SoC01 Siri iliyopo nyuma ya Biashara ya 'kujiuza' - Athari na hatua za kuchukua

Stories of Change - 2021 Competition

MoseeYM

Senior Member
Jul 19, 2021
134
192
YANAYOENDELEA ZINAKOFANYIKA BIASHARA HIZI
Uchunguzi wangu umebaini kuwa maeneo ambayo biashara hizi zimekuwa zikifanyika hasa ndani ya jiji la Dar es Salaam, wahusika wamekuwa wakitumia bangi na vilevi vikali kwa kile ambacho wamekuwa wakidai hufanya hivyo ili ‘kujitoa ufahamu’ wasione aibu wafanyapo mambo hayo, mathalani maeneo ya Sinza- Africa sana ambapo nyakati za usiku vibanda vingi hufunguliwa ambapo watu hao hujaa. Tunaweza kusema kwa tafsiri rahisi, biashara hii imekuwa ikiambatana na uuzwaji wa bangi na pengine hata aina nyinginezo za madawa ya kulevya suala hili linaweza kuwa chanzo mojawapo cha kuundwa kwa ‘magenge’ mbalimbali ya uhalifu.

Maeneo mengine wanaojihusisha na biashara hizi,wamekuwa wakidai kuporwa wakiwa njiani au wakiwa ndani na wanaowaita ‘wateja’ wao ambao kwa tafsiri nyingine ni ‘vibaka’ ambao huwa wakizunguka zunguka maeneo hayo wakitafuta riziki kwa kupora watu. Baadhi yao Wanadai kupigwa, kupokea vitisho au kunusurika kuuawa na wengine kuuawa wakiwa kwenye maeneo hayo ya ‘kazi’. Wanaouawa kesi zao hushindwa kufika mbali kutokana na ukweli kwamba wanakuwa ni watu ambao hawajulikani na wenyeji wa maeneo hayo, mathalani, mmojawao na wanaojihusisha na biashara hii alidai kuwa kuna ‘mwenzao’ mwenye asili ya kinyarwanda aliuawa maeneo hayo, lakini hakutambulika alipokutwa ameuawa.

JITIHADA ZINAZOFANYIKA, UTHABITI NA UDHAIFU WAKE

Zipo jitihada mbalimbali ambazo zimekuwa zikifanywa na serikali katika kupambana na suala hili kwa sabau sheria za nchi zinatambua kuwa ni biashara haramu. Hivyo mara kadhaa askari huzungukia maeneo yanayosadikika biashara hizi kufanyika na kukamata wahusika.

Uchunguzi umebaini kuwa siku ambazo askari huamua kusaka’’ vijiwe’ vya biashara hii maeneo huwa kimya na biashara huwa haziendelei au hata kama zinakuwa zinaendelea ni kwa kiasi kidogo sana na kwa usiri mkubwa sana. Hivyo, hakuna budi jitihada hizi ambazo huoneshwa na askari polisi kuwa ni mwendelezo wa kila siku kwenye maeneo hayo kwani zinaweza kusaidia kupunguza uhalifu wa aina nyingine ambao unawezekana kuwa ukitendeka maeneo hayo.

Kwa upande mwingine askari ‘sungusungu’ wamekuwa na msaada kwa baadhi ya maeneo ambako shughuli hizi hufanyika kwani huwakamata wahusika na kuwawajibisha kisheria.Japokuwa mbali na jitihada hizo ,uchunguzi wa siri wa mwandishi umebaini kuwa shughuli zimekuwa bado zikiendelea kwenye maeneo hayo kutokana na baadhi ya sungusungu wasio waaminifu kupokea ‘hongo’ ya pesa kutoka kwa wahusika ili kutowabugudhi wakati wakiendelea na biashara zao.Hili limepelekea biashara hii kuonekana kana kwamba ni ‘sugu’ kwa maeneo hayo.

MAGONJWA YA NGONO
Uchunguzi wa siri wa mwandishi kupitia mahojiano na baadhi ya wahusika ,umebaini kuwa wengi wao wanaishi na maambukizi ya virusi vya UKIMWI. Jambo hili linaonekana kuchukuliwa si tatizo kwa wahusika kutokana na kuamini kile wanachokiita ‘matumizi ya kinga’ hivyo kudai haiwezi kuwaathiri wao ,ijapokuwa wataalamu wa afya wanadai kuwa matumizi ya kinga hayatoi uhakika wa asilimia mia moja.kwani pia hutegemea matumizi.sahihi ya kinga.

Taarifa za karibuni kutoka UNAIDS imeonesha kuwa 37% ya wanaojihusisha na biashara za 'kujiuza' katika nchi ambazo hazijahalalisha,wanaishi na maambukizi ya VVU. Hii ni sawa na mmoja kati ya wanne wanaojishughulisha na biashara hizi anaishi na maambukizi ya VVU. Takwimu za maambukizi ya VVU kwa mwaka 2019 nchini zilionesha kuwa kuna maambukizi mapya 58,000. Maambukizi ya magonjwa mengine ya ngono yameonekana kukua hadi kufikia 5%,Huku ripoti ya WHO ikionesha kuwa huchangia kushuka kwa uchumi kwani gharama za matibabu huwa kubwa,lakini pia waathrika wakubwa ni vijana ambao ni tegemeo kwa uchumi wa nchi.

MAGONJWA MENGINE

Homa ya Ini.

Wataalamu wa afya wanadai kuwa kushiriki tendo la ndoa na mpenzi zaidi ya mmoja ni mojawapo wa vyanzo vikuu vya Ugonjwa wa homa ya ini (Hasa kirusi B na C ),ambavyo huchangizwa na jasho au majimaji.Kwa hivyo 'wanaojiuza' na 'wanunuaji' wapo katika hatari kubwa ya kupata ugonjwa huu.ikumbukwe kuwa njia ya kupata ugonjwa huu ni rahisi kuliko hata VVU ,kwani hata jasho huweza kuwa kisababishi.

UVICO-19

Tangu mwishoni mwa mwaka 2019,Dunia imekuwa ikikabiliwa na janga la ugonjwa wa Virusi vya Corona.Hapana shaka,kuwa wanaojihusisha na biashara za 'kujiuza' wapo katika hatari kubwa ya kupata maambukizi,kutokana na biashara ambayo huifanya huhusisha moja kwa moja migusano na 'wateja wao.Mbali na kuwepo na ugonjwa huu mpya ,bado biashara hizi zimekuwa zikifanyika,huku wahusika wakionekana kupuuzia'.Hakuna takwimu zinazoonesha kundi hili limeathiriwaje na ugonjwa huu,lakini haitii shaka kuwa kundi hili ni miongoni mwa makundi yaliyo katika hatari zaidi ya kupata na kuusambaza ugonjwa huu ,endapo biashara hizi zitaendelea

MTAZAMO WA KIMAADILI
Katika jamii yetu ya Tanzania ,suala la mabinti ama wanawake ' kujiuza' halikubaliki kwani ni kinyume na maadili.Suala la kuoa au kuolewa huonekana kuwa ni jambo la kheri na ustaarabu, kwani huonesha watu hao wamehalalishwa na hakuna mahusiano mengine yanayoruhusiwa nje ya mpango wa ndoa, kufanya hivyo huonekana ni kosa. Tafsiri rahisi ni kwamba, kuoa au kuolewa ni mojawapo ya njia ya kuondoa hali ya kuwa na mahusiano mengi ya 'kingono' (Ukiachana na sababu nyinginezo za lengo la ndoa).Viapo vya ndoa za kidini pia huashiria kukataza mahusiao ya kimapenzi nje ya ndoa

NINI KIFANYIKE?
Jamii ya maeneo ambako biashara hizi hufanyika.Ina nafasi kubwa sana ya kuzuia kufanyika kwa biashara hizi,kwani kuna athari kubwa kwao kuacha ikiendelea kufanyika.Watoto wadogo wakiendelea kuliona likifanyika kuna hatari ya kutengeneza kizazi kisicho na maadili cha baadae.

Ni muhimu wazazi na walezi kushirikiana kulea watoto kimaadili na kuwajengea uwezo wa kufanya maamuzi sahihi hata kama wao hawapo. Kwani imeonekana wengi mwa mabinti ambao hufanya biashara hizi,wanafanya kwa uhuru kwa vile ndugu ama wazazi wao wapo mbali.

Ipo haja ya askari polisi na askari jamii (Sungusungu) kufanya doria mara kwa mara maeneo ambayo yamekuwa yakisadikika kufanyika biashara hizi.Kwani imeonekana siku ambazo doria kali hufanyika.Biashara hizi husimama.Lakini pia askari ambao hupokea 'hongo' kuacha biashara zifanyike ni muhimu wakachukuliwa hatua za kisheria.

Ipo haja kwa serikali ama taasisi za kibenki kutoa mafunzo zaidi ya kijasiliamali, lakini pia kutoa mikopo yenye riba nafuu kwa vijana hasa wa kike ni muhimu wakapewa kipaumbele. Hii itasaidia kupunguza kujiingiza kwenye biashara hizi.

Taasisi za kidini pia zina nafasi kubwa ya kukabiliana na suala hili,kwa kulikemea na kutoa elimu mara kwa mara kwa vijana kupitia semina na mafundisho mbalimbali yanayohusu vijana.
 
1626928260027.png
 
Kitendo cha kugusa hii biashara, umekosa kura yangu
Mkuu Mkorea. Waweza soma hii pia,ili kufahamu zaidi.

HALI ILIVYO KWA NCHI ZILIZOHALALISHA

Ziko nchi zilizoamua kuhalalisha na kuwasajili wanaojihusisha na biashara hizi na kutengeneza mfumo wa kukusanya mapato,mategemeo yalikuwa makubwa ingawaje bado limezidi kuwa tatizo.

Mathalani,nchi ya Uholanzi iliamua kuhalalisha miaka takribani ishirini iliyopita,Utafiti uliofanywa unaonesha kuwa kulikuwa na wanawake na mabinti 31,000 lakini ni 5% ambao ni sawa na 1550 tu waliojisajili kwenye mfumo ili watambulike na kuhalalishwa,hii ni kwa sababu wengi wao hawakutaka kujulikana kwani ni jambo linaloonekana kutokuwa la kimaadili hivyo pamoja na kulihalalisha Lakini jamii ya wengi hailioni kuwa la halali

Nchi ya Senegal ni nchi ya Afrika iliyoamua kuhalalisha biashara hii tangu mwaka 1966 kwa kuwekea sera ya afya ambayo inawataka wahusika kuhudhuria kila mwezi hospitali kuangalia afya zao,Na baada ya vipimo hupewa kadi zenye kuonesha majibu kama wameathirika ama la.Lengo likiwa walioathirika kutokuwa na uhalali wa kufanya shughuli hiyo kwani kutapelekea kuenea kwa magonjwa ya ngono.

Lakini imekuja kuonekana kwamba hakujasaidia kuondoa tatizo la kuenea kwa magonjwa , kama lilivyo lengo la kuanzisha mfumo huu kwani majibu ya vipimo huchukua muda ,katika muda huo wahusika huwa wakiendelea na biashara zao,jambo hili linaleta shaka kwani endapo mhusika atagundulika kuwa na magonjwa ya ngono kuna uwezekano wa kuwa amewaambukiza wengine kipindi cha kusubiri majibu.

Lakini pia bado limeonekana kuwa jambo linalopingwa na jamii za kiafrika kwa mtazamo wa kimaadil.
 
Kitendo cha kugusa hii biashara, umekosa kura yangu
Ndugu yangu@mkorea
Niposema biashara hii ni tatizo ,Ni kweli ni Tatizo.

wanaofanya wenyewe, ukiwauliza muongoni mwa majibu watakayokupa ni yafuatayo:
(1):Hali duni ya kimaisha ,imenifanya niingie huku.Kwa sababu napata hela ya kodi,Chakula na mambo mengine.
(2).Sipendi watoto wangu waje kuifanya (Kwa wenye watoto).
(3).Nafanya ili nipate mtaji,nikiupata naacha.Sio nzuri ,siwezi Fanya maisha. Yangu yote.

Waweza soma hii pia;

ATHARI KWA MALEZI YA. FAMILIA.
Miongoni mwa wanaojihusisha na biashara hii ,alidai kuwa baadhi yao ni watu wenye watoto wanaotegemea malezi yao,anadai kuwa hufanya jambo hilo kwa siri ili watoto wao wasifahamu.Wengine huwadanganya kuwa wameajiriwa kama wahudumu wa kwenye mahoteli,hii inaweza kupelekea kukosekana kwa malezi ya kutosha kwa watoto jambo linaloweza kupelekea mwendelezo wa kizazi kisichokuwa na maadili.
 
Kitendo cha kugusa hii biashara, umekosa kura yangu
Kwa upande mwingine hata wanaume tumekuwa Tatizo.
Tunazalisha 'mabinti' tunawaacha pasipo kutoa malezi ,mwisho wa siku wanaamua kujiingiza huko ili kujikimu kimaisha.

Kwa hivyo! Ni muhimu kwa wanaume kutokimbia majukumu.
 
Hii biashara ipo toka enzi za manabii haitakaa iondoke kamwe
Japokuwa ,zipo jitihada zinazoweza kufanywa kupunguza.

Dunia kila siku inabadilika,Leo hii tuna COVID19,Enzi za manabii haikuwepo.Hatuwezi kusema kwa sababu Tatizo lilikuwepo enzi za manabii basi tuliache.

Ndio maana kama umesoma vizuri,ni kwamba kuna nchi ziliamua kuhalalisha kama njia za kutatua lakini athari zimeendelea kuwepo.

Walau tukianza na kupunguza hii ya barabarani tutakuwa tumepiga hatua.Kwa sababu watoto wadogo wanajifunza nini?.Lakini pia itapunguza ushawishi kwa mfano: kuna njia unaweza kuwa unakatiza saa moja jion au saa mbili unakuta wamekaa barabarani kila anayepita utasikia 'Baby njoo'.Kwa mpita njia ambaye sio mwenyeji na hajui wanafanya nini anaweza kuamua kwenda ,akashawishiwa mwisho wa siku inakuwa "mwendelezo". Msisitizo wangu ni kwamba tunaweza kuanza na hata hii ya Barabarani.

Lakini pia inawezekana inaonekana 'sugu' kutokana na njia zinazochukuliwa kutatua Sio thabiti.

Sungusungu na askari polisi wamekuwa msaada maeneo inakofanyika hadharani.kwa nini jitihada hizi zisiendelezwe?.Udhaifu wao ni kuwa hawafanyi hivyo mara kwa mara,na baadhi yao " hupokea hongo".
 
YANAYOENDELEA ZINAKOFANYIKA BIASHARA HIZI
Uchunguzi wangu umebaini kuwa maeneo ambayo biashara hizi zimekuwa zikifanyika hasa ndani ya jiji la Dar es Salaam, wahusika wamekuwa wakitumia bangi na vilevi vikali kwa kile ambacho wamekuwa wakidai hufanya hivyo ili ‘kujitoa ufahamu’ wasione aibu wafanyapo mambo hayo, mathalani maeneo ya Sinza- Africasana ambapo nyakati za usiku vibanda vingi hufunguliwa ambapo watu hao hujaa. Tunaweza kusema kwa tafsiri rahisi, biashara hii imekuwa ikiambatana na uuzwaji wa bangi na pengine hata aina nyinginezo za madawa ya kulevya suala hili linaweza kuwa chanzo mojawapo cha kuundwa kwa ‘magenge’ mbalimbali ya uhalifu.

Maeneo mengine wanaojihusisha na biashara hizi,wamekuwa wakidai kuporwa wakiwa njiani au wakiwa ndani na wanaowaita ‘wateja’ wao ambao kwa tafsiri nyingine ni ‘vibaka’ ambao huwa wakizunguka zunguka maeneo hayo wakitafuta riziki kwa kupora watu. Baadhi yao Wanadai kupigwa, kupokea vitisho au kunusurika kuuawa na wengine kuuawa wakiwa kwenye maeneo hayo ya ‘kazi’. Wanaouawa kesi zao hushindwa kufika mbali kutokana na ukweli kwamba wanakuwa ni watu ambao hawajulikani na wenyeji wa maeneo hayo, mathalani, mmojawao na wanaojihusisha na biashara hii alidai kuwa kuna ‘mwenzao’ mwenye asili ya kinyarwanda aliuawa maeneo hayo, lakini hakutambulika alipokutwa ameuawa.

JITIHADA ZINAZOFANYIKA, UTHABITI NA UDHAIFU WAKE

Zipo jitihada mbalimbali ambazo zimekuwa zikifanywa na serikali katika kupambana na suala hili kwa sabau sheria za nchi zinatambua kuwa ni biashara haramu. Hivyo mara kadhaa askari huzungukia maeneo yanayosadikika biashara hizi kufanyika na kukamata wahusika.

Uchunguzi umebaini kuwa siku ambazo askari huamua kusaka’’ vijiwe’ vya biashara hii maeneo huwa kimya na biashara huwa haziendelei au hata kama zinakuwa zinaendelea ni kwa kiasi kidogo sana na kwa usiri mkubwa sana. Hivyo, hakuna budi jitihada hizi ambazo huoneshwa na askari polisi kuwa ni mwendelezo wa kila siku kwenye maeneo hayo kwani zinaweza kusaidia kupunguza uhalifu wa aina nyingine ambao unawezekana kuwa ukitendeka maeneo hayo.

Kwa upande mwingine askari ‘sungusungu’ wamekuwa na msaada kwa baadhi ya maeneo ambako shughuli hizi hufanyika kwani huwakamata wahusika na kuwawajibisha kisheria.Japokuwa mbali na jitihada hizo ,uchunguzi wa siri wa mwandishi umebaini kuwa shughuli zimekuwa bado zikiendelea kwenye maeneo hayo kutokana na baadhi ya sungusungu wasio waaminifu kupokea ‘hongo’ ya pesa kutoka kwa wahusika ili kutowabugudhi wakati wakiendelea na biashara zao.Hili limepelekea biashara hii kuonekana kana kwamba ni ‘sugu’ kwa maeneo hayo.

MAGONJWA YA NGONO
Uchunguzi wa siri wa mwandishi kupitia mahojiano na baadhi ya wahusika ,umebaini kuwa wengi wao wanaishi na maambukizi ya virusi vya UKIMWI. Jambo hili linaonekana kuchukuliwa si tatizo kwa wahusika kutokana na kuamini kile wanachokiita ‘matumizi ya kinga’ hivyo kudai haiwezi kuwaathiri wao ,ijapokuwa wataalamu wa afya wanadai kuwa matumizi ya kinga hayatoi uhakika wa asilimia mia moja.kwani pia hutegemea matumizi.sahihi ya kinga.

Taarifa za karibuni kutoka UNAIDS imeonesha kuwa 37% ya wanaojihusisha na biashara za 'kujiuza' katika nchi ambazo hazijahalalisha,wanaishi na maambukizi ya VVU. Hii ni sawa na mmoja kati ya wanne wanaojishughulisha na biashara hizi anaishi na maambukizi ya VVU. Takwimu za maambukizi ya VVU kwa mwaka 2019 nchini zilionesha kuwa kuna maambukizi mapya 58,000. Maambukizi ya magonjwa mengine ya ngono yameonekana kukua hadi kufikia 5%,Huku ripoti ya WHO ikionesha kuwa huchangia kushuka kwa uchumi kwani gharama za matibabu huwa kubwa,lakini pia waathrika wakubwa ni vijana ambao ni tegemeo kwa uchumi wa nchi.

MAGONJWA MENGINE
Tangu mwishoni mwa mwaka 2019,Jamii imekuwa ikikabiliwa na ugonjwa wa Virusi vya Corona.Hapana shaka,kuwa wanaojihusisha na biashara za 'kujiuza' wapo katika hatari kubwa ya kupata maambukizi,kutokana na biashara ambayo huifanya huhusisha moja kwa moja migusano na 'wateja wao.Mbali na kuwepo na ugonjwa huu mpya ,bado biashara hizi zimekuwa zikifanyika,huku wahusika wakionekana kupuuzia'.Hakuna takwimu zinazoonesha kundi hili limeathiriwaje na ugonjwa huu,lakini haitii shaka kuwa kundi hili ni miongoni mwa makundi yaliyo katika hatari zaidi ya kupata na kuusambaza ugonjwa huu ,endapo biashara hizi zitaendelea

MTAZAMO WA KIMAADILI
Katika jamii yetu ya Tanzania ,suala la mabinti ama wanawake ' kujiuza' halikubaliki kwani ni kinyume na maadili.Suala la kuoa au kuolewa huonekana kuwa ni jambo la kheri na ustaarabu, kwani huonesha watu hao wamehalalishwa na hakuna mahusiano mengine yanayoruhusiwa nje ya mpango wa ndoa, kufanya hivyo huonekana ni kosa. Tafsiri rahisi ni kwamba, kuoa au kuolewa ni mojawapo ya njia ya kuondoa hali ya kuwa na mahusiano mengi ya 'kingono' (Ukiachana na sababu nyinginezo za lengo la ndoa).Viapo vya ndoa za kidini pia huashiria kukataza mahusiao ya kimapenzi nje ya ndoa

NINI KIFANYIKE?
Jamii ya maeneo ambako biashara hizi hufanyika.Ina nafasi kubwa sana ya kuzuia kufanyika kwa biashara hizi,kwani kuna athari kubwa kwao kuacha ikiendelea kufanyika.Watoto wadogo wakiendelea kuliona likifanyika kuna hatari ya kutengeneza kizazi kisicho na maadili cha baadae.

Ni muhimu wazazi na walezi kushirikiana kulea watoto kimaadili na kuwajengea uwezo wa kufanya maamuzi sahihi hata kama wao hawapo. Kwani imeonekana wengi mwa mabinti ambao hufanya biashara hizi,wanafanya kwa uhuru kwa vile ndugu ama wazazi wao wapo mbali.

Ipo haja ya askari polisi na askari jamii (Sungusungu) kufanya doria mara kwa mara maeneo ambayo yamekuwa yakisadikika kufanyika biashara hizi.Kwani imeonekana siku ambazo doria kali hufanyika.Biashara hizi husimama.Lakini pia askari ambao hupokea 'hongo' kuacha biashara zifanyike ni muhimu wakachukuliwa hatua za kisheria.

Ipo haja kwa serikali ama taasisi za kibenki kutoa mafunzo zaidi ya kijasiliamali kwa vijana, lakini pia kutoa mikopo yenye riba nafuu kwa vijana hasa wa kike ni muhimu wakapewa kipaumbele. Hii itasaidia kupunguza kujiingiza kwenye biashara hizi.

Taasisi za kidini pia zina nafasi kubwa ya kukabiliana na suala hili,kwa kulikemea na kutoa elimu mara kwa mara kwa vijana ili kuwasaidia vijana kufanya kazi za halali kujiingizia kipato

NAWASILISHA!
 
Kama kuna swali ,jingine lolote kuhusu maada
Uliza utajibiwa.
 
Biashara Kongwe hii hutoiweza.

Manabii na mitume wote wameikuta na wameiacha.

Yes mwenyewe anategemea akirudi ataikuta.
Unaposema hivyo lazima utambue kuwa Watafiti wanadai ipo kwa madaraja.

Kuna ambao husimama barabarani usiku (Walengwa wakuu wa maada).

Kuna ambao hukaa ndani ya maeneo ya starehe.

Kuna ambao,hutumia mitandao kupata wateja (Hawa hawana sehemu maalum,ni ngumu kuwatambua).

Lakini kundi La walengwa wakuu wa maada linaweza kuwa sio gumu kulitokomeza ,endapo jitihada za dhati zitachukuliwa.Kwa sababu Hata wao huona aibu,ndio maana hujificha gizani.lkn pia wanajua wanachokifanya sio sahihi ndio maana Hata askari wakija hukimbia. Tofauti na hilo kundi LA wa mtandaoni.hao ndio ngumu kuwatokomeza
 
Back
Top Bottom