Sipendi kuamini lakini ndivyo ilivyo kwa mh. Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sipendi kuamini lakini ndivyo ilivyo kwa mh. Kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sammosses, Jan 12, 2012.

 1. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #1
  Jan 12, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Ni hatari kubwa sana kwa nchi hii kujidhihirisha kuwa haina viongozi wazalendo,hatari hii si ndogo kama ukikaa chini ukatafakari kwa kina juu ya mustakabali wa nchi yetu na aina ya viongozi tulionao.Nchi inaendeshwa shaghalabaghala kama haina wenyewe(wananchi).Napata mashaka juu ya uongozi wa mh rais JK kama kweli ni chaguo la Mungu kama tulivyoaminishwa na viongozi wa taasisi za kidini kuwa nichaguo la Mungu.Wakati mwingine najiridhisha na maneno ya mwalimu JK Nyerere aliposema muda wa kijana huyo kwa kipindi hicho ulikuwa bado.Naamini mwalimu alitumia hekima kubwa kumkata JK kwa kujua mapungufu yake!Mwalimu alijaribu kuelezea sifa za kiongozi atakayefaa kuchaguliwa natakiwa awe na sifa zipi bila kutaja majina,lakini leo hii kama muongo mmoja umepita maneno ya mwalimu yanajidhihirisha.

  Mh Mkapa wakati anapitisha jina la JK,alishindwa kuvaa viatu vya mwalimu wake,kwa kushindwa kutoa ushawishi ikibidi zaidi ya ushawishi alioutoa mwalimu wake katika kupitisha jina la mgombea atayefaa kumpasia kijiti kama falsafa yake ilivyokuwa ikitamka.Leo hii taifa linakwenda wapi?Amiri jehsi mkuu na mkuu wa majeshi yote anakosa uthubutu wa kufanya maamuzi magumu katika mambo magumu yanayo husu mstakabali wa maendeleo ya taifa hili.Rais aliyepewa madaraka makubwa kikatiba anashindwa kukemea maovu yanayo tendeka ndani ya utawala wake hii ni hatari kwa taifa hili.Tumlaumu nani,ikiwa wananchi wanalalamika na serikali inalalamika?Tuna lwenda wapi katika sayansi na teknlojia ndani ya duinia hii!

  Sipendi kuamini japokuwa ndivyo ilivyo,serikali makini na kiongozi makini kukosa watendaji makini watakaoweza kusimamia maslahi ya umma uliowaweka madarakani.Inaniwia vigumu kuamini kama kweli ndani ya miaka kumi ya maandalizi ya kuingia madarakani kwa kuomba ridhaa ya wananchi mh JK hukuwa umeandaa safu ya uongozi katika kukusaidia kutuonyesha njia.Na kama ulikuwa nasafu ulikwisha iandaa ukiamini watakusaidia kuleta chachu ya maendeleo katika taifa hili lakini ghafla wamekugeuka unashindwa nini kuwawajibisha,mbona watanzania ni wengi tu ambao ni wazalendo na waadilifu kwa nchi yao!Ulipoanza kwa kauli kali kuwa serikali yako haina ubia na mtu,huku ukitembelea wizara mbalimbali baada ya semina elekezi,tuliamini kijiti alichokuachia Mh. Mkapa kilikustahili,sipendi kusema ilikuwa ni nguvu ya soda bali maneno na vitendo vyako vinathihirisha wazi kuwa ilikuwa ni nguvu ya soda huku ukifunika kombe mwanaharamu apite.

  Tunakwenda wapi,napata wakati mgumu wakati mwingine kuchambua hotuba zako,haiingii akilini katika utawala bora tena utawala wa nchi inayofuata sheria kwa waalifu kupewa muda wa kujisafisha.maana yake nini,ni kuwaogopa walengwa ambao kwa namna mmoja ama nyingine watakuwa na hisa na serilkali yako.Wapinzani wamesema sana,wananchi wamepiga kelele sana juu ya ufisadi wa mali ya umma lakini kweli nimeamini kelele za chura hazimzuii tembo kunywa maji.Nchi ina lalamika wewe umeweka pamba masikioni rasilimali zetu zinakwenda kama nchi haina wenyewe ni hatari sana.Watendaji wakuu serikalini wanaitilafiana kwenye media aibu iliyoje!Hivi vile vikao vyenu vya baraza la mawaziri vinafanyika ipaswavyo au vimekuwa ni kijiwe cha kugawana majukumu ya ksimamia uuzaji wa nchi tuliyopewa na Mungu.

  UPOLE
  Ulipoapishwa ulituaminisha katika moja ya hotuba zako kuwa tusihadaike na tabasamu lako,upo firm kwa mambo ya msingi.Kwanini lakini hupendi kutembea kwenye maneno uliyoyatamka kwa kinywa chako!Ukali uko wapi?Mbona unapenda lawama toka kwa wananchi waliokuchagua kwa kushindwa kusimamia yale waliyoyaamini tuyasimamia kwa udhabiti na kiwango cha ahali ya juu.Si kweli kuwa watangulizi wako walikuwa wema sana la hasha bali walithubutu kusimamia walichokiamini,lakini wewe umeonyesha udhaifu hata kwa yale uliyoyaamini kuwa ungeweza kuyasimamia.Ni mengi sana lakini kubwa ni hili la ubia juu ya urais wako.Hata simba akizeeka vipi kamwe uwezi mshika sharubu zake,sasa kwanini wewe unaruhusu hali hii inajirudia rudia nawe umenyamaza kimya!

  AMRI
  Amri inapotolewa na mkuu wa nchi ni zaidi ya sheria,lakini amri zako zimekuwa ni mchezo wa kuigiza,wakati mwingine ninazifananisha na joka la kibisa.Ni mara ngapi mh.Kila unachaagiza akitekelezwi nawe upo kimya tu.Tangu upige marufuku uzio wa mabati jangwani leo ni muda gani upita mpaka mabati yametolewa na mafuriko.Sipendi kuamini hiyo njia hupite tangu ulipotoa agizo hilo.Ububu huu hata kwa mambo ya msingi mpaka lini.

  MGONGANO WA MADARAKA
  Kuna mihimili mitatu ya dola kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.kuna serikali,bunge na mahakama.Imekuwa ni kawaida hasa katika kipindi cha utawala wako mihimili hii kulumbana tena malumabano yasiyo na tija.Mgawanyo na madaraka ya mihimili hii mipaka yake ipo wazi,kwanini serikali yako ina yafumbia macho malumbano haya yasiyo na tija.Matokeo yake mhimili mmoja unaamua kuuingilia majukumu ya rais kujipasishia posho na rais wa nchi amenyamaza kimya.Tuweke wazi basi kama kuna watu wanakupa mashinikizo sisi ndiyo tuliokupa dhamana tutawawajibisha kuliko fedheha hii mbele ya waajiri wako (wananchi),Au ndo kusema kasungura kenyewe kadogo mnagawana kimya kimya?Bunge linatoa mapendekezo likiwa kama msimamizi wa serikali,serikali inakaidi mapendekezo halali ya bunge kwa kuweka pamba masikioni, wapi tunaelekea.

  MIRADI HEWA
  Napenda kuita ni miradi hewa kwasababu haina tija kwa maendeleo ya nchi na watu wake.Ni kawaida kabisa kwa nchi yeyote duniani kufanya jubilee na kupima mafanikio na mapungufu katika miaka kadhaa iliyopita,lakini hapa kwetu ni tofauti na dhana hii.Sherehe za kutimiza miaka hamsini ya uhuru wetu inasikitisha kwa gharama zisizolezeka mpaka sasa.Gharama hizo zingitumika kununulia vitabu vya mitaala katika kufundishia tungekuwa wapi kimaendeleo.Huwezi amini ndani ya miaka hamsini katika teknolojia ya sayansi watoto wetu bado hawana madawati ya kutosha.Hata hayati JF kennedy aliwahi kusema usiulize marekani iatkufanyia nini,bali jiulize wewe utaifanyia nini marekani,wakati huo anahutubia wananchi wake.tukirudi hapa kwetu tunalipa kodi,je malipo ya kodi zetu ndo sherehe zisizo na tija kwa taifa hili?Kulikuwa na haja gani kwa serikali kutumia nguvu kubwa kuazimisha sheria hizi kwa kila wizara kuandaa sherehe zake kabla ya tisa desemba kama si ufisadi mwingine zaidi ya ule wa Richmond.Je ni kweli raisi wetu haya huyaoni au ndo remote control inafanya kazi?

  Mwisho,rungu tulilokupa ulitumie,unaliogopa,madaraka na uwezo mkubwa kisheria tuliokukabidhi unauogopa?Fanya maamuzi magumu,sipendi kuamini hata ikatokea nikakuliza unataka Watanzania wakukumbuke kwa lipi utashindwa kujibu kama ulivyoshindwa kulijibu swali hili toka kwa mwandishi mmoja tarahe 31/10/2010.Ule ubia uliosema huna mbona hutonyeshi kwa vitendo.Wezi wa rasilimali yetu wataendelea lini kula upepo mwanana ili hali magereza yamejengwa kwaajili yao.Rudisha imani na heshima ya kwa wananchi,imani waliyokujenge mwaka 2005 leo hii iko wapi. Mungu ibariki Afrika Mungu ibariki Tanzania
   
 2. Kikarara78

  Kikarara78 JF-Expert Member

  #2
  Jan 12, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,164
  Likes Received: 514
  Trophy Points: 280
  Sammosses na Wana JF,
  Umetueleza vizuri, je ujumbe umefika ?? Usikute unampigia Mbuzi gitaa, hivi unaweza kumkataza mtoto wako au yeyote asivute sigara, bangi, kufanya mabaya na huku wewe unafanya hayo hayo ??? Unafikiri utakuwa na Nguvu, Uwezo wa kumkanya.
  Tatizo ninaloliona kwenye mada hii ni Madaraka makubwa aliyonayo Mkuu wetu wa kaya na hili tatizo lipo kwenye Katiba ya Nchi.
  Nawakilisha


   
 3. R

  RMA JF-Expert Member

  #3
  Jan 12, 2012
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 409
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kikwete ndio chaguo la Mungu ili watanzania mjifunze!! Ni vema maisha yaendelee kuwa magumu zaidi ili mpate akili. Safari nyingine msifanye ushabiki wa Yanga na Simba katika siasa bila kutazama uhalisia wa mambo! Mnapiga kura kama vipofu halafu mnalalama kama vichaa!

  Maisha duni kwa kila mtanzania ni haki yenu! Mnastahili kwa kuwa huyo rais mnayemlalamikia ni ninyi mliomchagua!
   
 4. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #4
  Jan 12, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  This is very correct. Chaguo la mungu. Sijui yeye atatuachia chaguo la nani.
   
 5. Mkondakaiye

  Mkondakaiye JF-Expert Member

  #5
  Jan 12, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 839
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Maisha bora kwa kila mtanzania haiwezekani, nguvu zaidi, ari zaid na kasi zaid ya ufisadi, inawezekana
   
 6. H

  Haika JF-Expert Member

  #6
  Jan 12, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Rais wetu yuko makini sana. Jasiri sana jamani.
  Ila tu ni kwenye kulinda na kucreate fursa kwa watu wake, anajenga heshima sana kwa watu wake, nyie mlioko nje ya mzunguko wake poleni.
   
 7. M

  Maengo JF-Expert Member

  #7
  Jan 12, 2012
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ' Wengine wataingia ikulu kwa uzuri wa sura zao'
   
 8. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #8
  Jan 12, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,601
  Likes Received: 18,612
  Trophy Points: 280
  Ni kweli JK ni chaguo la mungu na Lowassa ndiye chaguo la Mungu!, hivyo JK ambaye ni chaguo la mungu, anatuachia Lowasaa ambaye ni chaguo la Mungu!.
   
 9. P

  PATALI Member

  #9
  Jan 12, 2012
  Joined: Dec 11, 2011
  Messages: 88
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Duh..watu tunaanza kujiuliza haya mapenzi uliyonayo kwa EL ni bahasa tu kweli?
   
 10. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #10
  Jan 12, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  la wanamonduli ndio atawaachia watanzagiza..
   
 11. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #11
  Jan 12, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  ndivyo ilivyo mambo ya kifalme zaidi....
   
 12. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #12
  Jan 12, 2012
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,151
  Likes Received: 3,340
  Trophy Points: 280
  Kikwete hakuna kitu pale.. Angalia jinsi anavyotumia mabavu kwenye mambo madogo kama migomo vyuoni.
   
 13. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #13
  Jan 12, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  It is very correct....tuliokuwa tunampinga huyu mhe. kwa kujua uwezo wake ulivyo hohe hahe kiuongozi tulilionekana vibaraka wa ibilisi. Mungu ni mwema hukubaliana na utashi wa mwanadamu....tuache kulalama, Mungu anatupitisha shule ili tujua kiongozi ni nani na mcheza bao ni nani.
   
 14. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #14
  Jan 12, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,676
  Trophy Points: 280
  Kuna mtu alisema huyu mtu anacheka hata msibani!
   
 15. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #15
  Jan 12, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ebwana,duh
   
 16. mwaJ

  mwaJ Tanzanite Member

  #16
  Jan 12, 2012
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 4,076
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Ha hahahahahaaaa, Pasco usilete usanii hapa! Yaani mmoja ni chaguo la "mungu" na mwingine ni chaguo la "Mungu" wenye akili na watambue!
   
 17. kanta

  kanta JF-Expert Member

  #17
  Jan 12, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 343
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Mwalimu aliwahi kumkebehi JK wakati flani mwaka 2005, akijibu swali la mwandishi mmoja wa habari alisema kama kuna mgombea unampenda kwa sababu ya sura yake basi mchukue mkanywe nae chai.Sasa hao waliokuwa wanampenda JK walitakiwa akanywe nae chai badala ya kumpeleka ikulu ambako ameshindwa kutekeleza majukumu yaliyompeleka pale.
   
 18. fyddell

  fyddell JF-Expert Member

  #18
  Jan 12, 2012
  Joined: Dec 19, 2011
  Messages: 2,082
  Likes Received: 774
  Trophy Points: 280
  Inawezekana Mungu ndo anatufundisha ili baadae tusifanye makosa katika kuchagua kiongozi wa nchi.
   
 19. H

  Huihui2 JF-Expert Member

  #19
  Jan 12, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 395
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Yule JK siyo kwamba anacheka kama tunavyodhani! La hasha, bali ni mlemavu wa mdomo. Lips zinaachia zenyewe kwa vile kuna tissues muhimu zimekufa. Hacheki wala hatabasamu, Tumsamehe bure
   
 20. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #20
  Jan 12, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  Jk hana tofauti na mti wa ASHOK( maarufu kama MU ashok)........mti huu haufai kwa kivuli..huwezi kutengeneza mbao kwa ajili ya fenicha...huwezi kujengea nyumba..huwez kuufanya kuni na upikie..haufai kuwa mkongojo..zaid sana mti huu huwa ni pango na makazi ya wale nyoka wa kijan..ndivyo alivyo kikwete
   
Loading...