Sipigi debe..lakini kumbe ni kweli!!!

Tulizo

JF-Expert Member
Jun 13, 2011
848
662
Duh!!!! Sipigi debe..lakini kumbe ni kweli!!! nimepata kwenda na kurudi kwa shs. 86,000.. Hatimaye napanda pipa......

FastJet.jpg
 
mbona ticket imeandikwa january?? hebu nielewesheni hapo....umeshalipanda au utalipanda??
 
Aisee na mimi sitaki kuja kuhadisiwa ngoja na mimi niwahi!
 
Usipokuwa na wasiwasi nayo basi inabidi na mimi niwe na wasi wasi na wewe, hivi Community Airline ya Diallo iko wapi?

Diallo atakuwa anajua ilipo, ila nakumbuka ilianza kwa mbwe mbwe kama hivi.
 
Usipokuwa na wasiwasi nayo basi inabidi na mimi niwe na wasi wasi na wewe, hivi Community Airline ya Diallo iko wapi?
Community kwa taarifa nilizokua nazo ilikua bad business pengine walikua wanakwepa na kodi za hapa na pale, lakini hakukua na sustainability for obvious reasons. Sasa nna mashaka sana na hii the so-called "Fastjet"..maswali ni mengi kuliko majibu/
 
Ila kama iko moja tu inaaaaanza nitia wasiwasi!
isijekuwa DESI......... ................:confused2:
 
Kubalini kuwa tulikuwa tunalizwa sana kwa kuwa hapakuwa na ushindani. Natamani TANESCO nao wapate mshindani bei yao iko juu mno.
 
Kama ndivyo, hizi bei ni za muda tu. Hii inanikumbusha mapema mwaka jana, British Airways ilianzisha promo kama hii kwa safar kati ya Cape Town na Dar. Nakumbuka jamaa akilipa R1300 (sawa Tsh. Laki mbili na kidogo) kwa one way. Wakati huo huo airlines kama SAA wakiuza R4500 na zaidi. Ile route haipo tena.
 
Mliokata tiket za january mtakuja lia,haya mambo ya kukimbilia vitu rahisi rahisi huwa yanagharimu sana,ningekuwa na uhakika na hawa jamaa kama wangekuwa na hata ndege mbili ili moja ikigaribiaka basi wawe na nyingine ya kusaidia,siombei mabaya yatokee ila twende na nauli hizi tukiwa tunajiuliza maswali pia.
 
wakati wengine wanaendelea kuwa na wasiwasi, mimi nimeshakata tiket yangu kurejea saridalama mwezi huu. Sitaki kuishi kwa wasiwasi, ingekuwa biashara yagu sawa.
 
wakati wengine wanaendelea kuwa na wasiwasi, mimi nimeshakata tiket yangu kurejea saridalama mwezi huu. Sitaki kuishi kwa wasiwasi, ingekuwa biashara yagu sawa.
typical mdanganyika..kwa hio hujali kama wanalipa kodi, hujali kama ndege inazingatia safety, flying guidelines & regulations, etc etc
 
Back
Top Bottom