Sir george kahama;nilitamani kuendelea kuwa madarakan kutimiza azma yangu; qwi...qwi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sir george kahama;nilitamani kuendelea kuwa madarakan kutimiza azma yangu; qwi...qwi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by sijafulia, Mar 27, 2010.

 1. s

  sijafulia Member

  #1
  Mar 27, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 86
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  MWANASIASA wa siku nyingi, Sir George Kahama ameungama mbele ya Rais Jakaya Kikwete, mambo matatu ambayo hakuyafanikisha wakati akiwa mtumishi wa umma na mojawapo ni ujenzi wa Makao Makuu ya Taifa Dodoma.

  “Nilitamani kuendelea kukaa Dodoma hadi kukamilisha kazi niliyokuwa nimekabidhiwa ya kujenga mji wa kisasa ambao Tanzania ingejivunia kama Makao yake Makuu yaliyoongozwa na Watanzania wenyewe katika ujenzi,” alisema Sir Kahama.

  Sir Kahama aliyasema hayo juzi wakati wa uzinduzi wa kitabu kinachohusu utumishi wake wa miaka 50, ambacho kimeandikwa na mtoto wake Joseph Kahama.

  Mwanasiasa huyo mstaafu alisema jambo la pili ambalo hakuweza kufanikisha, ni kuanzishwa kwa benki ya kitaifa ya ushirika wakati akiwa Waziri wa Ushirika mwaka 2000 hadi 2005.

  Alisema alidhamiria kuanzisha tena benki ya ushirika ambayo ingeshirikisha Saccos zote nchini kama wanahisa waanzilishi wakuu, lakini hadi utumishi wake ulipofikia kikomo mwaka 2005, aliambulia kuacha mwongozo wa uanzishwaji wa benki hiyo.

  Jambo la tatu ambalo alisema alishindwa kutekeleza, ni ndoto yake kwa Zanzibar wakati huo akiwa Balozi wa Tanzania nchini China.

  Alitamani aigeuze Zanzibar kutumika kama kichocheo mama cha kuchochea maendeleo makubwa zaidi ya kiuchumi kwa Tanzania na Afrika Mashariki.

  Naye Rais Kikwete amewataka wanasiasa na viongozi wastaafu kupendelea kuandika historia ya maisha yao ili jamii na vizazi vijavyo viweza kufaidika na kutambua maisha ya wanasiasa hao.

  Rais Kikwete alimpongeza mtunzi wa kitabu hicho, Joseph Kahama kwa kuandika kitabu kinachohusu maisha ya baba yake ambaye amekuwa waziri baada ya uhuru hadi awamu ya tatu ya uongozi wa Taifa hili.

  “Kitabu hiki kitakuwa na manufaa kwa Watanzania hasa kutokana na sifa nyingi za Sir George Kahama,” alisema Kikwete na kumwaga sifa nyingi ikiwemo ya mwanasiasa huyo kuiwakilisha vyema Tanzania wakati akiwa balozi katika nchi mbalimbali.

  Baadhi ya sifa alizozitaja Kikwete za Sir Kahama ni kuongoza mashirika makubwa hapa nchini kama Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC), Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA), na amewahi pia kuongoza Kituo cha Uwekezaji (TIC).

  Mtunzi wa kitabu hicho, Joseph alisema sababu za kuandika kitabu hicho ni shukurani ya watoto wote kwa baba yao akiwa bado hai kwa mchango wake mkubwa katika ujenzi wa Taifa tangu mwaka 1957 kabla ya uhuru hadi leo.

  “Kuna Mengi ya kujifunza toka kwake kuhusu namna alivyotumikia nchi yake bila dosari mpaka hapo alipostaafu,” alisema Joseph na kumtaja wakili maarufu mjini Arusha Nyaga Mawalla, kuwa miongoni mwa watu waliomsaidia kuandika kitabu hicho na kuchangia mawazo mengi.

  “Kwa kweli Nyaga ni kijana mbishi hasa kuhusu masuala ya biashara na uchumi pamoja na uchumi wa dunia…ni kijana msikivu na mnyenyekevu ndio maana amefanikisha kuandika kitabu hiki,” alisema Joseph.
   
 2. s

  sijafulia Member

  #2
  Mar 27, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 86
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jamani...mmmhhh

  umekuwa waziri tangu marehemu nyerere..wacha mkapa akaja kukupa 2000- 2005 badala ya vijana kuongoza wizara ukufanya unachosema jamani hata ukipewa urais utamaliza???tatizo la wengi wakiwa uongozini wanatimiza matakwa yao binafsi kwanza mwakani ntapitaje kwenye ubunge,,..sijajua alikuwa mbunge muda gani lakini mzee wetu dodoma nahisi aliichoka mwenye kwa kweli,..siku nyingi sana,..mzee wangu kahama sir george akuna anaemaliza kutimiza matakwa yake,...ila kuna kuanzisha bank bado unaweeza shirikiana na mwanao hata watu wa uko vijini wakanufaika na mzee ama kupata fadhila kwa kuchagua muda wote...bado una nafasi ingawa by eyes too late..... Mshukuru mungu kwa kuendelea kuwa na afya njema......

  Hongera kwa kulitumikia taifa miaka 50..bila kutimiza mawazo yako!!!mia tungemaliza kweli!!!!!

  Nakumbuka nikiwa darasa la .....waziri wa ushirika ni .....

  Sir george kahama...watu weweeee!!!!
   
 3. s

  sijafulia Member

  #3
  Mar 27, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 86
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Rais kikwete ujumbe umeupata huo!!!!

  Kazi kwako 2011...embu kakumbuke mzee wetu tena hata miaka miwili jamani amalize haja ya moyo wake asijelilaani taifa kwa kushindwa kumaliza aliopanga!!!yawezekana tatizo ni pesa wakati huo wakati huu kuna za waungwana wa epa zinaendelea kurudi embu mkumbuke mzee wetu

  kwenye wale ""old is gold"" mungu atakupa fadhila
   
 4. s

  sijafulia Member

  #4
  Mar 27, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 86
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Yaani ngoja nkalale tu nakula shule hata siku mja nije kuukwaa uwaziri kumbe kuna wengine wana hamu nao!!!!
  Bravo sir g
   
 5. saitama_kein

  saitama_kein JF-Expert Member

  #5
  Mar 27, 2010
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 982
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Sir George amekuwa muwazi kusema mapungufu yake katika enzi za uongozi wake...tunataka na viongozi wengine wastaafu wajitokeze kumuunga mkono............
   
 6. s

  sijafulia Member

  #6
  Mar 27, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 86
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  weeeeeeeeeeee mapungufu akila penshen yake

  ataje mapungufu hadharani akiwa kwenye uongozi!!!!amefikisha 25/35/40 ajaandikaama kukiri akiwa madarakani upungufu wake 2000-2005...,na nyuma yake ije leo hii ....mzee pumzika kila la kheri m nakuombea aafya njema
   
Loading...