Sipendezwi na tabia ya viongozi kuwatuma walemavu kuomba omba maofisini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sipendezwi na tabia ya viongozi kuwatuma walemavu kuomba omba maofisini

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Andindile, Aug 4, 2009.

 1. Andindile

  Andindile JF-Expert Member

  #1
  Aug 4, 2009
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kumezuka tabia chafu sana kwa viongozi wa manispaa ya kuwaandikia walemavu vijikaratasi ili wazungukie maofisini kuomba misaada mbalimbali. Mfano leo amenitembelea mlemavu wa mguu ambaye alikuwa na form iliyosainiwa na kiongozi manispaa ya Kinondoni ili achangiwe fedha zifikie sh. 85,000 akanunulile mangongo ya kutembelea. Kwa kweli imenisikitisha sana kwa jinsi ambavyo anasumbuka kuzungukia ofisi mbalimbali. Nilipochungulia list ya wanaotoa, wanaweka sh. 500, 1000 au 2000. Itamchukuwa mizunguko mingapi mpaka afanikishe hiyo 85,000?

  -Nimejiuliza, hivi Manispaa haina mfuko wa ustawi wa jamii kuwasaidia watu wenye shida kama hizo kuliko kumpa shida mtu ya kuzunguka ofisi mbali mbali kusaka 85,000 ya mangongo?
  -Kuna walemavu wengine ambao ulemavu wao si kikwazo cha kuwazuia kuendesha baadhi ya shughuli ndogondogo za kujipatia kipato, hivi halmashauri zimeshindwa hata kutoa upendedelo kwa walemavu ili wauze hata vocha au kibiashara chochote kwenye maeneo yenye msongamano wa watu mfano stendi ya mwenge, ubungo, kariakoo n.k ili wajipatie kipato kwa kuendesha shughuli zao badala ya kuombaomba?
  -manispaa zifike mahali zionyeshe mfano kuwa ukizaliwa mlemavu au hata ukiupata ukubwani kwa sababu mbalimbali, utaishi maisha ya heshima na staha na furaha badala ya ilivyo hivi sasa ambapo ukiwa mlemavu ujue kuwa maisha yako yatakuwa ya kilio na kusaga meno

  nawasilisha
   
 2. Wa mmoja

  Wa mmoja Member

  #2
  Aug 5, 2009
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndio Tanzania yetu ilivyo mkubwa!!
  Vitu vingi vinahitaji mfuko kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya kila siku lakini tatizo ni utekelezaji...Mfuko unaweza ukaanzishwa baada ya siku chache utasikia mafisadi wanaunyemelea...Viongozi wanalitambua hilo lakini tatizo linakuja kwenye utekelezaji...Muheshimiwa wa nchi mwenyewe anawaona huko posta hao omba omba walivyojaa,sidhani kama huwa anapita kwa mwendo wa kasi sana kiasi cha kutowaona...!Imeshindikana ajira kwa kila Mtanzania hii ndo itawezekana??!
  Tuwasaidie tu pale inapowezekana kwani tukisema tusubiri huo mfuko uanzishwe,tutangoja hadi siku ya kiama!
   
 3. m

  maembe Member

  #3
  Aug 5, 2009
  Joined: Jun 4, 2009
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nchi inakwenda kama tren isio kua na breki kwenye mteremko mkali hawawezi kuweka mambo kama hayo ya maendeleo. kwani kila kiongozi akipewa madaraka anakuja na namna yake na mawazo yake .hakuna master plan kwamba kila mtu anafata au anatakiwa kuboresha. we ukipewa madaraka unaanza kufanya kazi kama unavyotaka wewe.hakuna wa kuuliza na kama ikionekana unamawazo mazuri uwatafanya kila namna wakuhamishe au uachisheswe kabisa kazi.
  hii ndio tanzania zaidi ya uijuavyo sijui lini tutafika kweli
   
 4. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #4
  Aug 6, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Sasa hawa ustawi wa jamii wanafanya nini?
   
Loading...