Sipendi kusikia upendeleo kwa wanawake!

Jackbauer

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
6,005
2,140
Napata hasira kusikia tumeteua majaji,wabunge na sasa wagombea uspeaker kwa misingi ya upendeleo kwa wanawake.hii haisaidii chochote kwa maslahi ya wanawake wenyewe na taifa kwa ujumla.serikali ilipaswa kufanya jambo moja tu;kuweka fair ground kwa jinsia zote kushindana,mfano kuhakikisha watoto wa jinsia zote wanapelekwa shule.let them compete mbona nimesoma na wasichana vichwa sana ambao hawakuhitaji upendeleo?ndio maana utakuta watu wenye uwezo wa kuingia chuo wanaachwa badala yake wanachukuliwa vilaza( kwa kigezo cha wanawake) wanapigwa msasa then wanaingia chuo.ombi langu kwa watz ni kwamba tusiwe kama kasuku kila linalosemwa na wazungu ni zuri.tuzingatie tuko kwenye hatua ipi ya maendeleo sio kuiga iga kila kitu.shame on cc!!mmezoea kutufanya wajinga ee?hamkomi ee?iko siku yenu.maoni yangu kwa wabunge wateule wachague speaker anayefaa. sio wa chama,dini au jinsia fulani bali atakayeweka maslahi ya taifa na utaifa mbele.
Mungu ibariki Tanzania na watu wake wa jinsia zote.
 

mmlaponi

Member
Jan 29, 2010
23
3
mkuu nakuunga mkono kwa 100% hii haiko sawa kabisa badala ya haki sawa hii inakuwa ni upendeleo kwa wanawake!Wanaume tuamke tuache poteza haki zetu kwa kisingizio cha jinsia!
 

hashycool

JF-Expert Member
Oct 2, 2010
6,566
2,805
mkuu nchi ya wasanii hii hujui? na kama uwajuavyo wasanii na mademu damudamu unategemea nini sasa hapo?
 

mageuzi1992

JF-Expert Member
Apr 9, 2010
2,503
251
Mungu wetu Mungu wetu kuna nini Tanzania
Nchi yetu inauzwa Mafisadi wana nia
Tuhurumie Mungu wetu mafisadi zao nia
Nchi yetu nchi yetu Mafisadi waiuza

Angalia zao nia Matokeo chakachua
Wenye haki wananyimwa Kura zao Kuibiwa
Kwa kishindo watangaza Aliyeshindwa Kashinda
Nchi yetu nchi yetu Mafisadi waiuza

Nawaombea Mabaya Mafisadi angamiza
Wenye haki wabakie Nchi nzuri wawe nayo
Mafisadi wafutike kwa ajali wamalize
Nchi yetu nchi yetu mafisadi wanauza

Wananchi wamtaka SITA wetu Uspika
Mafisadi chakachua wameweka vibaraka
Wanawake wanafaa kumbe nao mafisadi
Nchi yetu nchi yetu mafisadi wanauza

Tumesha wasoma mbeleni Makindakinda Kumuweka
Wanasema anafaa ni wakati wanawake
Wanawake kitu gani mbona chaguo Fisadi
Nchi yetu nchi yetu mafisadi waiuza

Bora angkuwa KIlango tungesema wameweza
Makindakinda kumuweka Mafisadi kuwalinda
Wanawake gani hawa mkakati twaujua
Nchi yetu nchi yetu mafisadi waiuza

Walipanga awe Chenge wengi wutu tukaguna
Wakaona watuvunge Makindakinda kumuweka
Huyu makindakinda ni wakwao wananchi tukatae
Nchi yetu nchi yetu mafisadi waiuza

Mkumbukeni kinda kinda enzi zile ni naibu
Tofaute yake na SITA hoja nzuri alipinga
Mafisadi kumuweka ni faida yao pia
Nchi yetu nchi yetu mafisadi waiuza

Nitamati nafikia ndugu zangu muwaase
Wawakilishi wasitoe kura zao kwa vibaraka
Bora sana MABERE kuliko kinda kinda wa mafisadi
Nchi yetu nchi yetu Mafisadi waiuza
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom