Sipendi kuishi sehemu moja muda mrefu, je nina tatizo? Hata kazi kila baada ya miaka 4 inaniboa natamani nihame

FRESHMAN

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
8,822
33,526
Habari wadau..

Mimi ni kijana early 30, najihisi nina tatizo la kuboreka.. nikifanya kitu kimoja muda mrefu, nikikaa sehemu moja muda mrefu, au nikikaa na watu fulani muda mrefu nahisi naboreka.

Nashukuru Mungu kipato kidogo napata cha kuniwezesha kupanga nyumba zenye privacy ila kila baada ya miaka mitatu hadi minne nachoka hilo eneo natamani kuhama na inatokea nahama.

Kazi pia nafanya sekta binafsi hivyo hivyo nikifanya majukumu ya aina moja miaka mitatu naichoka hiyo kazi naanza kutafuta ingine nikipata nasepa hata kama hakuna shida yeyote.

Na hata biashara nikifanya miaka kazaa mfululizo naichoka kama inalipa huwa naajiri kijana aendelee nayo, huku mimi na mmonitor na kumsaidia ikibidi najaribu kabiashara kengine hata kama hako kingine hakalipi.. najikuta nakapenda tu.

Je, mimi ni mzima kweli?
 
Kwaio mpaka hapo ulipo umbadili kazi ngapi? Biashara ngapi na nyumba ngapi?
 
Mi pia nipo hivyo hata Kama ni mahusiano itakuja tu hali itakua inanisukuma niachane na uyo mtu na nitafanya juu chini niachane with no reason yaan. af badae naanza kujilaum....kuna mtalaam mmoja akiniambia ninanyota ya upepo so ningum kutulia sehem moja
 
Nna tatizo kama lako mkuu ila mimi huwa nachoka wanawake siwez kaa na mwanamke miez 6 ntamchoka tu...
 
Back
Top Bottom