Interest
JF-Expert Member
- Apr 11, 2015
- 3,433
- 7,055
Kipindi msanii huyu ana-hit na ngoma zake zile Latifa na Mapenzi Kitu Gani alifunguka kwamba anampenda Nancy Sumari na anatamani awe hata mkewe wa ndoa.
Kwa namna jamaa alivyokuwa juu, si rahisi kwa mdada yeyote kuchomoa ofa ya kuwa naye. Warembo walimpapatikia sana na ofkoz alitawala wingu la Bongo Fleva. Historia inakumbuka.
Na enzi hizo Nancy ndio alitoka kunyakua ushindi wa Miss World Africa.
Jamaa akashindwa kujizuia. Kila akihojiwa akawa anasema wazi anamzimikia sana Nancy Sumari. Na ndoto zake zitatimia akifanikiwa kumnasa maana lengo lake halikuwa kumchezea bali kumuoa kabisa.
Kama haitoshi, Doggy Man akarekodi wimbo mahususi kwa ajili ya Nancy akafunguka ya moyoni. Ngoma ilihit sana kwa wanaoikumbuka. Iliitwa "Ina maana".
Sikumbuki kama Nancy alizungumzia chochote.
Leo nimemuona Nancy sehemu nikawaza laiti angemkubalia jamaa wawe couple wangekuwaje leo hii? Kama angemkubalia kwa sababu ya umaarufu, wangedumu kweli?
Shubaamita!
Sent using Jamii Forums mobile app