Siri iliyojificha kwenye nazi, muhogo na karanga mbichi

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,254
2,000
Umewahi kukaa kwenye foleni? Kama jibu ni ndiyo, je, umewahi kuwaona kina mama wanaouza nazi, muhogo na karanga mbichi katika mabeseni?

Kama jibu pia ni ndiyo, basi ukae ukijua kuwa bidhaa hizo sasa ndiyo habari ya mjini kwani muhogo, karanga mbichi na nazi vinatajwa kuwa vyakula vya kuongeza urijali na kulinda heshima ya baba nyumbani.

Ni kawaida siku hizi kuwaona kina mama wakiwa wamebeba mabeseni yaliyojaa, muhogo, nazi na karanga. Muhogo huwa umesafishwa vizuri huku gamba la juu likiachwa, lakini likikwaruzwa na kusafishwa hadi kuwa jeupe.
Karanga hufungwa kwenye vifuko vya plastiki na nazi (mbata) hukatwa vipande vidogo vidogo na kufungwa katika vifuko pia.

Muuzaji aghalabu hutembea na kisu chake kwa ajili ya kukata muhogo kwa sababu, kuna kipande cha Sh100, 200 hadi cha 500. Karanga mbichi huuzwa Sh200 kwa pakiti na nazi ni Sh100 kwa pakiti.
Wauzaji hawa ambao wengi wao ni wanawake, hutega wateja wao katika foleni za magari ambako madereva wa daladala na wanaume wengine wengi walio kwenye magari hununua kwa wingi bidhaa hizo.

Kadhalika, wanaume wenye biashara zao katika masoko makubwa kama Kariakoo, Tandika au Buguruni nao huichangamkia mihogo, karanga na nazi.
Lakini, swali ni kwa nini bidhaa hizi huuzwa kwa pamoja na kwa nini zinapendwa zaidi na wanaume?

Mwandishi wetu aliwatafuta wauzaji hao, ambao walikuwa wametingwa kuuza bidhaa zao katikati ya magari yaliyo kwenye foleni yakielekea Buguruni.
Akiwa amebeba beseni lake lililosheheni bidhaa hizo kichwani, Magdalena Mwombeki, alisema anauza karanga mbichi na mihogo kwa sababu ni vitu ambavyo wanaume wamekuwa wakivikimbilia kwa wingi.

“Zamani nilikuwa nauza matunda na muhogo mibichi, lakini wateja wakawa wanaulizia na karanga na nazi, nikaamua kuanza kuuza hivyo tu na kwa kweli vina wateja,” alisema.
Alisema baada ya kuanza kuuza kwa wingi aligundua wanaume wanapenda zaidi bidhaa hizo kwa sababu zinaongeza hamu na nguvu ya tendo la ndoa, “Wanaponiita wakitaka kununua, wanasema hebu tuletee karanga hizo tuongeze heshima ya ndoa.”

Alisema baadaye wateja wake wengi wakawa wanaulizia nazi na ndipo akaanza kuziuza lakini alisema anaikata vipande vidogo vidogo na kuvifunga katika mifuko ya plastiki.
Muuzaji mwingine, Shyrose Kamunguye alisema sasa hivi wanawake wengi wameacha kuuza matunda na wamekimbilia kuuza karanga mbichi, muhogo na nazi kutokana na wanunuzi wa bidhaa hizo kuwa wengi.

“Hata nikijaza matango na maembe kwenye beseni bado wateja wanaulizia muhogo mbichi na karanga na hawa wa nazi nao wanakuja kwa kasi sasa,” alisema.
Mtaalamu wa chakula na lishe katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Pazi Mwinyimvua alisema manufaa ya muhogo, nazi na karanga yameibuliwa na ujuzi wa asili.

“Binadamu mwenyewe amekula vitu hivi na akaona faida zake ndiyo maana unaona vinahitajika kwa wingi na wanaume. Ni ajabu kuona wengine wanakanusha kuwa vyakula hivi vinaongeza nguvu wakati hata sayansi inaonyesha hivyo,” alisema.

Alisema kwa mfano karanga, ina wingi wa protini na inazalisha seli nyingi kwa hali ya kawaida anayekula lazima atazalisha pia manii kwa wingi. “Kwa upande wa muhogo huu una wanga na nishati kubwa kwa hiyo ukila unakusaidia kukupa nguvu na joto na mtu ambaye hajala na hana nishati, hawezi kuwa imara katika tendo la ndoa,” alisema.

Mwinyimvua alisema nazi nayo ni muhimu zaidi kwa sababu ina protini na mafuta na yote kwa pamoja husaidia kuufanya mzunguko wa damu uende sawasawa, hivyo kumfanya mwanamume apate hamu ya tendo la ndoa na pia kuwa na nguvu zaidi.

“Hatuhitaji hata maabara kupima umuhimu wa muhogo, nazi na karanga katika kuongeza nguvu za kiume. Kwa sababu nguvu za kiume siyo miujiza ni namna unavyoishi na kile unachokula,” alisema.

Daktari wa uchunguzi wa magonjwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Innocent Mosha alisema vyakula hivyo vinaongeza wingi wa mbegu za kiume kwa sababu vina mafuta na protini kwa wingi.

“Mafuta na protini vinazalisha seli na hivyo manii kuwa mengi. Kwa kifupi, hivi huweza kuongeza hamu ya tendo la ndoa, lakini kwa nguvu za kiume nadhani ni kwa sababu vyakula hivyo huongeza nguvu mwilini,” alisema.

Utafiti wa Mpemba

Mwandishi wetu pia alizungumza na Abeid Sultan Ghassani (81), mkazi wa Mjini Magharibi, Zanzibar ambaye kwa sasa anaishi Dar es Salaam.
Ghassani alisema wengi hawajui kuwa ili kuwa na nguvu za kiume huna haja ya kutumia dawa za hospitali, bali vyakula vya asili.
Ghassani ambaye ana wake watatu, alijisifu kuwa mpaka sasa ana nguvu za kutosha kwa kuwa katika maisha yake amekuwa akila muhogo, karanga, nazi na samaki vibua.

pic%2Bmihogo.jpg

“Tunakula vyakula vya asili vilivyotoka shambani, muhogo mbichi na kila kitu hakijawekwa kemikali, kwa nini nisiwe imara kama simba?”
 
Da'Vinci

JF-Expert Member
Dec 1, 2016
29,537
2,000
Kazi mnayo wanaume wa darisalama..
Mm asubuh ninagonga kipolo cha dona na mgebuka mbichi, kisha naingia shamba nachimba ogo langu la haja kisha nachukua na bakuli la karanga kisha nafuna taratibu na kidumu cha maji pembeni..
Mchana nagonga futari ya viazi au mihogo na mtindi..
HESHIMA KWETU MIKOANI BOYS NA MEN..
 
msakaa jr

JF-Expert Member
May 18, 2017
3,156
2,000
Tunatibu magonjwa yote bila kusahau upungufu wa nguvu za kiume waganga wa siku izi buana ngachoka.
 
Norshad

JF-Expert Member
Jun 3, 2013
4,527
2,000
Joto hupunguza nguvu za kiume, angalia tatizo hili lipo sana ktk nchi za sahara na zenye joto kali mfano dubai na Oman hasa Oman naweza sema robo wanatatizo hili akili yangu inanituma hivyo, pia kwa wanaume wa Dar sijui wana shida gani, dar lazma guvu ztapungua tuu KWANZA KUKAA MUDA MREFU KTK FOLENI HUKU UKIWA UMESIMAMA IWE MWENDO KASI AU DALADALA HUKU DUME LENZAKO LIMEKUSIMAMIA KWA NYUMA LINAKUPUMULIA KISOGONI,tabia hii ikiendelea kila siku unajikuta unazoea kupanda mwendo kasi ili uguswe na zipu za wenzio, Urijali hauji kwa kutafuna mihogo njiani huku ukifika kwako unaenda kula chips yai na pepsi ya baridi ama unanudi nyumbani umebeba ki broiler chako unapelekea familia,

Kuleni mbegu za maboga, kuleni maboga, tafuneni vitungunguu maji, tumieni matikiti, kunyweni juice za ndizi na maziwa, mihogo ya kuchemsha asali, chocolate kabla ya, kahawa ya buni, mamung'unya, magimbi viazi vitamu, lakini ninyi wazee wa wali na mchuzi wa mafuta, angalieni ndugu zetu wapemba mchuzi maji na samaki na nyanya mbili kamaliza, akipigilia na urojo wake hapo, sasa mwauzarau urojo bila kujua mla ulojo na mla broiler wako tofauti sana

Endeleeni kutupa promotion wa mikoani maana ukiona mkeo safari za mikoani haziishi na akirudi atabasamu tuu ujue huko aendako anakutana na wanaume...shenz kbsa.....unakula nazi, karanga za mia mbili, njiani wakati vitu hizi watakiwa ule nyumbani inatakiwa ukimwaga mzigo ujaze kikombe cha kahawa na muda wowote uwe tayari kwa game.......Wavulana wa Dar.....unaingia na manzi alafu wewe ndio unaskika unagumia huku nje badala ya manzi wewe ndio unaonekana kama unabanduliwa huko ndani.......mnapotea kwa kukosa maarifa
 
Mshuza2

JF-Expert Member
Dec 27, 2010
7,772
2,000
Mbona hujatoa credit ulikokopi hii habari..btw shukurani kwa kushea..
 
koba lee

JF-Expert Member
Sep 29, 2016
408
500

Mzee umeua,nadhan watakua wameelewa
 
nyanimzungu

JF-Expert Member
Mar 4, 2017
1,211

Ai thinki yua righti

Sent from my Halotel H8401 using JamiiForums mobile app
 
sisame

JF-Expert Member
Nov 1, 2016
365

Imebidi tu nicheke kwa sauti....ati njemba ndio inabanduliwa na manzi.....haaaaah haaaaah....lol
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom