELEA ZINAKOFANYIKA BIASHARA HIZI
Uchunguzi wangu umebaini kuwa maeneo ambayo biashara hizi zimekuwa zikifanyika hasa ndani ya jiji la Dar es Salaam, wahusika wamekuwa wakitumia bangi na vilevi vikali kwa kile ambacho wamekuwa wakidai hufanya hivyo ili ‘kujitoa ufahamu’ wasione aibu wafanyapo mambo hayo, mathalani maeneo ya Sinza- Africa sana ambapo nyakati za usiku vibanda vingi hufunguliwa ambapo watu hao hujaa. Tunaweza kusema kwa tafsiri rahisi, biashara hii imekuwa ikiambatana na uuzwaji wa bangi na pengine hata aina nyinginezo za madawa ya kulevya suala hili linaweza kuwa chanzo mojawapo cha kuundwa kwa ‘magenge’ mbalimbali ya uhalifu.

Maeneo mengine wanaojihusisha na biashara hizi,wamekuwa wakidai kuporwa wakiwa njiani au wakiwa ndani na wanaowaita ‘wateja’ wao ambao kwa tafsiri nyingine ni ‘vibaka’ ambao huwa wakizunguka zunguka maeneo hayo wakitafuta riziki kwa kupora watu. Baadhi yao Wanadai kupigwa, kupokea vitisho au kunusurika kuuawa na wengine kuuawa wakiwa kwenye maeneo hayo ya ‘kazi’. Wanaouawa kesi zao hushindwa kufika mbali kutokana na ukweli kwamba wanakuwa ni watu ambao hawajulikani na wenyeji wa maeneo hayo, mathalani, mmojawao na wanaojihusisha na biashara hii alidai kuwa kuna ‘mwenzao’ mwenye asili ya kinyarwanda aliuawa maeneo hayo, lakini hakutambulika alipokutwa ameuawa.

JITIHADA ZINAZOFANYIKA, UTHABITI NA UDHAIFU WAKE

Zipo jitihada mbalimbali ambazo zimekuwa zikifanywa na serikali katika kupambana na suala hili kwa sabau sheria za nchi zinatambua kuwa ni biashara haramu. Hivyo mara kadhaa askari huzungukia maeneo yanayosadikika biashara hizi kufanyika na kukamata wahusika.

Uchunguzi umebaini kuwa siku ambazo askari huamua kusaka’’ vijiwe’ vya biashara hii maeneo huwa kimya na biashara huwa haziendelei au hata kama zinakuwa zinaendelea ni kwa kiasi kidogo sana na kwa usiri mkubwa sana. Hivyo, hakuna budi jitihada hizi ambazo huoneshwa na askari polisi kuwa ni mwendelezo wa kila siku kwenye maeneo hayo kwani zinaweza kusaidia kupunguza uhalifu wa aina nyingine ambao unawezekana kuwa ukitendeka maeneo hayo.

Kwa upande mwingine askari ‘sungusungu’ wamekuwa na msaada kwa baadhi ya maeneo ambako shughuli hizi hufanyika kwani huwakamata wahusika na kuwawajibisha kisheria.Japokuwa mbali na jitihada hizo ,uchunguzi wa siri wa mwandishi umebaini kuwa shughuli zimekuwa bado zikiendelea kwenye maeneo hayo kutokana na baadhi ya sungusungu wasio waaminifu kupokea ‘hongo’ ya pesa kutoka kwa wahusika ili kutowabugudhi wakati wakiendelea na biashara zao.Hili limepelekea biashara hii kuonekana kana kwamba ni ‘sugu’ kwa maeneo hayo.

MAGONJWA YA NGONO
Uchunguzi wa siri wa mwandishi kupitia mahojiano na baadhi ya wahusika ,umebaini kuwa wengi wao wanaishi na maambukizi ya virusi vya UKIMWI. Jambo hili linaonekana kuchukuliwa si tatizo kwa wahusika kutokana na kuamini kile wanachokiita ‘matumizi ya kinga’ hivyo kudai haiwezi kuwaathiri wao ,ijapokuwa wataalamu wa afya wanadai kuwa matumizi ya kinga hayatoi uhakika wa asilimia mia moja.kwani pia hutegemea matumizi.sahihi ya kinga.

Taarifa za karibuni kutoka UNAIDS imeonesha kuwa 37% ya wanaojihusisha na biashara za 'kujiuza' katika nchi ambazo hazijahalalisha,wanaishi na maambukizi ya VVU. Hii ni sawa na mmoja kati ya wanne wanaojishughulisha na biashara hizi anaishi na maambukizi ya VVU. Takwimu za maambukizi ya VVU kwa mwaka 2019 nchini zilionesha kuwa kuna maambukizi mapya 58,000. Maambukizi ya magonjwa mengine ya ngono yameonekana kukua hadi kufikia 5%,Huku ripoti ya WHO ikionesha kuwa huchangia kushuka kwa uchumi kwani gharama za matibabu huwa kubwa,lakini pia waathrika wakubwa ni vijana ambao ni tegemeo kwa uchumi wa nchi.

MAGONJWA MENGINE

Homa ya Ini.

Wataalamu wa afya wanadai kuwa kushiriki tendo la ndoa na mpenzi zaidi ya mmoja ni mojawapo wa vyanzo vikuu vya Ugonjwa wa homa ya ini (Hasa kirusi B na C ),ambavyo huchangizwa na jasho au majimaji.Kwa hivyo 'wanaojiuza' na 'wanunuaji' wapo katika hatari kubwa ya kupata ugonjwa huu.ikumbukwe kuwa njia ya kupata ugonjwa huu ni rahisi kuliko hata VVU ,kwani hata jasho huweza kuwa kisababishi.

UVICO-19

Tangu mwishoni mwa mwaka 2019,Dunia imekuwa ikikabiliwa na janga la ugonjwa wa Virusi vya Corona.Hapana shaka,kuwa wanaojihusisha na biashara za 'kujiuza' wapo katika hatari kubwa ya kupata maambukizi,kutokana na biashara ambayo huifanya huhusisha moja kwa moja migusano na 'wateja wao.Mbali na kuwepo na ugonjwa huu mpya ,bado biashara hizi zimekuwa zikifanyika,huku wahusika wakionekana kupuuzia'.Hakuna takwimu zinazoonesha kundi hili limeathiriwaje na ugonjwa huu,lakini haitii shaka kuwa kundi hili ni miongoni mwa makundi yaliyo katika hatari zaidi ya kupata na kuusambaza ugonjwa huu ,endapo biashara hizi zitaendelea

MTAZAMO WA KIMAADILI
Katika jamii yetu ya Tanzania ,suala la mabinti ama wanawake ' kujiuza' halikubaliki kwani ni kinyume na maadili.Suala la kuoa au kuolewa huonekana kuwa ni jambo la kheri na ustaarabu, kwani huonesha watu hao wamehalalishwa na hakuna mahusiano mengine yanayoruhusiwa nje ya mpango wa ndoa, kufanya hivyo huonekana ni kosa. Tafsiri rahisi ni kwamba, kuoa au kuolewa ni mojawapo ya njia ya kuondoa hali ya kuwa na mahusiano mengi ya 'kingono' (Ukiachana na sababu nyinginezo za lengo la ndoa).Viapo vya ndoa za kidini pia huashiria kukataza mahusiao ya kimapenzi nje ya ndoa

NINI KIFANYIKE?
Jamii ya maeneo ambako biashara hizi hufanyika.Ina nafasi kubwa sana ya kuzuia kufanyika kwa biashara hizi,kwani kuna athari kubwa kwao kuacha ikiendelea kufanyika.Watoto wadogo wakiendelea kuliona likifanyika kuna hatari ya kutengeneza kizazi kisicho na maadili cha baadae.

Ni muhimu wazazi na walezi kushirikiana kulea watoto kimaadili na kuwajengea uwezo wa kufanya maamuzi sahihi hata kama wao hawapo. Kwani imeonekana wengi mwa mabinti ambao hufanya biashara hizi,wanafanya kwa uhuru kwa vile ndugu ama wazazi wao wapo mbali.

Ipo haja ya askari polisi na askari jamii (Sungusungu) kufanya doria mara kwa mara maeneo ambayo yamekuwa yakisadikika kufanyika biashara hizi.Kwani imeonekana siku ambazo doria kali hufanyika.Biashara hizi husimama.Lakini pia askari ambao hupokea 'hongo' kuacha biashara zifanyike ni muhimu wakachukuliwa hatua za kisheria.

Ipo haja kwa serikali ama taasisi za kibenki kutoa mafunzo zaidi ya kijasiliamali, lakini pia kutoa mikopo yenye riba nafuu kwa vijana hasa wa kike ni muhimu wakapewa kipaumbele. Hii itasaidia kupunguza kujiingiza kwenye biashara hizi.

Taasisi za kidini pia zina nafasi kubwa ya kukabiliana na suala hili,kwa kulikemea na kutoa elimu mara kwa mara kwa vijana kupitia semina na mafundisho mbalimbali yanayohusu vijana.
 
SERIKALI
tumeishauri tumeshindwa itujengee kasino ipate kodi eti wapimwe haitaki

Umelewa na umenyoa vuzi nawembe zooote para parakweli kondom hua hazifiki kwenye kingo

Ili ukimwi uishe inatakiwa kilamtanzania awe tajiri
Ni sehemu ipi UKIMWi uliisha kwa sababu ni matajiri?.

Kwani kipindi UKIMWI haupo Tanzania,tulikuwa Matajiri?
 
Ni sehemu ipi UKIMWi uliisha kwa sababu ni matajiri?.

Kwani kipindi UKIMWI haupo Tanzania,tulikuwa Matajiri?
ukiwa tajiri na shule haitakosekana nilimanisha
Maskini muda wote tu nawaza kuchengana tu yaani via vyetu vya uzazi vimekua faraja yaumasikini wetu, haaaaa
 
ukiwa tajiri na shule haitakosekana nilimanisha
Maskini muda wote tu nawaza kuchengana tu yaani via vyetu vya uzazi vimekua faraja yaumasikini wetu, haaaaa
'Tajiri na Mali zake,masikini na watoto zake'.
Nimekuelewa vizuri Mkuu!.

Nchi ina utajiri wa rasilimali ,lkn watu wake masikini.
Nadhani nguvu kubwa inabidi iwekezwe kwenye mapinduzi ya mfumo wetu wa kielimu.

Si tu kwamba tukiwa matajiri tutakuwa na Elimu.Bali Elimu kuwa msaada

Kwa sababu mfano 'Dada zetu' tunaowaita 'wasomi' nao utawakuta kwenye vijiwe 'wakijiuza' sina shaka ukiwauliza watadai ajira hamna.Si ajabu wazazi wake ni wakulima au wafugaji wenye maeneo makubwa,ambayo angeweza Fanya kitu.kujikomboa na 'utumwa wa kingono'.
 
Msisitizo wangu ni kwamba bado tunayo nafasi kwa watoto wetu
 
'Tajiri na Mali zake,masikini na watoto zake'.
Nimekuelewa vizuri Mkuu!.

Nchi ina utajiri wa rasilimali ,lkn watu wake masikini.
Nadhani nguvu kubwa inabidi iwekezwe kwenye mapinduzi ya mfumo wetu wa kielimu.

Si tu kwamba tukiwa matajiri tutakuwa na Elimu.Bali Elimu kuwa msaada

Kwa sababu mfano 'Dada zetu' tunaowaita 'wasomi' nao utawakuta kwenye vijiwe 'wakijiuza' sina shaka ukiwauliza watadai ajira hamna.Si ajabu wazazi wake ni wakulima au wafugaji wenye maeneo makubwa,ambayo angeweza Fanya kitu.kujikomboa na 'utumwa wa kingono'.
Mapinduzi ya elimu Tanzania yanahtaji tilion moja tu, kufumua mtaala na kila kitu nakutoa huduma bora ya elimu kuazia msingi hadi vyuoni

KWAKUA
CCM NASERIKALI wanaitambua silaha iliyobakia kuwa ondoa madarakani nihyo inafikia hatua wanabumba kila kitu.

Katiba wataiita chokochoko
Katiba kabisa kabisa mtu anasimama pahala anaiita chokochoko kweli Ccm choko chokozoa choko
 
Kiufupi hii biashara sio ya 'kuishadadia' kama wengi wanavyofanya kwenye thread zinazohusu haya mambo humu JF.
Tunaweza furahi kwa kitambo.Inaweza fika siku ikawa 'nyuma geuka' haya mambo yakahamia kwenye familia zetu.Unamkuta 'mkeo' au 'mwanao' yupo na kijeba kwenye madanguro.
Si ajabu
'Washadadiaji' wa haya mambo ,wakiwakuta wakezao au mabinti zao huko.Nyumbani hakutokalika.
 
Usitake easy hivyo bro!.
Binadamu tumeumbiwa aibu
Mke wangu nikimkuta huko kuna mawili;
i. Mi najua kwamba anaifanya kazi hiyo (hapa hakutokuwa na tatizo kati yetu)
ii. Kama anaifanya Kwa umalaya wake au nye ge zake (basi uhusiano wetu utakuwa umefika tamati)

Mwanangu nikimkuta hapo kwenye danguro
i. Je? Bado yuko chini ya uangalizi wangu au anajitegemea.( vyovyote vile Kwa hapa nitamwambia aendelee na kazi yake ila anitafute ili tuyazungumze)
ii. Kama Ana miaka chini ya 18 (nitamwambia nimemfuata ili twende nyumbani)

Mkuu wale wauzaji ni watu Kama sisi wana ndugu na familia zao. Wapo ambao waume/mabwana zao na baadhi ya ndg zao wanajua kila kitu kuhusu wao
Nalog off
 
Kwa Ninachokifahamu

~Ni ngumu mwanaume kuoa mwanamke anayejua 'anajiuza' Labda 'mchepuko'(Hidden + bitter Truth)

~Wanaume wazoefu wa 'kununua' akikukuta na mkeo au Binti yake wa under 18 anaweza kukuua (Sad truth).

~Ni rahisi ndoa kuendelea mwanaume akifumwa na 'mchepuko' au 'muuzaji' kuliko mwanamke asiyemuuzaji kufumaniwa na mwanaume 'mnunuaji mzoefu'. (Bitter+Hidden truth again).

~Nakubaliana na wewe Ni kweli kuwa wapo wanaofanya 'hizi shughuli' lakini wanafahamika na baadhi ya ndugu zao INGAWAJE wengi wao hawajulikani ila 'wanahisiwa' kutokana na may be their 'lifestyle'.Ndio maana wanazifanya hizo shughuli mbali kabisa na makazi wanayoishi.Kwa lengo la kutojulikana (Kachunguze ukweli kuhusu hilo,utajua)

~Ni kweli 'wauzaji' ni watu kama watu wengine ndio maana wanahitaji msaada wa jamii.Kwani sio wote walioingia 'huko' wanapenda.Wapo walioingia huko wakihisi ni njia ya kujikwamua kiuchumi.Matokeo yake wamekuwa na 'Uraibu' wameshindwa kutoka ilihali hawaipendi hiyo shughuli.(KACHUNGUZE),huko wapo 'walioachwa' na waume zao wamejikuta ili kulea familia wako huko.Huko wapo waliozalishwa na watu waliokataa kulea watoto wao,Huko wapo waliotengwa na familia au ndugu,Huko wapo walioletwa mjini kutoka vijijini kutokana na kuahidiwa kazi zenye maslahi mazuri,mwishowe 'wametupwa'.Huko wapo waliokuja mjini kutafuta maisha wakiishi na rafiki zao mwishowe kutokana na hao rafiki zao kuwa 'wanajishugjulisha' na hizi biashara,wakajikuta wameingia kwa nguvu ya ushawishi wao.Huko wapo wanawake walio kwenye ndoa ambao yamkini walikosa malezi mazuri kutoka kwa wazazi/walezi.

NAWASILISHA
 
Mi ni mnunuaji mzuri wa wauza ngozi. Wapo waume wanajua kuwa wake zao ni wauzaji na wanaishi hivyo. Vile vibanda vyá wahaya baadhi yao kuna wanaume wanaishi mule. Dunia ina siri nyingi za kushangaza
Nalog off
 
Hahahaha.

Sema dunia ina mambo Mengi ya kushangaza.Maana kama hata wewe umejua ina 'siri' basi hamna siri hapo.

Ila naomba kuuliza kwa wanaJF wengine,hivi hao wanaume 'wanaosemekana' wanawaoa 'wanatasnia' wakijua kuwa hata baada ya hapo wataendelea na 'tasnia' ni kweli wanawaoa kwa ndoa rasmi ? Au ni ile kwa kuwaweka watoto wa watu ndani tu?.

Naomba kujuzwa ukweli kuhusu hayo madai
 
Back
Top Bottom