Siri CCM yafichuka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siri CCM yafichuka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Josh Michael, Oct 4, 2009.

 1. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #1
  Oct 4, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  MKAKATI wa kuwadhoofisha kisiasa baadhi ya wabunge waliojipambanua kuwa wapambanaji wa vita ya ufisadi ambayo imekigawa Chama Cha Mapinduzi (CCM) pamoja na Bunge umebainika.

  Wabunge walioandaliwa mkakati huo ni Christopher ole Sendeka (Simanjiro), Samuel Sitta (Urambo), Fred Mpendazoe (Kishapu) Lucas Selelii (Nzega), James Lembeli (Kahama) Anna Kilango Malecela (Same Mashariki) na Dk. Harisson Mwakyembe (Kyela).

  Tanzania Daima Jumapili, imebaini kuwa mkakati huo ambao umeanza kutekelezwa na Rais mstaafu, Ali Hassan Mwinyi na Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, wameamua kuziba mashimo na kuzima moto wa hoja hiyo ili isionekana kuwa ni kundi la wabunge wachache bali ni ajenda ya chama hicho.

  Mbali na hatua hiyo, CCM imepania kwa kiasi kikubwa kufanya ajenda hiyo kuwa ya kitaifa ili kutishia nguvu na uhai wa kambi ya upinzani ambayo ndiyo iliibua mjadala huo.

  Wachunguzi wa masuala ya kisiasa wanasema, ajenda hiyo ambayo iliibuliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa kutaja hadharani majina ya viongozi waliowaita mafisadi, sasa inaonekana kupokwa kwa nguvu zote na CCM ili kujijenga mbele ya macho ya jamii.

  Licha ya hali hiyo, kinachoonekana sasa ni kuwa nguvu ya kina Dk. Mwakyembe na wenzake ya kukinusuru chama hicho inaelekea kupwaya.

  CCM chini ya Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete, wamekuja na mkakati mzima ambao wanaamini utawasaidia dhidi ya wabunge wapambanaji.

  Kwa mujibu wa chanzo kimoja cha Tanzania Daima Jumapili, kimedokeza mkakati huo umeanza kwa viongozi hao kuwa pamoja na baadhi ya wabunge hao katika majimbo yao kila wanapofanya mikutano ya hadhara ili ionekane vita wanayoipigana ni ya chama na si ya watu fulani kama inavyoonekana hivi sasa.

  Wabunge walio mstari wa mbele katika vita ya ufisadi wameonekana kuwa tishio ndani ya chama na kukubalika katika jamii, hivyo kutoa hofu kwa CCM kuwa kama isipoungana nao inaweza kupoteza viti vingi vya ubunge, hususan watu wanaotuhumiwa kwa ufisadi.

  Mkakati huo ambao kwa hivi sasa pia umekuwa ukitumika kama mapambano baina ya wale wanaotajwa kujijenga ndani na nje ya chama kwa lengo la kuwania nafasi ya urais mwaka 2015.

  Wakati mkakati huo ukianza kutekelezwa, tayari baadhi ya watu wamekwisha kubaini mbinu hizo na kuwapa tahadhari wabunge hao ambao katika siku za hivi karibuni, wamekuwa vinara wa mapambano ya ufisadi unaodaiwa kufanywa na wanachama wenzao waliopata kushika nafasi za juu serikalini na ndani ya CCM.

  Kitendo cha Rais msataafu Mwinyi, ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya kuchunguza chanzo cha uhusiano mbaya kati ya wabunge wa CCM na mawaziri, kupanda jukwaani katika Jimbo la Same Mashariki akiwa na Mbunge, Anne Kilango Malecela, kumezusha maswali kadhaa miongoni mwa wafuatiliaji wa masuala ya siasa hapa nchi.

  Wachambuzi wa masuala ya siasa wanabainisha kuwa Mwinyi hataweza kuwa msuluhishi mzuri au mtafutaji wa chanzo cha uhusiano mbaya kama ataendelea kushiriki katika mkakati huo unaotabiriwa kuwa mgumu na wenye kuhitaji ujasiri.

  Kilango, ambaye ni mmoja wa wabunge walio mstari wa mbele kutoa hoja nzito zinazoitoa jasho serikali na chama tawala, nafasi yake hivi sasa inaonekana kupata mpinzani ambaye ni mwanamke mmoja aliyekuwa kambi ya upinzani.

  Mwanamke huyo ambaye mpaka sasa bado hajatangaza hadharani licha ya kuwaambia jamaa zake wa karibu nia yake hiyo, ameonekana kusaidiwa na vigogo wa chama hicho wenye nia ya kumng’oa Kilango.

  Miongoni mwa vigogo hao wanaomsaidia mwanamke huyo ni wale waliokumbwa na kashfa ya ufisadi, ambao katika siku za hivi karibuni wamekuwa wakihaha kujinusuru na tuhuma zinazoelekezwa kwao.

  Wakati kukiwapo taarifa za mikakati ya kuwadhoofisha wabunge hao, Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, amebainisha kuwa uamuzi wa kusimama jukwaani akiwa na Spika Sitta ni kukiimarisha chama na wala si vinginevyo.

  Katibu Mkuu huyo amepuuza taarifa hizo kwa kudai zina lengo la kukichafua na kupandikiza chuki miongoni mwa wanachama ili wasiweze kuwa na umoja na mshikamano, vitakavyowawezesha kushinda katika chaguzi mbalimbali.

  Makamba kwa muda mrefu amekuwa akitaka watu wasikihusishe chama hicho na ufisadi, bali unafanywa na baadhi ya wanachama wa chama hicho ambao pia hawawezi kuwajibishwa kwa tuhuma mpaka watakapofikishwa mahakamani na kutiwa hatiani.

  Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wameweka wazi kuwa mkakati huo wa kuwadhoofisha wabunge machachari kwa hivi sasa ni hatari, kwa kuwa upepo wa wananchi ni kuona wale wote wanaotuhumiwa kwa ufisadi wanawajibishwa ndani ya chama na serikali.

  Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete amekwisha kuweka wazi kuwa hajawafunga midomo wabunge wa chama hicho kujadili mijadala mbalimbali, lakini ni vema wakaangalia isije ikakibomoa pamoja na serikali kinayoiongoza.

  Kikwete pia aliwataka vigogo kuacha kuzungumza mambo mazito hadharani, bali watumie vikao vya kichama kuzungumzia matatizo yao, hasa yale yanayokihusu chama na serikali.

  Kauli hiyo inaonekana kutofuatwa na baadhi ya vigogo, ambapo aliyekuwa Waziri Mkuu na Katibu Mkuu wa Umoja wa Afrika (OAU) mstaafu, Dk. Salim Ahmed Salim, ameweka bayana kuwa nchi haielekei pazuri, kwani serikali inaonekana kuwakumbatia matajiri na kuwasahau maskini.

  Dk. Salim, alisema kamwe serikali haiwezi kupambana na rushwa kwa kuwa mapambano yake yamejikita katika rushwa hiyo badala ya kuangalia mfumo.

  Wakati Dk. Salim akitoa kauli hiyo, aliyekuwa Waziri Mkuu Jaji Joseph Warioba naye hakuwa nyuma kutoa kauli nzito na kuonya kuwa kama pengo la walionacho na wasionacho lisipozibwa kuna kila dalili ya kutokea machafuko kwa siku za usoni.

  Warioba alibainisha kuwa wakati wa awamu ya kwanza chini ya hayati Baba wa Taifa, Julius Nyerere, wala rushwa walikuwa wakidhibitiwa sana na hakukuwa na pengo kati ya walionacho na wasionacho. Onyo la viongozi hao wawili dhidi ya serikali inayoongozwa na CCM limeonekana kuwakera baadhi ya wanasiasa wa chama tawala, kiasi cha kudai kuwa viongozi hao wamekuwa wakosoaji wakuu wa serikali na hawaoni zuri linalofanywa.
   
 2. Amosam

  Amosam Senior Member

  #2
  Oct 4, 2009
  Joined: Jan 15, 2009
  Messages: 154
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Propaganda ya Mbowe na wapambe wake hii,tumeishtukia!Hatudanganyiki!
   
 3. Semenya

  Semenya JF-Expert Member

  #3
  Oct 4, 2009
  Joined: Sep 5, 2009
  Messages: 572
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 35
  source TANZANIA DAIMA
  teh teh teh teh
   
 4. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #4
  Oct 4, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Sasa hapa Mbowe amefanyaje?? acha uzushi wewe jamani
   
 5. M

  Mayolela JF-Expert Member

  #5
  Oct 4, 2009
  Joined: Sep 21, 2009
  Messages: 383
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kama source ni hiyo -basi imeeleweka -mchezo mchafu wa mbowe?
   
 6. K

  Keil JF-Expert Member

  #6
  Oct 4, 2009
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hii habari ina walakini kwa kiasi fulani. Sidhani kama ni propaganda za Mbowe ila ni propaganda za mafisadi kwa kutumia magazeti ambayo hayako chini yao moja kwa moja. Chumba cha habari cha Tanzania Daima kimeingiliwa na kidudu mtu, kama siyo Mhariri Mkuu basi Mhariri Habari ama waandishi wamekuwa wakitumiwa kupotosha news na hasa zinazowagusa mafisadi.

  Kwanza Mzee Mwinyi alienda Ndungu kuzindua Kituo cha Afya, of which angealikwa mtu yeyote ambaye Mama Kilango angemuona anafaa kuhudhuria shughuli hiyo. Kwa bahati mbaya ama nzuri, kura iliangukia kwa Mwinyi ambaye tayari alikuwa ni Mwenyekiti wa Kamati ya kuziba ufa. Hatujui mwaliko ulienda kwa Mwinyi kabla ama baada ya kikao cha NEC. Maneno aliyoyasema Mwinyi jukwaani yalikuwa ni majibu ya kilio cha Mama Kilango ambaye alitoa machozi jukwani (kama ilivyoripotiwa na magazeti), kuhusu ufisadi na jinsi wananchi wa Tanzania wanavyozidi kuwa masikini wakati watu wachache (mafisadi) wakiendelea kuneemeka.

  Makamba alienda Urambo kujikomba kwa Sitta na ndiyo maana hakwenda kwenye jimbo jingine zaidi ya Urambo na Tabora mjini. Walishaona upepo haukuwa unavuma vyema na alitakiwa kwenda kufukia mashimo haraka sana ili kuepuka CCM kuwa na bad image ingawa tayari walishajipaka kinyesi kutokanana matamko rasmi ya Makamba na Chiligati ambayo yalitolewa mara baada ya kikao cha NEC. Safari ya Makamba haina uhusiano wowote na kuwanyamazisha wabunge waliotajwa. Bahati mbaya ama nzuri wabunge waliotajwa wote wana bif na Makamba na ndio walikuwa wanaongoza kampeni ya wabunge wa CCM wakitaka Makamba ang'olewe kwenye nafasi ya Katibu Mkuu, hiyo bif haijaisha na haitakuja kuisha.

  Lengo la habari hii ni kujenga mazingira kwamba Mwinyi amepoteza sifa ya kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya suluhu kati ya mafisadi na wapinga ufisadi kwa kuwa tayari ameonyesha msimamo wake uko wapi. Kwa hiyo mafisadi wanataka kutanguliza dukuduku lao kwamba Report ya Mzee Mwinyi itakuwa na upendeleo na haiwezi kuwatendea wao haki.

  Waliotajwa kwenye orodha iliyo kwenye habari ni wabunge kama 7, Mzee Mwinyi alialikwa kwenda Ndungu. Makamba alijialika mwenyewe wala hakuitwa kwenda Urambo. Je, sample hiyo ya wabunge 2 kati ya 7 inatosha ku-justify hoja inayojengwa? Mbona wengine kama Kimaro, Zambi na wengineo hawajatajwa?

  Wakati mwingine hawa waandishi wetu wa habari huwa wanatumika vibaya bila hata kufikiria kwamba wanaandika nini. Ukisoma hiyo news unakuta kuna gaps nyingi na hoja yao inapwaya. Hoja siyo uongozi wa CCM kuwanyamazisha hao wabunge bali ni mafisadi kutokuwa na imani na Mzee Mwinyi kwa kuwa ameonyesha yuko upande gani.
   
 7. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #7
  Oct 5, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Taifa linahitaji mabadiliko makubwa sana
   
 8. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #8
  Oct 5, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,314
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Tena yanataka yaanzie kwa kila mmoja wetu kama indivual
   
 9. b

  bnhai JF-Expert Member

  #9
  Oct 5, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,207
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Huu ni ufisadi wa kiandishi. Makala haina maana hata kidogo. Hakuna substance ndani yake
   
 10. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #10
  Oct 5, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,344
  Likes Received: 3,111
  Trophy Points: 280
  ila jamani ukweli ni kuwa hii habari haijatulia.......inaning'inia haieleweki.....
  CHADEMA wanahofu kuingiliwa kenye vita walivyoanzosha......wanaopambana wote ni watz.......tuwaache wapiganie nchi yao.
   
 11. MwanaCBE

  MwanaCBE JF-Expert Member

  #11
  Oct 5, 2009
  Joined: Sep 23, 2009
  Messages: 1,773
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 280
  Ebu tuwe makini kidogo tu. Ni nani anayepinga ufisadi katika CCM? Tangu lini? Kivipi? Kwa maslahi ya nani?
   
 12. B

  ByaseL JF-Expert Member

  #12
  Oct 5, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 2,223
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Gazet la Tanzania Daima Jumapili kusema kweli ni la ki-propaganda zaidi kuliko kuhabarisha hasa upande wa “lead strory”. Mara Nyingi vichwa vya habari katika Gazeti hili ni kama za kichambuzi zikilenga awamu ya nne ya utawala au CCM. Habari zenyewe ukisoma ni za kihisia zaidi (speculative news) kuliko utafiti (researched news). Ukisoma between the lines utaona mwandishi wa habari ndiye yule yule anayejiita “chanzo chetu cha habari” kinasema………..Vile vile anageuga na kujiita “wachambuzi wa mambo” wanasema………. Tunajua Tanzania Daima kimtazamo ni gazeti la upinzani lakini tunaomba watupe quality news za kipinzani kuliko hii “arm chair” journalism. Binafsi nalisoma Tanzania Daima Jumapili kusoma Makala zake ambazo ni nzuri.
   
 13. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #13
  Oct 5, 2009
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,145
  Likes Received: 1,238
  Trophy Points: 280

  Tafadhali usitujumuishe kwennye mafikara yako Sema umeishtukia na kwamba haudanyiki.

  Ukweli ndio huo, uliona wapi hawa wahuni kupiga U turn ya nguvu namna tena hawakuhitaji hata round about then wakafuata wapambanaji wa ufisadi

  Anyway nadhani lingeripoti gazeti la Uhuru nadhani ungeweza kusema Propaganda za Kikwete ama ungenyamaza. tehe tehe, ukishalambishwa ufisadi ......
   
 14. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #14
  Oct 5, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Pokea tano zako mkuu:D
  Umesema yote ingawa umekuwa kama umeuliza swali!
   
 15. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #15
  Oct 5, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Weeeeeeee! vita hii ni ya watanzania wote? are you serious?
  Hivi unataka kuniambia hii ni vita pia ya RA? Ni vita pia ya Chenge? ni vita pia ya Lowasa? hii ni vita pia ya Karamagi na Msabaha? Kweli hii ni vita ya Mramba? hii kweli ni vita ya Kikwete? na Yona? na Mkapa? are you serious you people?
  Hapa ndipo nataka ujue hii ni vita imeanzishwa na Chadema dhidi ya sisi ni Mafisadi. Wala si ya watanzania wote. Siku ikigeuka kuwa ya watanzania woet basi nchi itaishi kwenye neema wala hatakaa kupiga kelele za ufisadi hapa.
  Kataa kubali huu utabaki ndio ukweli!
   
 16. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #16
  Oct 5, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Hapa Chadema na Mbowe wameingiaje hadi wewe ni target ya direct attack ?Au mie sijaelewa vyema ?Hivi Watanzania wana haja ya kuelezwa kwamba si Chadema wenye list of shame na wakaisema hadharani ? Mie sijaelewa kwa nini mara nyingi tuna acha kujadili hoja na tunaleta vioja .
   
Loading...