Sipendi kuona mume wangu anakosa hela, huwa nampa hela, je inatokea kwa wanandoa wote?

Emoj

JF-Expert Member
Oct 9, 2015
837
1,282
Habari wapendwa,

Naomba kwa wale wanandoa mnisaidie hapa kama ni kawaida kwa wanandoa ama ni nini? Namshukuru Mungu tulipata kuoana na mume wangu, kweli maisha ni mazuri tunafurahia ndoa yetu na watoto wetu pia.

Namshukuru Mungu pia amenipa mume ambaye sio mlevi wala mpenda starehe yaani inshort hela hachezei anafanyia vitu vya maana sana.

Kuna wakati tulifungua joint account ilivyofika kiwango tulikuwa tunataka tukakubaliana akazitoa na akafanyia kazi nzuri sana kwa uaminifu. Na pia mara nyingi nikiwa na hela ambazo najua sizitumii kwa muda huo nampa anafanyia biashara zake baadaye nikihitaji anazirudisha.

Kabla na baada pia ya kuolewa nina ndoto nyingi za mimi kufikia level fulani na nilimshirikisha pia na akalifurahia.

Sasa tatizo linakuja kwamba kweli mpaka leo karibia miaka minne sasa hakuna kitu nimefanya katika kuachieve ndoto zangu, nimepiga kihatua kidogo sana, hela naweka akiba inafikia kabisa kiasi nataka kutimiza malengo yangu but najikuta tu nimempa mume wangu bila yeye kuniambia nimsaidie.

Yaani niko hivi sipendi kuona mume wangu hana amani au akiwaza wapi apate hela au akiniambia hasara aliyopata katika business muda mwingine nachukua card yangu ya bank naenda kutoa hela zote nampa kwa kumwambia hii hela siko na kazi nayo na naona niweke huko kwa business yako so zitumie tu kule usirudishe. (But lengo langu ni kutaka tu ajisikie vizuri pamoja na hasara aliyoipata hela nyingine imekuja) na ukimpa anapeleka pale kwa uaminifu kabisa.

Hela ya matumizi akinipa kweli namrudishia sijui kwanini but naona tu kwanini nichukue hela wakati mahitaji madogomadogo ya nyumbani naweza toa hela na vile bado hatujaanza kusomesha so mahitaji sio mengi si bora hiyo hela aendelee kuizungusha kwa biashara.

Basi naona tu hivyo na nakuwa na amani. Weekend hii ilikuwa nikachukue frame ya kufanyia kabiashara kangu (hili hata sikumwambia kwamba nimeshapata frame) but juzi akaniambia habari ya kiwanja alichokiona mjini sehemu nzuri sana na kina title na alipokuwa anaongea anaonesha kabisa kwamba we real need that land.

Hakuniambia toa hela wala nini but mimi mwenyewe nikamwambia niko na pesa nikaenda bank nimetoa hela zote hadi za mtaji wa biashara yangu ninayofanya online nimempa. Nimebakiwa tu na 100k za kuniweka hadi mwisho wa mwezi nianze upya kusave .

Wapendwa jamani hii ni kwangu tu ama ni kwa wanandoa wote? Sifanyi chochote kuachieve my dreams but niko na amani sana ndani ya moyo wangu kwasababu my husband is so happy napenda tu kumwona ana furaha sitaki kabisa apate stress kisa hela au kisa mambo yake hayaendi vizuri.

Namuombea sana na pale naweza kutoa pesa natoa sana na pale pa kumencourage namuencourage sana na kwa mimi hakuna kitu mimi nimejifanyia and am happy.hii itakuwa ni nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndoto zilikuwa zako ulipokuwa single sa hivi umeolewa ni zenu coz ninyi sasa ni mwili mmoja so kama kuna vitu viko achieved those are your dreams satop saying hujaachieve dreams zako

Umesema kila ukimpa mumeo anafanyia kitu mlichopanga kwa uaminifu na wewe uko happy hujihisi kupungukiwa chochote and your family is happy what is it that you need to worry???
 
Mpo wachache sana na mumeo akikuacha ataishi maisha ya tabu sana huk aendako kwa maana katika sayari hii kupata mwenza kama wewe ni vigumu sana.

Wangu anatabia kama zako mpaka huwa ninamuomba Mungu tuishi pamoja na kifo ndio kitutenganishe kwa maana nikienda sehemu nyingne nitapata shida ,

Wengine hawajui kukosa kwa mume wao wanataka kodi ya meza tu daily ukiacha kidogo wananuna bila sababu ya msingi.
 
Ni bora uwe na amani huku ukiwa na njaa kuliko kuwa kwenye vita ukiwa umeshiba. Hizo dream zako ndio zipi? Mimi naona kama umeshaolewa na una amani kwenye ndoa hiyo ndio dream pekee kwa mwanamke mambo mengine waachie wanaume.
Mimi nnachoona kuna kitu kinakusumbua kwenye akili yako na kuna jinsi umeshamchoka mume wako kwa kisa cha kuumpa hela. Huo ni ubinafsi kama ukiamua kusaidia saidi kwa moyo mmoja ni sawa na kutoa sadaka unatoa mfuko mmoja huku mfuko mwingine ukiwa hauoni.
Wewe ni mwanamke heb jaribu kuwa mwanamke achana na madream kwenye maisha. Unaweza ukawa unatimiza hizo dream huku huna mume wa kueleweka utaishi maisha mabovu kuliko hayo. Mshukuru Mungu kwa kile alichokupa hayo mengine achana nayo.
 
Ushatimiza ndoto zako ndo maana huna haraka,... Ila kama ni vitu vingine ungependa kufanya mshirikishe mumeo, mwambie na wewe ungependa kufany hiki na kile,..nadhani atajivunia pia,kwa sabab ameshampata mwanamke msaidizi kwa nn na yeye asimsaidie,..itakua roho mbaya,Mumeo atakusikiliza we ongea nae muyajenge,
 
Hongera Emoj,
Kama nimekuelewa ni kwamba unajihisi wewe sio mkamilifu au uko na utofauti na wanawake ingine....ni kweli una moyo wa kipekee na mapenzi yasiyo na mfano wake.

Jaribu kuongea na mumeo, mweleze yote haya uliyosema hapa...ataelewa ni jinsi gani ungependa akushike mkono uweze kufanya vile ndoto zako zinakutuma.

Inawezekana hajui kama unakitu hujamalizia kukifanya ndio maana hawezi kukataa support yako.

It's time to Turn The Tables Emoj.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom