Sipo tayari kulea mimba kabla ya ndoa

binywa

Member
May 31, 2012
18
2
Habari zenu wakuu,
Leo naomba ushauri wenu.
Nina mchumba wangu ambaye nimeshamlipia mahari na tayari nimemvisha ya uchumba. Jana jioni aliniambia kuwa ni mjamzito na kuwa hiyo mimba ni yangu, kwa kuwa namwamini sina tatizo na hilo. Ila tatizo langu ni kuwa kwa sasa ssipo tayari kulea mimba hapo tutakapofunga ndoa. Tunategemea kufunga ndoa Feb 2013
Kwa kweli nipo njia panda na ninafikia hadi wakati namemwambia my fiancee kuwa aafanye abortion jaapo yeye anakataa.
Naombeni ushauri katika hili coz nimekosa raha kabisa. Na jambo la pili km nikifanya abortion je ni njia zipi salama za kufaanya jambo hili (japo naajua ni illega)
Naombeni ushauri wenu tafadhali
 
kasheshe , yaani ufikirie kuabort kwa mtu ambaye ni official mchumba wako,kazi kwelikweli hilo fundisho uwape wadogo zako we ushachelewa, lea mimba tu ila jiandaeni kwenye kutafuta shela
 
......hivi mnajua kazi ya tendo la ndoa?...........

EBU TSAIDIA KUMUULIZA UYU, IVI WAFANYA TENDO BILA KONDOM Den UNATOA MACHO KWA MSHANGAO, LKN C MBAYA ATA UKIITOA UNAMUUA MWANAO PIA UNALEGEZA KIZAZ CHA MTARAJIWA WAKO, DOGO ACHA ULOFA
 
Mbona siku hizi ma bibi harusi wengi wanafunga ndoa na mimba hata za miezi nane!!

Mie sioni sababu ya kutoa hiyo mimba... ( Angalizo: Mimba siku hizi ngumu kupatikana jamani)

Huo uamuzi unaotaka kuufanya unaweza kuwagharimu sana..!
 
naomba ueleze jukwaa kwa nini hauko tayari kulea mimba kwa sasa....naje,katika abortion,akipoteza uwezo wake wa kupata tena mtoto,utamlaumu nani?....katika abortion akiumwa ,atakayeingia gharama si wewe/,na ujue kuna uwezekano wa yeye kufariki kama hamtakuwa makini,huoni kwamba utapoteza mke?;;;;;;na pia unafahamu hiyo mimba ndio firstborn wako?....fikiria kama mama yako angekutoa,kwa shindikizo la baba yako........KUOA SIO FASHION,NI HATUA......TUMIA HEKIMA.
 
kha!! wanawake hawa bana...sasa kwa kuwa umempa pete ya uchumba ndio anadaka mimba?
wee mbwage na mwambie hapa hamna tena ndoa maana mambi gani hayo ya kutegana...kwani ulimwambia wataka mtoto? make her pay kwa kumbwaga. wamezidi sana hawa wanawake kudaka mimba wakati njemba hajakwambia kuwa anataka mtoto
 
kasheshe , yaani ufikirie kuabort kwa mtu ambaye ni official mchumba wako,kazi kwelikweli hilo fundisho uwape wadogo zako we ushachelewa, lea mimba tu ila jiandaeni kwenye kutafuta shela

SIO SHELA, BALI PIA LILE GUO WANALOVAA WANAWAKE WENYE MIMBA, MAJI YAKIMWAGIKA HAYAZOLEKI, MLEE MAANA YAWEZEKANA NDO MTOTO PEKEE ALOKPANGIA MOLA WAKO IVO USIITOE IYO MIMBa
 
Hakuna njia salama ya kutoa mimba, pia kutoa mimba ni dhambi ya kuuwa, sasa kama ni mchumba wako unaempenda na unapanga kumuoa, kwa nini usikubali hili jukumu hata kama hamkupanga iwe hivi, kuna mambo mengine hutokea tofauti na vile tunavyopanga lakini tunapambana nayo in a positive way na maisha yanaenda.
 
Sasa si uwahishe harusi iwe December ILI UILEE HIYO MIMBA NDANI YA NDOA!!!!!!!!!! Mambo mengine kama YA KICHAWI/ USHIRIKINA vileee!!!!!!!!!

Kweli hayo mawazo yao utafikili wapo gamboshi aisee We eti uuwe maisha ya asiye na hatia kisa tuzae ndani ya ndoa,Ndoa inafungwa moyoni sio kwenye matarumbeta.KUNA NDOA NA HARUSI/SHEREHE
 
kha!! wanawake hawa bana...sasa kwa kuwa umempa pete ya uchumba ndio anadaka mimba?
wee mbwage na mwambie hapa hamna tena ndoa maana mambi gani hayo ya kutegana...kwani ulimwambia wataka mtoto? make her pay kwa kumbwaga. wamezidi sana hawa wanawake kudaka mimba wakati njemba hajakwambia kuwa anataka mtoto

We vipi kwani hiyo mimba aliipata kwa njia ya hewa?
 
wewe ebu jipange ufanye ngono zembe harafu umwachie mzigo mtu mwingine ungelijua hilo ungetumia kinga ebu acha ulofa huo.
 
kha!! Wanawake hawa bana...sasa kwa kuwa umempa pete ya uchumba ndio anadaka mimba?
Wee mbwage na mwambie hapa hamna tena ndoa maana mambi gani hayo ya kutegana...kwani ulimwambia wataka mtoto? Make her pay kwa kumbwaga. Wamezidi sana hawa wanawake kudaka mimba wakati njemba hajakwambia kuwa anataka mtoto

maoni aya hatari sana, usiyachukue, kwani mimba ni ya nani? Si yenu nyote? Nina muimagine uyo mtoto malaika kila siku akilia kuwa atapenda kuwaona baba na mamake, dah uyu nae mshari anakushauri umtose? Plz brother siku izi imekuwa dil kuwapa mimba mademu, wagumba kibao siku izi
 
kha!! wanawake hawa bana...sasa kwa kuwa umempa pete ya uchumba ndio anadaka mimba?
wee mbwage na mwambie hapa hamna tena ndoa maana mambi gani hayo ya kutegana...kwani ulimwambia wataka mtoto? make her pay kwa kumbwaga. wamezidi sana hawa wanawake kudaka mimba wakati njemba hajakwambia kuwa anataka mtoto

kitendo cha wewe njema kufanya mapenzi kavukavu maana yake ushakubali matokeo eiza mimba au VIRUSI ,haina haja ya kuuliza hapo,alllaaaaaaaaaaaaaa,ambwage aone raha ya mwanawe kulelelewa na wanaume wenzie ye atafute mwingine amjaze mimba responsibo men walee
 
Habari zenu wakuu,
Leo naomba ushauri wenu.
Nina mchumba wangu ambaye nimeshamlipia mahari na tayari nimemvisha ya uchumba. Jana jioni aliniambia kuwa ni mjamzito na kuwa hiyo mimba ni yangu, kwa kuwa namwamini sina tatizo na hilo. Ila tatizo langu ni kuwa kwa sasa ssipo tayari kulea mimba hapo tutakapofunga ndoa. Tunategemea kufunga ndoa Feb 2013
Kwa kweli nipo njia panda na ninafikia hadi wakati namemwambia my fiancee kuwa aafanye abortion jaapo yeye anakataa.
Naombeni ushauri katika hili coz nimekosa raha kabisa. Na jambo la pili km nikifanya abortion je ni njia zipi salama za kufaanya jambo hili (japo naajua ni illega)
Naombeni ushauri wenu tafadhali

Hiyo ni damu yako, usimuue mwanao. Kaza moyo lea mimba maana hauwezi kujua ya kesho. Inawezekana huyo ndo mwanao wa kwanza na mwisho, ukitoa mimba na kumuangamizia mbali mwingine utatoa wapi? Nakushauri, achana na hizo fikra. Kiumbe hiko hakina hatia na adhabu ya kifo kwake haimstahili kwa namna yeyote ile.
 
Kweli hayo mawazo yao utafikili wapo gamboshi aisee We eti uuwe maisha ya asiye na hatia kisa tuzae ndani ya ndoa,Ndoa inafungwa moyoni sio kwenye matarumbeta.KUNA NDOA NA HARUSI/SHEREHE

Aaa dogo umenifuraisha sana kwa ushauri mulua, lkn gamboshi unapajua weye?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom