Sipokei simu yenye namba nisiyoijua: Hii tabia imemkosesha jamaa ulaji wa nguvu!

ndyoko

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,971
1,649
Imekuwa ni tabia ya kawaida sana miongoni mwa wamiliki wa simu kutopokea simu ambayo namba yake ahijui. Hata hivyo ni ujinga wa kutojua matumizi hasa ya simu. Inawezekana nduguyo kapatwa na shida-sema ajali au jambo lingine lolote ambapo anahitaji msaada toka kwako na kuamua kutumia simu ya msamaria mwema kuwasiliana nawe. Kwa ujinga wako unaamua kutopokea. Au ukipokea, baada ya kuona usumbufu, unatoa lugha ya ukali-una shida gani, unataka nini, wewe nani unanisumbua? Na mengine mengi ya mtindo huo.

Tabia hii majuzi imemkosesha jamaa kazi nzuri-hebu fikiria kaenda kafanya usaili vizuri-computer interview, written interview, oral na mwishowe driving interview. Baada ya siku tatu wamarekani wakafika bei kwake, wakaamua kumpigia simu kumtaka waende wakakubaliane siku ya kuanza kazi na kufanya preliminary arrangement. Ile anapigiwa simu, kwanza ikamchukua muda kupokea.alipigiwa mara nne, ya tano ndo akaamua kupkea.

Ile anapokea tu maneno ya karaa tupu: 'Wewe nani unanisumbua, haya sema shida yako'. Ghafla akakumbana na kiingereza, "oooh, sorry james for the disturbance, I am (akataja cheo chake na ofisi). I just called to tell you that our office has decided to hire you. However, I am sorry my friend, the expression you have shown me when you received my call may not be good for our organisation with respect to the post you were to hold in our organsation'.

Jamaa akabaki, ooooh i am sorry Sir. Mshikaji akamwambia tu, 'thanks for your time', akakata simu. Mchezo ukaisha. Hebu fikiria, maana katika majadiliano ya interview walikubaliana mshikaji awe anakamata mshahara wa milioni 5.5.

Tuna la kujifunza hapa jamani. Kama huna matatizo ktk jamii kwa nini uogope kupokea simu yako mwenyewe? Yaani simu yako lakini ikipigwa unapata shinikizo la damu, why?
 
Ni upompompo!
Hivi inawezekana mtu ukawa na namba zote za jamaa, ndugu , Marafiki, Wafanyakazi wenzako, watu wa kijijini, school-mates, social affairs-mates na majirani zako?..Si rahisi!
Huyo mtu anakula jeuri yake!...pambaaaaf!
 
Hii mada ni ya jukwaa hili kweli?

Anyway, ni kweli mkuu, si ustaarabu kuacha kupokea simu usizozijua. Ni vizuri kuzipokea na kuomba mpiga simu ajitambulishe. Utambulisho unaweza kukuongoza nini cha kufanya kama huna mpango wa kuongea au kuendekeza mahusiano na mawasiliano na mtu usiyemfahamu.
 
Ni upompompo!
Hivi inawezekana mtu ukawa na namba zote za jamaa, ndugu , Marafiki, Wafanyakazi wenzako, watu wa kijijini, school-mates, social affairs-mates na majirani zako?..Si rahisi!
Huyo mtu anakula jeuri yake!...pambaaaaf!
i wish hisani ya watu wa marekani ije iwafanyie wanaume course ya communication skills maana hali zenu mbaya
 
Kuna watu wana misimamo ya kijinga kama ya sipokei simu nisiyoijua khaa! mi nafikiri ni uelewa mdogo wa mambo pia!

Wapo watu wengi tu tena wanaheshima zao wasiotaka kupokea simu mpaka wajue wanaongea na nani...ila kama ni mfanya buiashara halali, that is not the way to go about.
 
Imekuwa ni tabia ya kawaida sana miongoni mwa wamiliki wa simu kutopokea simu ambayo namba yake ahijui. Hata hivyo ni ujinga wa kutojua matumizi hasa ya simu. Inawezekana nduguyo kapatwa na shida-sema ajali au jambo lingine lolote ambapo anahitaji msaada toka kwako na kuamua kutumia simu ya msamaria mwema kuwasiliana nawe. Kwa ujinga wako unaamua kutopokea. Au ukipokea, baada ya kuona usumbufu, unatoa lugha ya ukali-una shida gani, unataka nini, wewe nani unanisumbua? Na mengine mengi ya mtindo huo.

Tabia hii majuzi imemkosesha jamaa kazi nzuri-hebu fikiria kaenda kafanya usaili vizuri-computer interview, written interview, oral na mwishowe driving interview. Baada ya siku tatu wamarekani wakafika bei kwake, wakaamua kumpigia simu kumtaka waende wakakubaliane siku ya kuanza kazi na kufanya preliminary arrangement. Ile anapigiwa simu, kwanza ikamchukua muda kupokea.alipigiwa mara nne, ya tano ndo akaamua kupkea.

Ile anapokea tu maneno ya karaa tupu: 'Wewe nani unanisumbua, haya sema shida yako'. Ghafla akakumbana na kiingereza, "oooh, sorry james for the disturbance, I am (akataja cheo chake na ofisi). I just called to tell you that our office has decided to hire you. However, I am sorry my friend, the expression you have shown me when you received my call may not be good for our organisation with respect to the post you were to hold in our organsation'.

Jamaa akabaki, ooooh i am sorry Sir. Mshikaji akamwambia tu, 'thanks for your time', akakata simu. Mchezo ukaisha. Hebu fikiria, maana katika majadiliano ya interview walikubaliana mshikaji awe anakamata mshahara wa milioni 5.5.

Tuna la kujifunza hapa jamani. Kama huna matatizo ktk jamii kwa nini uogope kupokea simu yako mwenyewe? Yaani simu yako lakini ikipigwa unapata shinikizo la damu, why?

Kwamba jamaa kafanya intavyuu...kaacha na namba ya simu (wazi watampigia na namba asoijua)......
Halafu hapokei namba asoijua.....well...kama ni kweli kampime akili 'huyo jamaa' yako!
 
Ni wengi kweli hao! Sijui ni ulimbukeni wa kutojua matumizi sahihi ya simu? Au ndio hizi simu za kujifunza sasa.
Inakera sasa sana unapompigia simu mtu wako kwa simu isiyo yako au simu ya mezani aidha asipokee kabisa au akipokea anajibu hovyo, ukimuuliza kisa atakujibu hiyo namba siijui. Usahihi ni kupokea kama desturi kisha kumsikiliza yule mpigaji anasema nini tena hapo ndio uamue.
Sawa na kusema "usikatae wito kataa maneno".
 
Wapo watu wengi tu tena wanaheshima zao wasiotaka kupokea simu mpaka wajue wanaongea na nani...ila kama ni mfanya buiashara halali, that is not the way to go about.

Exactly my point! na si biashara tu nazani hata kazi zingine mtu anaweza akapewa contacts zako na akataka kuclarify jambo! na. mambo mengine mengi! ila kiustaarabu ajitambulishe akishajua amepiga simu na huna namba yake sio tena we nani duh! kwenye communication skills watu wengi iko shida!
 
sasa hicho kingereza ni nukuu ama tafsiri isiyo rasmi? Maana sidhani kama jamaa alinyaka yote hayo. Ila ni fundisho kiukweli
 
Kwamba jamaa kafanya intavyuu...kaacha na namba ya simu (wazi watampigia na namba asoijua)......
Halafu hapokei namba asoijua.....well...kama ni kweli kampime akili 'huyo jamaa' yako!

Mkuu kama kweli uanze huo mchakato wa kupima mbona hiyo hospitali itakuwa 'overpopulated'! usiniambie hujakutana na watu wa sampuli hii.
 
Back
Top Bottom