Siri iliyofichwa kwenye safari ya mafanikio

pureman2

JF-Expert Member
Aug 21, 2019
1,494
2,538
Kila ukiuliza Watanzania 10 nini kinachowaumiza kichwa, 8 kati yao watakuambia changamoto za maisha ni jinamizi linalotesa familia, mahusiano, urafiki na hata taaluma zao.

Wengi wanaishi na swali lini mambo yatakua sawa? au wapi ninafeli?

Kutafuta jibu hilo -wengine wameamua kukimbia familia zao, wengine wanashinda kwa manabii na mitume- wakiongeza upako na kukanyaga mafuta ili kuvunja nira na uchawi, wengine kutwa kuvunja nazi njia panda na kuchomewa hubani kwa mashekhe- ili kuvunja mikosi na laana, wengine wamezama kwenye ulaibu wa pombe na madawa ili tu kujipa fursa za kusahau shida na matatizo yao.

Yote haya ni kuonyesha kuwa hakuna jibu la moja kwa moja juu ya swali hili la lini mambo yatajipa.

Napenda ufahamu hili ni fumbo la maisha. Hata waliofanikiwa wengi ukiwaeleza nini special walifanya ili kufanikiwa Unaweza shangazwa na majibu ya wengi wakikuambia Kuna U-turn moja ilitokea bila kutarajia ikabadiri upepo kabisaa. Mchongo , au fursa moja ilitokea from no where ika change game kabisaaaaa.

Fumbo hili sio ruksa ya kubweteka na kutokimbizana na fursa. Daima do your best, weka mipango, Jenga uwezo na ujuzi, pambana na wala usikate tamaa, na zaidi ya yote ishi kwa matumaini chanya.

Kuna usemi mmoja husema fursa huwapata waliojiaandaa.

Wakuu ebu tujengane - nini kilikutoa kimaisha? Na je, ulikikusudia au ndo zali la mentali?
 
Akina Pierre liquid mtu yupo busy anapiga mitungi mara paaap umaarufu huu hapa mara madili kama yote saivi maisha mazuri mitungi kama kawa.

Maisha hayana formula aiseee
 
Principle of success
1. Purpose (kusudi)- destiny

Kusudi ni jambo ambalo umeumbiwa kufanya mfano ndege kaumbwa kuruka ,Samaki kaumbwa kuogelea ,mbegu imeumbwa kuota

2. Persepection(maono)-vision
Huwezi kwenye sehemu ambayo huioni kuwa jijengee picha mwenyewe nitakuwa na kampuni yangu mbele nitakuwa na biashara zangu pale kariakoo nitakuwa na shamba kubwa na kuzalisha mahitaji nitakuwa na shule yangu na kusomesha wanafunzi na shule yangu itakuwa Bora

3. Potential (uwezo)-ability
Lazima uwe na uwezo nacho hicho ambacho unataka kufanya lazima kama hauna uwezo nacho utaona umelogwa unafanya biashara moja na mwenzako ,mwenzako anafanikiwa lakini wewe bado hali yako inazidi kushuka na hasara inazidi kuwa kubwa

4. Passion (hamasa )-desire
Kuwa na hamasa na kile ambacho unafanya kutokana na Matunda ambayo utayapata au mambo ambayo unayaona

5. Principles (kanuni)-laws
Kuwa na kanuni zako
Mfano sitaondoka kazini paka niandike matumizi yangu ya kila siku ,sitakuwa mtu wa starehe bali mtu wa Juhudi

6. Planning(mipango)- strategy
Weka mipango yako vizuri baada ya kutoka hapa nitaenda pale baada ya kutoka pale nitaenda kule kufikia kwenye lengo lako kuu ambalo umeliweka mwanzoni kabisa

7. People (watu wanaokuzunguka)-influence
Ukikaa na watu wa chini na wewe utakuwa chini ukikaa na watu ambao wanawaza ya juu nawe utakuwa juu ndio maana matajiri huwa Hawakai sana na maskini kwasababu ya utofauti wao wa fikra na malengo yao

8. Persistence (kuendelea)- commitment
Kuweka Juhudi katika kile ambacho umeanza kufanya na kuendelea kukifanya kwa bidii kubwa

9. Perseverance (uvumilivu) - dedication
Kuwa na uvumilivu utapingwa na kukataliwa lakini wewe usikate tamaa wewe endelea kupambana paka kieleweke

10. Prayers(maombi) - Spiritual reserve
Wale wachawi na wengine sio rahisi sana kiathiri unachofanya kama utakuwa mwana maombi

Nawasilisha
 
Iko njema
 
Back
Top Bottom