Siri iliyofichwa kuhusu BIBLIA

NIV ni kitabu batili cha biblia na wakristo wote wanatakiwa wazitupe kwenye dustbin au zipelekwe kwenye vijiji visivyo na maji ya kutosha kwa ajili ya kuchambia....Scholars wote walioiandika (New International Version) mkristo una haki ya kuwajua pamoja na tabia zao chafu,,zaidi pia wafadhili wa kuandika hio biblia ni watu wasio sahihi,,,kila mkristo awafatilie ili ajiridhishe kuhusu njama na mwenendo wao ili kuitupa chooni hii version.KING JAMES VERSION ni biblia sahihi ilioandikwa na schollars sahihi wakati bado ulaya kukiwa na hofu ya MUNGU.
Hivyo vitabu kama kitabu cha yashari,,enock,,esdras,,judith,,tobith na vingine vingi vya kihistoria havina nafasi katika biblia yenye lengo kamili la Imani maana vimejaa mashairi na historia isio na faida katika maisha ya kiroho na kiimani kwa mkristo makini aliemuamini YESU KRISTO.Ni vitabu vizuri kwa ajili ya kufundishia darasani.

Mfano miaka michache imepita serikali ya South Afrika imeingiza mtaala wa uchawi katika mtaala wake wa elimu ya juu,,,degree,,masters,,phd nk.Sasa sitoshangaa serikali ya Afrika ya kusini kukitumia kitabu cha enock kama reference.
sasa mbona hata KJV nayo ina contradict sehemu nyingi
 
Earthen scrolls nyingi ziliongezwa aidha kupunguzwa aidha kubadilishwa na COSTANTINE WA ROMA!
IPO SHIDA ETHIOPIC SCROLL NYINGI NI ZA KALE ZAIDI KULIKO SCROLL ZA KOKOTE KULE DUNIANI, VERY COMFUSED! HATA ETHIOPIC BIBLE SCROLL ZINATENGENEZA BIBLIA KUBWA KWELI YA KUSTAAJABISHA!
 
MAANDIKO YENYE UTATA
Kuna mistari mingine ambayo ni halali kibiblia ila imebadilishwa maeneo husika ipo mistari zaidi ya 50 kwenye agano jipya mfano Yohanna 7:53-8:11 kuhusu Yesu kuwepo hekaluni ila ghafla kipande kati ya 7:52 na 8:11 vimechomeka story ya mwanamke kahaba alietaka kupigwa mawe na ghafla mstari wa 12 unaendelea Yesu akiwa hekaluni hii inakubaliwa na wanatheolojia wote kuwa kilichomekwa na hakikuwepo kwenye maandiko orijino kama una biblia hapo kasome hiki kipande alafu utaelewa nachosema. Kanisa likaamua kuita vitabu vyenye maandiko na uandishi wa utata kuwa ni disputed books ilihali zina sifa zile zile za kuitwa pseudepigraphi na kutakiwa kufutwa kwenye biblia. Mfano Marko 16 inaishia mstari wa 8 ila 9-20 haikuwepo bali iliongezwa miaka mingi mbele na mtu asiyetambulika ila bado kipo kwenye biblia lakini kitabu cha Enoch au Yuda iskariot vimetolewa kwa hoja hiyo hiyo?? Kuna ajenda gani hapa wakuu?? Kipi tunafichwa?? Anyway disputed books kulingana na mwanatheolojia E. P. Sanders ni waefeso,wakolosai,2 wathesalonike, 1 & 2, Tito na vingine vingi.... Je kama vina kasoro kwanini vimeachwa??

VILIANDIKWA NA MUNGU?
Kuna hoja inasema vitabu vya Biblia viliandikwa kwa uweza wa Roho mtakatifu hivyo vile vilivyoachwa havikuandikwa na Roho mtakatifu sasa tujiulize GT kama kuna mistari ya Biblia imeongezwa na wanadamu mfano isaya,wimbo ulio bora,Tito,Yeremia,marko je bado hoja hii ina mashiko ilihali wanatheolojia wanakiri biblia ilichezewa kwa mifano niliyotoa hapo juu na kama si kweli viliandikwa kwa uweza wa Roho bali fahamu za wanadamu je kwanini basi ilitumika kuzuia vitabu kama Injili ya Yuda ama Thomaso?? Je hakuna agenda ya siri kwanini vilizuiwa alafu sisi tukaaminishwa tu kuwa havikuwa na uvuvio wa Roho mtakatifu??
View attachment 830349
PSEUDEPIGRAPHI ZINAKINZANA NA BIBLE
kuna hoja ilitolewa kwamba vitabu vya biblia vinakinzana na Pseudipigrapha ndio maana vikatolewa kwenye bible ila cha kujiuliza GT mbona kuna taarifa zinakinzana ndani ya biblia lakini havijatolewa??

MIFANO
Mathayo 4:1-11 inasema mara tu baada ya ubatizo Yesu alienda kufunga siku 40 ila Yohana 2:1 anasema siku tatu baada ya kubatizwa Yesu alikua kwenye harusi ya Cana!!

Au mathayo 27:44 wale wezi wawili walimtukana Yesu ila luka 23:39 inasema mmoja alitukana mwingine alimtetea.

Mathayo 28:9 inasema Yesu baada ya kufufuka aliruhusu Mary amshike ila Yohana 20:17 Inaonyesha baada ya kufufuka na kuonana na mary, Yesu akamzuia kumgusa sababu alikua bado hajarudi kwa Baba!!

Hiyo ni mifano tu ila kuna mistari zaidi ya mamia inayopishana taarifa ila vimeachwa kwenye bible lakini pseudipigraphi zikipishana hata neno moja ndio wanajengea hoja kwamba ndio sababu havipo kwenye bible je sababu hii ilisababisha vitolewe ama kuna mengi tunafichwa?

HITIMISHO
Kwa kuhitimisha labda niseme tu kumekuwa na maswali mengi juu ya chanzo hasa cha vitabu vingine kutolewa kwenye biblia na vingine kuachwa wakato vina kasoro zile zile..... Na hata mkuu Pendael24 alishawahi kuhoji kwamba kama tunafikiri biblia imechezewa je Mungu haoni hadi aruhusu hilo?? Na akahoji mbona Biblia inatenda ina maana kazi ya forgery inaweza kuwa na nguvu za Mungu na akanihoji je wachungaji wote hawa wakubwa hawalijui hili kiasi Mungu awaache watumie bibloa iliyochakachuliwa?? Kiukweli nilikosa majibu ila nategemea leo humu majibu yote yatapatikana

NB: Mimi nimechokoza mada tu ili kupata maarifa ya GT ila sio msimamo wangu kuwa bible ni batili au Qur'an ndio sahihi hivyo tunapojadili hoja humu tuhakikishe tunazingatia hilo pia udini na kejeli na matusi sio uwanja wake humu, nataka tujadili kwa kujifunza sio kupambana.

Karibuni kwa mjadala
All in all biblia ni juu au tuseme inafichua juu ya
1.uumbaji wa Mungu,
2.chanzo cha dhambi
3.madhara ya dhambi
4.ukombozi kutoka kwenye dhambi
5.dunia mpya-yaani kwenda mbinguni
Sasa kama kuna kitabu kitakuwa na mada tofauti na hizo lazima kitolewe
 
Back
Top Bottom