Sipendi kuishi sehemu moja muda mrefu, je nina tatizo? Hata kazi kila baada ya miaka 4 inaniboa natamani nihame

Mkuu naamini hii tatizo litaisha tu pale utakapojenga kwako,

Hakika na mimi hili janga ilinisumbua sana mi ndani ya miezi mitatu lazima nilikuwa nahama na kodi pia naacha hata ya miezi miwili hadi mitatu,na cjui ilikuwa ni ujana inanisumbua au nn maana nilikuwa napachoka sana tu mazingira

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu wenye tabia za umalaya huwa wapo hivyo wakiume na wakike wanapenda kuhamahama
 
Mm Nina miaka 6 kazini tangia nuajiriwe ila nimeishapanga Zaid ya nyumba 7. Hii ya nyumba ya saba saiz ndio naenda kukamirisha mwaka .
Sehem Kama nne ivi nimeish mwaka mmoja mmoja ,zingine ni miez.

Sema mm nahama kwa matatizo ya hizo nyumba .

Nyumba ya kwanza niliondoka sabab ya mdada fulan tulikuwa tunaish nae sasa alikuwa mkorof balaa alaf hatak kununua umeme ,mkinunua anawasha Brenda inaunguruma tu alaf anasepa ,Sasa mwamba nikona huyu furaha yake ni kutukomoa basi nam nikamla mdogo wake ambae alikuwa anaish nae na ndie roho yake na dogo alikuwa haelew kitu kuhusu mm hata aongee vipi dogo bado alimchana dada ake kuwa namwelewa sana jamaa .Basi baada ya kuona hivyo alianza kunisukia mipango ya kuniwekea dawa kwenye maji ,ikabid nihame.

Sehm ya pili niliibiwa kila kitu nikiwa rikizo niliporud ikanibid nihame.

Sehem ya tatu baba mwenye nyumba akawa ananituhumu et namla mke wake wakat mm sikuwah hata muwaz yule mdada sema tu nilimchukulia Kama dada angu sasa ule ukaribu jamaa akawa na wivu had niakona nisepe hapa maana alinitangazia vita kitaa na ukichek ana mkwanja mrefu .

Sehem ya nne ,umbea wa majiran yaan ukileta tu manzi wao Wana note kwenye daftar then wanakutangaza kitaa nikaona hapanifai.

Sehem ya tano baba mwenye nyumba alikuwa kauzu sana nikaona hapanifai hapa

Sehem ya sita nilienda mbali kabisa na mji ili nione itakuwaje lakin huko nilikaa mwez mmoja tu nikarud mtaan kwangu

Sehem ya saba ndio nipo had saiz na hapa sitegemei kuhama ingawa Kuna kiroho fulan kilianza kuniambia nisepe hapa lakin hapa siham had siku naingia kwenye kibanda changu ambacho nipo nakijenga .

Kwahiyo mm naona Kuna namna haiko sawa kabisa either kuna mambo yanatuendesha bila kujua or Kuna watu washatufanyia tayal kuwa tutakuwa watu wa ivo .

Ila Kama Kuna uchaw washindwe kabisa pia Kama ni mambo ya nyota aisee hii nyota izimike kabisa ije nyota nzur, maana mm nina tatizo hilo had kwenye mahusiano siwez dumu na mtu kwa miez mitano bila kuzinguana haijawah tokea ,yaan siipend hi hali ila ndio inakuja bila kutarajia.
 
Back
Top Bottom