Sipati umeme siku ya tatu leo, tatizo ni nini?

mkayeye

New Member
Oct 28, 2015
2
0
Luku hipo lakini umeme auwaki tatizo ni nini arafu nilikuwa naongeza luku nikajua imeisha inasomaa arafu aimarizi inazima leotena nimejaribu kuuhingiza ule umeme naambiwa umeshatumika lkn umeme auwaki tatizo ni nini?

TANESCO
 
tafuta fundi ahakikishe wiring yako ipo sawa na ikiwa ipo sawa wapigie tanesco kituo cha luku kwa msaada zaidi 0768985100
 
Ita tanesco waje...watakuombea namba za kufungua mita....ila kabla ya hapo hakikisha unamuita fundi arekebishe shoti ndan kwako nd uziweke hzo namba....kiufupi kuna shoti...hasa hizo soket hizo
 
Unatumia mita luku ya namna gani? Kama Ni Ile ya remote taa nyekundu inawaka kwenye temper Basi nyumba Ina shot mahali ..ita fundi akague halafu wapigie Tanesco wakupe number ya kufungulia..imenitokea majuzi nikasolve

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Hivi hata kama mtu hujamaliza chuo, huu uumbaji wa Herufi na Uundaji wa Sentensi si tulifundishwa Darasa la Pili hapo Mbugani Shule ya Msingi!? Wewe Urikuwa Wapi!!!?
 
Luku hipo lakini umeme auwaki tatizo ni nini arafu nilikuwa naongeza luku nikajua imeisha inasomaa arafu aimarizi inazima leotena nimejaribu kuuhingiza ule umeme naambiwa umeshatumika lkn umeme auwaki tatizo ni nini?
Luku yako ndio yenye matatizo, unit za umeme haziwezi kutumika bila wewe kutumia umeme, kwa hivo basi, wasiliana TANESCO kitengo cha luku wakubadilishie mashine nyingine ya luku.
 
hujaeleza vizuri nafikiri tatizo ni pale juu kwenye nguzo ya nyumba yako umeme unapoingilia carbon imejaa inakata umeme muite fundi akuweke clemp kwenye waya zako pale juu kwenye nguzo
 
Back
Top Bottom